Wednesday, August 27, 2014

CAPITAL ONE: MAN U YAPIGWA KIPIGO CHA MBWA MWIZI NA KITIMU CHA MCHANGANI,GIGGS AMWAGA CHOZI

Wachezaji wa MK Dons wakishangilia bao lao la kwanza
Analia: Kocha Msaidizi Ryan Giggs akiwa ameshika kichwa akilia kwa uchungu mwishoni mwa mchezo huo, huku kocha Louis van Gaal akiwa haamini macho yake
Wachezaji wa United wakiwa hoi baada ya kipigo

KOCHA Louis van Gaal ameendelea kuogelea katika bwawa la maji moto Manchester United, baada ya usiku huu kfungwa na Mk Dons ya Daraja la Kwanza mabao 4-0 katika michuano ya Kombe la Ligi, maarufu Capital One. Mabao yaliyomtia machungu Van Gaal leo yamefungwa na Will Grigg dakika ya 25 na 63 na Benik Afobe anayecheza kwa mkopo kutoka Arsenal dakika ya 70 na 83. Kocha Msaidizi Ryan Giggs alionekana kufuta machozi baada ya bao la tatu, akiwa kwenye benchi na bosi wake, van Gaal. Kikosi cha MK Dons: Martin, Baldock, Kay, McFadzean, Lewington, Carruthers, Potter, Reeves, Alli, Bowditch, Grigg. Subs: Green, Spence, Randall, McLoughlin, Powell, Hitchcock, Afobe. Man Utd: De Gea, Vermijl, Evans, Michael Keane, James, Janko, Anderson, Kagawa, Powell, Welbeck, Hernandez.

0 comments:

Post a Comment