Tuesday, October 07, 2014

SHILOLE AKUTWA NA DOGODOGO NYINGINE...NUH MZIWANDA HANA CHAKE TENA

Baada ya kutokuwa na maelewano mazuri kati ya nuhu mziwanda na mpeni wake shilole hivi sasa tetesi zimeibuka upya kwamba wawili hao hawako pamoja tena , hii imefatia kuzagaa kwa picha ambayo shilole amepiga akiwa na njemba mmoja ambaye jina lake halikupatikana mara moja,

PICHA UJIONEE TEAM YA AKILI ZA USIKU ... WENGINE WAKIWA WAMELALA WENGINE WANAFANYA KUFURU NA ANASA

BALAA, NABII JEREMIAH ATANGAZA KIAMA,AWATAKA WAGANGA WA KIENYEJI WAJISALIMISHA.. ATOA SIKU 14

Dokta Manyaunyau ambae ameombwa kuwa wa kwanza kujisalimisha kwake kutokana na matatizo makubwa aliyokuwa nayo. Na Mwandishi wa Maskanibongotz Katika hali isiyokuwa ya kawaida Nabii Jerry wa kanisa la Holly Ghost Fire lilipo Mbezi Juu kwa Temba Jijini Dar ametoa mpya baada ya kuwatangazia kiama waganga wote wanaotumika kwa ushirikina pamoja na wachawi kujisalimisha kanisani kwake mara moja kabla moto wake haujatua kwenye vichwa vyao. Akiongea na waandishi wa habari mbalimbali Kanisani kwake mwishoni mwa juma Nabii huyo alisema kuwa katika maono yake amegundua jinsi gani waganga wa kienyeji baadhi na wachawi jinsi wanavyoaathiri maisha ya wakazi wa Jiji. Nabii Jerry aliongeza kusema" Natamka hadharani mbele ya vyombo vya habari juu ya hawa waganga wakienyeji na wachawi nawatangazia vita juu yao na natoa siku 14 wawe wamejisalimisha mahara hapa kwa ajili kuchoma hizo tungur zao na endapo watakiuka maagizo haya basi moto wa injiili utawafanya vibaya na kuumbuka kwenye jamii" Alisema Nabii Jerry Mtumishi huyo wa Mungu amekuwa na kalama ya kipekee huku maelfu ya wananchi wakimiminika kanisani kwake kwa ajili ya kupata msaada wa haraka, na amekuwa kati na manabii tofauti kwenye kutoa huduma ya maombi nchini kwani yeyey humuombe mtu na kuponywa ugonjwa wake papo hapo na sio longolongo. Aidha nae Mtumishi huyo hakusita kutoa uwito kwa wakazi wote wa Jiji la Dar kuendelea kumiminika kwenye Huduma yake kwa ajili ya kazi moja tu ya Uponyaji na maombi maalum na hii ndiyo namba yake ya huduma kwa maombi +225713-976786 Na ratiba zinaanza kila siku za Jumatano, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi, ni saa kumi jino na Jumapili ibada inaanza saa tatu asubuhi hasi saa saba mchana. Na tayari maamia ya watu wamefungulia maradhi yao hadi sasa wako huru kila hitaji kwake linafanikiwa kwa kipindi kifupi na huo ndiyo moto unavyofanyakazi kwa Mchungaji huyo. CDT: XDEEJAYZ

Dully Sykes: ‘Hakuna rapper wa Bongo anayefikia utajiri wangu’, Fid amjibu

Msanii mkongwe wa muziki nchini, Prince Dully Sykes amefunguka kuwa hakuna msanii wa Hip Hop hapa Tanzania anayemfikia kwa maendeleleo. Dully ambaye anamiliki studio pamoja na vifaa vya muziki aliongea hayo mbele ya Fid Q. “Kwa hapa nilipofikia na uwezo na mali nilizokuwa nazo hakuna mwana hip hop anayenifikia. Umaskini mliokuwa nao ni mwana hip hop gani anaweza akafikia uwezo wangu? Sio studio tu kwani mali ni studio peke yake!Katika mali zangu studio haipo, mimi ni mwanamuziki lakini wanahiphop ni maskini zaidi yangu mimi, siwezi taja mali zangu, kuna studio na home studio, wewe (Fid Q) una home studio,” alisema Dully kwenye maongezi ya kwenye basi la ziara ya Fiesta ambayo yalikuwa on the record (ruhusa kurekodiwa). Baada ya kauli hiyo, Fid Q ameiambia Bongo5 kuwa Dully hajui utajiri anaouzungumzia huku akidai kuwa wasanii wa muziki wa kuimba wanapewa nafasi kubwa kwenye muziki wao na ndio maana wanakuwa na kiburi. “Kwanza Dully ana utajiri gani kuliko wasanii wa Hip Hop? Mimi naona yupo kawaida sana. Sema wasanii wengi wa muziki wa kuimba wanapewa nafasi nyingi za kuonekana kuliko wana Hip Hop lakini sio kusema anawazidi utajiri,” alisema Fid Q. Unahisi Dully ameongea ukweli? Funguka.

Wiki mbili kabla ya kukutana na Yanga – Okwi apata majeruhi, Daktari azungumza

Zikiwa zimebaki takribani mbili kabla ya mchezo wa watani wa jadi Simba na Yanga, daktari wa Simba SC, Yassin Gembe amesema kwamba mshambuliaji, Mganda Emmanuel Okwi aligongwa kwenye enka na goti katika mchezo dhidi ya Stand United, lakini yuko fiti kabisa kucheza Oktoba 18, dhidi ya Yanga SC. Okwi alitolewa nje mara mbili kupatiwa huduma ya kwanza na Dk Gembe, lakini mara zote alirejea uwanjani kuendelea na mchezo. Pigo la pili lilimfanya mchezaji huyo aendelee kucheza huku akichechemea, hali ambayo ilizua hofu labda amepata maumivu makubwa. “Ni kweli Okwi aligongwa mara mbili, mara moja kwenye enka na mara moja kwenye goti. Lakini hayakuwa maumivu makubwa na ataendelea na mazoezi na wenzake” amesema Gembe Aidha, Dk Gembe amesema kwamba kipa Ivo Mapunda na beki Nassor Masoud ‘Chollo’ wataanza mazoezi ya kujiweka fiti wiki hii. Ivo aliumia kidole na anatakiwa kuwa nje kwa wiki nane, hivi sasa akiwa yupo katika wiki ya tatu, wakati Chollo aliyeumia mkono, anatakiwa kuwa nje kwa wiki tatu, hivi sasa akiwa anaingia katika wiki ya pili. “Hawa wachezaji maumivu yao hayawazuii kufanya mazoezi ya kujiweka fiti, kwa hivyo niliwapa mapumziko mafupi kabla ya kuanza mazoezi ya kukimbia na gym. Ivo nilimpa wiki mbili za kupumzika na Chollo wiki moja, kwa hivyo wote wiki hii wataanza mazoezi,” Issa Rashid ‘Baba Ubaya’ na Haroun Chanongo ambao wiki iliyopita walifanya mazoezi mepesi, nao wataanza mazoezi kikamilifu na wenzao. Majeruhi mwingine wa muda mrefu Simba SC ni Mkenya, Paul Kiongera ambaye anatakiwa kuwa nje kwa wiki sita baada ya kuumia goti, hivi sasa akiwa katika wiki ya nne- na Dk Gembe amesema ‘fowadi’ huyo anaendelea vizuri.

MAMBO YANAYOFANYIKA NYAKATI ZA USIKU DAR NI HATARI

kimemnasa msaidizi wa kazi za ndani (hausigeli) akifanya biashara haramu ya kuuza mwili kwa kisingizio cha mshahara kiduchu. Kushoto ni hausigeli akifanya biashara ya uchangudoa maeneo ya Sinza jijini Dar.Tukio hilo la aina yake liliingia kwenye kamera za OFM maeneo ya Sinza jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita ambapo msichana huyo wa kazi alikutwa kwenye harakati za kusaka wanaume ili kuwapa penzi kwa malipo. Mara baada ya kumnasa na kumlamba picha akiwa na wenzake ambao nao kama yeye walikuwa wamevaa nguo fupi yaani nusu utupu, alianza kuangua kilio hasa alipokuwa akihojiwa kwa nini anajihusisha na biashara hiyo hatarishi katika maisha yake. “Jamani mmenipiga picha mtanipotezea kazi yangu, jamani mimi nimeajiriwa, ni mfanyakazi wa ndani kwa mheshimiwa Mikocheni (Dar), nafanya kazi za ndani hii yote ni kujitafutia riziki nje ya kazi,” alilalama binti huyo aliyekadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 20 hadi 23.
Baadhi ya machangudoa wakiwa mawindoni.Binti huyo aliwaambia OFM kwamba alifikia hatua hiyo ya kujiingiza katika biashara hiyo ya ngono kutokana na ugumu wa maisha huku lawama akizielekeza kwenye mshahara kidogo wa kazi za ndani. “Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa shilingi elfu 50 kwa mwezi, nina watoto wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi nitafutieni kazi nitaacha kuuza mwili,” alisema. Alipoulizwa namna anavyotoka kwa bosi wake kwenda kujiuza, hausigeli huyo alisema kwamba huwa anakula dili na walinzi wa bosi wake usiku wakiwa wamelala anatoka na akirudi freshi anawakatia walinzi chao.
Machangudoa wengine wakizikimbia kamera.Alisema kuwa yeye analala katika vyumba vya uani kwa hiyo anapotoka waajiri wake hao inakuwa vigumu kumsikia kwani wanakuwa wamepitiwa na usingizi. Aliendelea kueleza kwamba kuna siku nyingine huwa anarudi nyumbani akiwa amevuna fedha nyingi kuliko mshahara wake. “Hii kazi yangu inaniingizia kipato kikubwa sana kuliko mshahara,” alisema hausigeli huyo.

 HABARI ZINGINE BOFYA HAPA 

MAHABA NIGALAGAZE: MREMBO HUYU APONZWA NA PENZI LA MGANGA..AFUKUZWA NYUMBANI KWAO! SOMA ZAIDI HAPA!

Ulozi? Mrembo aliyejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23), anadaiwa kufukuzwa nyumbani kwao kufuatia kuchanganywa na penzi la mganga wa kienyeji ambaye pia ni ustadhi aliyejulikana kwa jina moja la Zein. Mrembo anayejulikana kwa jina la Shaharzad Hassan Othman (23) anayedaiwa kufukuzwa nyumbani. Akizungumza na gazeti hili mara baada ya kutimuliwa kwao, binti huyo ambaye alikuwa akiishi na wazazi wake walezi maeneo ya Kariakoo jijini Dar alisimulia kwamba alifukuzwa kwao kwa sababu hakulala nyumbani siku moja wiki iliyopita na aliporudi wazazi wake walezi wakamtaka arudi alipotoka. “Baada ya kufukuzwa sikuwa na sehemu nyingine ya kwenda zaidi ya kuja kwa mpenzi wangu (Zein) maana ninampenda na siku si nyingi atanioa.

 HABARI ZINGINE BOFYA HAPA 

HUYU NDIO MWANAMKE TAJIRI ZAIDI AFRIKA MASHARIKI: CHEKI PICHA ZAKE HAPA

Charity begins @ home. On a charity day at katanga. Served the shelter with Easter lunch
At work
Party Zari diva always celebrating her life
Zari with her hubby

WABONGO KUNA MUDA HUWA WANAJITAKIA MATATZO WENYEWE,HUFANYA VITU KAMA WAMEKATWA VICHWA

Inapoelekea kwa sasa ni hatari maana kibao kimekataza kufanya biashara lakini yeye anafanya, sasa hapa lawama kwake au kwa waliokiweka? hii nimeipata maeneo ya Njombe jamaa akiendelea kuuza mahindi ya kuchoma

 HABARI ZINGINE BOFYA HAPA 

Rekodi 7 tofauti alizoweka Cristiano Ronaldo baada ya kufunga hat trick dhidi ya Bilbao

Mwanasoka bora wa dunia Cristiano Ronaldo jana usiku alifunga magoli matatu na kutimiza jumla ya magoli 17 katika michuano yote aliyoitumikia Real Madrid.
Magoli hayo yalimfanya Ronaldo aweke rekodi kadhaa kwenye historia ya soka na rekodi hizo zipo kama ifuatavyo:

*3 – Hii ni Hat trick ya 3 ya Ronaldo katika La Liga msimu huu na amefanikiwa kufunga hat tricks hizo katika kipindi cha siku 15 tu.

*111 – Mchezo wa jana usiku ulikuwa wa 111 kwa Ronaldo kuitumikia timu yake ya taifa au klabu na katika mechi hiz zote amefunga zaidi ya goli moja.

*Cristiano amekuwa mchezaji wa pili kufunga hat tricks 3 katika mechi 7 za raundi ya kwanza ya La Liga – baada ya Mariano Martin kufanya hivyo msimu wa 1943-44.

*Cristiano ndio mchezaji wa kwanza kufunga magoli 13 au zaidi katika mechi 7 za kwanza Liga – tangu alipofanya hivyo Echevaria katika msimu wa 1943.

*50 – Cristiano Ronaldo mpaka sasa ameshatoa assists 50 kwa wachezaji wenzie wa Real Madrid.

*190 – Magoli matatu aliyofunga Cristiano Ronaldo jana dhidi ya Athletic Bilbao yalimfanya atimize jumla ya magoli 190 katika mechi 171 alizoichezea Real Madrid kwenye ligi.

*9 – Gareth Bale mpaka sasa amempa Cristiano Ronaldo assists nyingi kwenye La liga tangu mwanzo mwa msimu uliopita – amempata assists 9.

MWANAFUNZI WA MIAKA 17 AMPA MIMBA MWALIMU WAKE MWENYE UMRI WA MIAKA 25.....KAMANDA WA POLISI ASEMA MWALIMU HANA KOSA KISHERIA!

WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu wake. Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu wake ana umri wa miaka 17, wakati mwalimu huyo anayefundisha katika Shule ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25. Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya jirani. Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa kupata mtoto katika umri wake huo mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni mtumishi serikalini. Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo, mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi wake bado anaendelea na masomo shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa kiume akifundishwa na mzazi mwenzake. Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini Namanyere hivi karibuni, Mkuu wa Shule ya Sekondari Nkasi mjini Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko ya umma, Amiamie Nanga alisema mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu chuoni. “Yameshatokea, lakini haileti picha nzuri sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa na wakazi wa mwambao wa Ziwa Tanganyika, kwao si ajabu kuwa na uhusiano na watu waliowazidi umri, iwe kwa mtoto wa kike au wa kiume, wote ni sawa tu… alisema. “Lakini katika kisa hiki, inaonesha walimu sasa wanapoteza haiba ya ualimu. Hii kazi ina miiko na maadili yake …kwa mwalimu huyu hii ni ajira yake ya kwanza, nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza cha kazi tangu ahitimu masomo yake…” Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima. “Isitoshe katika kisa hiki ni nadra kumpata mlalamikaji … Mwalimu mwenyewe huyu wa kike hawezi kuwa tayari kujidhalilisha kuwa amebakwa, yalikuwa maamuzi yake.” Aliongeza kuwa, kwa mwalimu huyo kupata ujauzito wa mwanafunzi wake hakuwezi kuathiri ajira yake, tofauti na mwalimu wa kiume akimpatia ujauzito mwanafunzi wake wa kike ambaye huathirika kwa kukatisha masomo. Jitihada za kumpata mwalimu huyo wa kike na mwanafunzi huyo zimegonga mwamba baada ya watu wao wa karibu kumweleza mwandishi kuwa hawako tayari kuuzungumzia mkasa huo. Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi kwa masharti ya kutoandikwa majina yao kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za kinidhamu shuleni hapo, pamoja na kukiri kutambua uhusiano baina ya mwanafunzi mwenzao na mwalimu wao, lakini walisema hivi sasa mwalimu huyo amesitisha uhusiano na mwenzao na kuanzisha uhusiano mpya na mwalimu mwenzao. Walisema pamoja na mambo mengine ni kama mwanafunzi mwenzao ameathirika kisaikolojia baada ya ‘kupinduliwa’ na mwalimu wake wa kiume ambaye kwa sasa ndiye baba mlezi wa mtoto. alisema mmoja wao. “Huyu mwalimu wa kike sisi sasa tunamwita shemeji yetu alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mwenzetu… penzi lao lilikolea hadi sasa ameweza kumzalia mtoto huyo…, lakini kwa sasa inavyoelezwa ni kwamba penzi limehamia kwa mwalimu mwenzake,“ Baadhi ya watu wa karibu na mwanafunzi huyo wanakiri kuwa mwanafunzi huyo hana uwezo wa kifedha kumudu kumpatia malezi stahiki mtoto wake huyo, hivyo hata mzazi mwenzake alipoanza uhusiano na mwalimu mwenzake hakuwa na jinsi, bali kukubaliana na matokeo. “Usiniandike jina, sisi tunashauri mwalimu huyo wa kike na mpenzi wake huyo wa kiume ambaye ni mwalimu mwenzake wahamishiwe shule nyingine kwa sababu kama kioo katika jamii wameteleza kwa kiasi kikubwa na watashindwa kuwajenga na kuwalea wanafunzi wao kimaadili. Alihoji. “Isitoshe tunajiuliza sheria hapa inasemaje maana kama angekuwa ni mwalimu wa kiume amempatia mwanafunzi wake wa kike ujauzito angeshitakiwa na kufikishwa mahakamani na pengine kuhukumiwa kifungo kisichopungua miaka 30 jela, sasa kwa hili sheria inasemaje?” Baadhi ya wazazi mkoani hapa waliohojiwa na mwandishi kwa nyakati tofauti wameelezea kushangazwa na tukio hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu alivyoshindwa kujizuia `kujiachia’ kimapenzi kwa mwanafunzi wake. Credit: Habarileo

   HABARI ZINGINE BOFYA HAPA 

ANGALIA PICHA ZA KUWANANGA WENGER, MOURINHO ZILIVYOZAGAA MITANDAO MBALIMBALI

BAADA YA KUSHIKANA WAKITAKA KUZICHAPA KATIKA MECHI YA JUZI KATI YA CHELSEA DHIDI YA ARSENAL, WADAU MBALIMBALI WA SOKA WAMETENEGENEZA PICHA KIBAO NA KUZISAMBAZA KWENYE MITANDAO MBALIMBALI KILA MMOJA AKIJARIBU KUONYESHA HISIA ZAKE PIA KUWANANGA MAKOCHA HAO MAARUFU WA ARSENAL NA CHELSEA. ANGALIE MWENYEWE.

HIKI NDICHO WAZIRI ALICHOWAAGIZA TFF KUKIFANYA KUHUSU 5% YA FEDHA ZA WADHAMINI WA KLABU

Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, leo amekutana na uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na ule wa Bodi ya Ligi Kuu (TPLB) na kuagiza kusitishwa kwa zoezi la ukatwaji wa asilimia 5. TFF iliiagiza bodi kukata asilimia 5 ya fedha za klabu kutokana na udhamini wa Vodacom na Azam TV, halafu ziwekwe kwenye akaunti yake ili zitumike kwa maendeleo ya soka. Lakini katika mkutano wa leo, Nkamia amewasisitiza TFF, Bodi ya ligi na klabu kukutana, halafu kulijadili hilo suala. TFF wametakiwa kukutana kwa pamoja na wadau hao, halafu wafikie mwafaka kabla ya kurejea serikalini. “Wanatakiwa wakutane, wazungumze na kukubaliana na siku nzuri ya kufanya hivyo nimeona ni Jumamosi. “Baada ya hapo watakachofikia mwafaka, basi watarudi serikalini na sisi tuangalie, lakini suala la kukata fedha hizo kweli nimesitisha na sasa liangaliwe hilo la kukutana kwanza,” alisema Nkamia ambaye kitaaluma ni mwanahabari. Mkutano huo unasubiriwa kwa hamu kwa kuwa pande zote tatu zimekuwa na msimamo wa aina mbili. Bodi ya ligi pamoja na klabu hizo za ligi kuu, zimesisitiza haziwezi kukubaliana na hilo la kukatwa fedha zao za udhamini kwa kuwa mikataba ya Vodacom na Azam Tv iko wazi na haielezi hilo la asilimia tano. Lakini tayari TFF kupitia Rais wake Jamal Malinzi ilishatangaza suala hilo halitakuwa na mjadala na lazima wakatwe. Pia kwa hesabu za kawaida, inaonyesha TFF inachukua fedha nyingi zaidi kuliko hata klabu moja moja kupitia udhamini wa Vodacom na Azam TV.

 HABARI ZINGINE BOFYA HAPA 

HARUFU YA SAFARI YA PHIRI KWENDA KUSALIMIA ZAMBIA, INAANZA KUNUKIA

NILIWAHI kuandika makala na kuelezea kuhusiana na suala la Simba kushindwa kufanya kwenye Ligi Kuu Bara kwa mechi mbili mfululizo. Nilichokuwa nakipinga ni kuhusiana na zile hisia za zama za mawe, eti inashindwa kufanya vizuri kwa ajili ya laana ya kundi linalojulikana kama Simba ukawa. Wako mashabiki au waliojiita wanachama wa Simba walihojiwa kwenye vyombo vya habari na kueleza jambo hilo, nikaona wanasambaza hisia ambazo si sahihi kwenye jamii. Vizuri ilikuwa ni kuangalia vizuri mambo kiufundi, tena uwanjani na si kuyaangalia kishabiki kupindukia au kishirikina kwa hisia za kudhani, kitu ambacho si kizuri kwa dunia tunayoishi sasa. Naendelea kupinga hisia hizo zisizo na mashiko za kuwa Simba haifanyi vizuri kwa sababu ya Simba ukawa. Ila nahimiza suala la umoja, kupatana, kurekebisha na kuelewana ni hema kwao kama Wanasimba. Tukirudi kwenye kikosi cha Simba, juzi kimetopata sare ya tatu mfululizo na kuweka reokodi mpya ya kufululizo sare katika mechi za kwanza za ligi. Mbaya zaidi mechi zote tatu iko nyumbani ikianza na sare ya mabao 2-2 dhidi ya Coastal Union, 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro na juzi 1-1 ilipokutana na Stand United ya Shinyanga. Usisahau Simba imeweka rekodi mpya ya kutoka sare mbili mfululizo dhidi ya timu mbili zilizopanda daraja, yaani Polisi Moro na Stand United, hii inaonyesha lazima jambo lifanyike. Hali inavyokwenda na hasa katika mechi dhidi ya Stand unaweza ukasoma jambo miongoni mwa wachezaji wa Simba, kuwa kuna presha kubwa nyuma yao inayowasukuma, kwamba lazima wapate ushindi. Kweli, viongozi wanaonekana wamechoka na sasa wanesukuma presha, huenda wanalazimika kwenda mazoezini na mazoezini ili kuhimiza wachezaji wao lazima washinde. Bado utaona, Kocha Patrick Phiri hana raha, baada ya mechi dhidi ya Stand alitikisa kichwa, kuonyesha anaumia na hakubaliani na matokeo hayo. Kutikisa kwake kichwa, kitu ambacho ni nadra kunaweza kutafsiriwa kwa hisia tofauti lukuki. Kwamba huenda amechoka, anashangazwa au anfikiria kuondoka na kurejea nyumbani kwao. Kwani anajaribu kufundisha au kuelekeza kinachotakiwa, lakini inaonekana inashindikana na makosa ya aina moja yanajirudia katika mechi tatu mfululizo, kushindwa kuzitumia nafasi kufunga na kuruhusa mabao ya kusawazisha! Kwa wanaojua rekodi zake, akichoshwa huwa anaanga na kuondoka zake kurejea kwao kimyakimya, hataki makuu. Yote yanawezekana ikawa anapinga presha kutoka kwa uongozi au vinginevyo. Pia inawezekana akawa amechoshwa na malekezo yake kutofanyiwa kazi kama ambavyo amekuwa akitaka na wachezaji wake wamekuwa wakipoteza nafasi nyingi zaidi. Ukipata nafasi rudia kuangalia mechi za Simba dhidi ya Coastal, Polisi Moro na Stand utaona Simba ndiyo timu inayoongoza hadi sasa kupoteza nafasi nyingi zaidi za kufunga. Kuwa na bunduki bila ya risasi unaweza usiwe hatari, ukazidiwa na mwenye kisu. Ndiyo ilivyo Simba, ina uwezo mkubwa wa kutengeneza nafasi, lakini hakuna wenye uhakika wa kuitupia wavuni, ni kupoteza muda. Inaonyesha maelekezo yote anayotoa Phiri yanafanya kazi ndiyo maana Simba imeweza kutengeneza nafasi nyingi zaidi za kufunga mabao, lakini wafungaji hakuna. Kweli wachezaji wanataka wafundishwe kupita kiasi namna ya kuuweka mpira wavunini. Wangekuwa Watanzania pekee tungeingia kwenye hofu labda hatuna shule za kutosha ndiyo maana wanapata shida. Lakini kuna Waganda na Warundi, vipi sasa wanashindwa? Tena rekodi zinaonyesha wako ambao wamefanya vema hapo kabla ya kufunga mabao mengi kama Emmanuel Okwi na Amissi Tambwe, sasa tatizo nini? Nasisitiza, kusema eti Simba ina kikosi kichovu si sahihi, mpira wanaucheza tena mzuri, lakini wanatakiwa kufunga na ndiyo tatizo kubwa walilonalo. Ndiyo maana nasisitiza suala la presha linaweza kuwa zuri lakini pia linaweza kuwa baya kwa Simba. Hivyo namna ya kuwahimiza wachezaji kunatakiwa kuwa na umakini mkubwa sana, la sivyo itakuwa ni kubomoa badala ya kujenga.

Na salleh ally  HABARI ZINGINE BOFYA HAPA 

Monday, October 06, 2014

WENGER AELEZA KISA CHA UGOMVI WAKE NA MOURINHO, ASISITIZA WALA HAJUTII

Kocha Arsene Wenger amesema wala hatajuta kutokana na kitendo chake cha kumsukuma Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho. Wenger alishikana na Mourinho wakati timu zao zilipokutana kwenye mechi ye Premier League kwenye Uwanja wa Stamford Bridge na Arsenal ikalala kwa mabao 2-0. “Nini cha kujuta, wala sitafanya hivyo. Nilikuwa ninatoka upande mmoja kwenda mwingine. “Nilipogeuka nikakuta mtu yuko mbele yangu kabisa kanizuia. “Halafu hasemi lolote, sasa unafikiri nitafanya nini,” alisema Wenger. Mwamuzi wa akiba alilazimika kuingia kati kuwatenganisha makocha hao wasifikie kuchapana makonde. Baadaye mwamuzi wa mchezo naye aliwaita na kutoa onyo kali akitishia kuwatoa uwanjani.

HIVI NDIVYO DIAMOND ALIVOFANYA MAKAMUZI YA NGUVU BIG BROTHER HOTSHOTS

STAA wa Bongo Fleva nchini Tanzania , Nasibu Abdul ' Diamond Platnumz ' usiku huu amefanya makamuzi ya nguvu katika uzinduzi wa shindano la Big Brother Hotshots unaofanyika jijini Johanessburg nchini Afrika Kusini. Katika shindano hilo, Tanzania inawakilishwa na watu wawili mrembo Irene ' La Veda ' na Idriss. Jumla ya washiriki 26 kutoka mataifa 12 ya Afrika watachuana kwa siku 63 kutafuta mshindi atakayejinyakulia kitita cha dola za Kimarekani 300, 000 .

DOWNLOAD NGOMA YA FID Q FT AY - UJIO WA VERSE MOJA

RONALDO AFANYA YAKE TENA REALMADRID IKIICHAPA ATHLETIC BILBAO

null
KLABU ya Real Madrid imeifumua mabao 5-0 Athletic Bilbao katika mchezo wa La Liga jana Uwanja wa Bernabeu. Mwanasoka Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo amepiga hat-trick ya 22 katika ligi ya Hispania, wakati Mfaransa Karim Benzema amefunga mabao mawili. Ronaldo alifunga katika dakika ya pili, 55 na 88, wakati Benzema alifunga dakika ya 41 na 69 na sasa Real have imepunguza pengo la pointi dhidi ya vinara, Barcelona hadi kubaki pointi nne KIkosi cha Real Madrid kilikuwa: Casillas, Carvajal, Pepe, Ramos/Varane, Marcelo, Modric, Kroos/Illarramendi, Rodriguez, Bale, Benzema/Isco na Ronaldo. Athletic Bilbao: Iraizoz, Laporte, Benat, Iturraspe, De Marcos, Susaeta (López Cabrera), M. Rico, Gurpegi, Muniain/Etxeita, Guillermo/Gomez na Balenziaga.

SASA NYIE MNAOJICHUBUA AMJUI KAMA MTU MWEUSI NI DILI SASA MCHEKI MZUNGU ALIVOJIBADILISHA KUWA MTU MWEUSI