WAKATI ikiwa imezoeleka kuwa baadhi ya
walimu wa kiume huwarubuni wanafunzi
wao wa kike na hata kuwaharibia kabisa
ndoto zao za kielimu kutokana na kuwapa
ujauzito, hali imekuwa tofauti mkoani
Rukwa ambako mwanafunzi wa Kidato
cha Pili anadaiwa kumzalisha mwalimu
wake.
Mwanafunzi huyo aliyemzalisha mwalimu
wake ana umri wa miaka 17, wakati
mwalimu huyo anayefundisha katika Shule
ya Sekondari ya Umma ya Nkasi, iliyopo
mwambao mwa Ziwa Tanganyika wilayani
Nkasi, Rukwa, ana umri wa miaka 25.
Tukio hilo linalotajwa kuwa la kwanza
kutokea wilayani hapa, limekuwa gumzo
kubwa kwa wakazi wa Nkasi na wilaya
jirani.
Hata hivyo, kwa wanafunzi, wamekuwa
wakimpongeza mwenzao kwa kujaliwa
kupata mtoto katika umri wake huo
mdogo, huku mzazi mwenzake akiwa na
uhakika wa maisha kutokana na kuwa ni
mtumishi serikalini.
Imeelezwa kuwa licha ya tukio hilo,
mwalimu huyo aliyezaa na mwanafunzi
wake bado anaendelea na masomo
shuleni hapo, huku `mzazi’ huyo wa
kiume akifundishwa na mzazi mwenzake.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi
mjini Namanyere hivi karibuni, Mkuu wa
Shule ya Sekondari Nkasi mjini
Namanyere ambayo ni ya mchanganyiko
ya umma, Amiamie Nanga alisema
mwalimu huyo alianza kazi shuleni hapo
ikiwa ni mara yake ya kwanza kufundisha
baada ya kuhitimu mafunzo ya ualimu
chuoni.
“Yameshatokea, lakini haileti picha nzuri
sana, lakini mimi nina uzoefu mkubwa na
wakazi wa mwambao wa Ziwa
Tanganyika, kwao si ajabu kuwa na
uhusiano na watu waliowazidi umri, iwe
kwa mtoto wa kike au wa kiume, wote ni
sawa tu…
alisema.
“Lakini katika kisa hiki, inaonesha walimu
sasa wanapoteza haiba ya ualimu. Hii
kazi ina miiko na maadili yake …kwa
mwalimu huyu hii ni ajira yake ya kwanza,
nikimaanisha ni kituo chake cha kwanza
cha kazi tangu ahitimu masomo
yake…”
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Rukwa, Jacob Mwaruanda
alisema hakuna kosa kwa mwalimu huyo
wa kike kwa kuwa tayari ni mtu mzima.
“Isitoshe katika kisa hiki ni nadra kumpata
mlalamikaji … Mwalimu mwenyewe huyu
wa kike hawezi kuwa tayari kujidhalilisha
kuwa amebakwa, yalikuwa maamuzi
yake.”
Aliongeza kuwa, kwa mwalimu huyo
kupata ujauzito wa mwanafunzi wake
hakuwezi kuathiri ajira yake, tofauti na
mwalimu wa kiume akimpatia ujauzito
mwanafunzi wake wa kike ambaye
huathirika kwa kukatisha masomo.
Jitihada za kumpata mwalimu huyo wa
kike na mwanafunzi huyo zimegonga
mwamba baada ya watu wao wa karibu
kumweleza mwandishi kuwa hawako
tayari kuuzungumzia mkasa huo.
Baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo
waliohojiwa na mwandishi wa habari hizi
kwa masharti ya kutoandikwa majina yao
kwa hofu ya kuchukuliwa hatua za
kinidhamu shuleni hapo, pamoja na kukiri
kutambua uhusiano baina ya mwanafunzi
mwenzao na mwalimu wao, lakini
walisema hivi sasa mwalimu huyo
amesitisha uhusiano na mwenzao na
kuanzisha uhusiano mpya na mwalimu
mwenzao.
Walisema pamoja na mambo mengine ni
kama mwanafunzi mwenzao ameathirika
kisaikolojia baada ya ‘kupinduliwa’ na
mwalimu wake wa kiume ambaye kwa
sasa ndiye baba mlezi wa mtoto.
alisema mmoja
wao.
“Huyu mwalimu wa kike sisi sasa
tunamwita shemeji yetu alikuwa na
uhusiano wa kimapenzi na mwenzetu…
penzi lao lilikolea hadi sasa ameweza
kumzalia mtoto huyo…, lakini kwa sasa
inavyoelezwa ni kwamba penzi limehamia
kwa mwalimu mwenzake,“
Baadhi ya watu wa karibu na mwanafunzi
huyo wanakiri kuwa mwanafunzi huyo
hana uwezo wa kifedha kumudu kumpatia
malezi stahiki mtoto wake huyo, hivyo
hata mzazi mwenzake alipoanza uhusiano
na mwalimu mwenzake hakuwa na jinsi,
bali kukubaliana na matokeo.
“Usiniandike jina, sisi tunashauri mwalimu
huyo wa kike na mpenzi wake huyo wa
kiume ambaye ni mwalimu mwenzake
wahamishiwe shule nyingine kwa sababu
kama kioo katika jamii wameteleza kwa
kiasi kikubwa na watashindwa kuwajenga
na kuwalea wanafunzi wao kimaadili.
Alihoji.
“Isitoshe tunajiuliza sheria hapa
inasemaje maana kama angekuwa ni
mwalimu wa kiume amempatia
mwanafunzi wake wa kike ujauzito
angeshitakiwa na kufikishwa mahakamani
na pengine kuhukumiwa kifungo
kisichopungua miaka 30 jela, sasa kwa
hili sheria inasemaje?”
Baadhi ya wazazi mkoani hapa
waliohojiwa na mwandishi kwa nyakati
tofauti wameelezea kushangazwa na tukio
hilo, na hasa kwa jinsi mwalimu
alivyoshindwa kujizuia `kujiachia’
kimapenzi kwa mwanafunzi wake.
Credit: Habarileo |
0 comments:
Post a Comment