NILIWAHI kuandika makala
na kuelezea kuhusiana na
suala la Simba kushindwa
kufanya kwenye Ligi Kuu
Bara kwa mechi mbili
mfululizo.
Nilichokuwa nakipinga ni
kuhusiana na zile hisia
za zama za mawe, eti
inashindwa kufanya vizuri
kwa ajili ya laana ya
kundi linalojulikana kama
Simba ukawa.
Wako mashabiki au
waliojiita wanachama wa
Simba walihojiwa kwenye
vyombo vya habari na
kueleza jambo hilo,
nikaona wanasambaza hisia
ambazo si sahihi kwenye
jamii.
Vizuri ilikuwa ni
kuangalia vizuri mambo
kiufundi, tena uwanjani na
si kuyaangalia kishabiki
kupindukia au kishirikina
kwa hisia za kudhani,
kitu ambacho si kizuri kwa
dunia tunayoishi sasa.
Naendelea kupinga hisia
hizo zisizo na mashiko za
kuwa Simba haifanyi vizuri
kwa sababu ya Simba
ukawa. Ila nahimiza suala
la umoja, kupatana,
kurekebisha na kuelewana
ni hema kwao kama
Wanasimba.
Tukirudi kwenye kikosi cha
Simba, juzi kimetopata
sare ya tatu mfululizo na
kuweka reokodi mpya ya
kufululizo sare katika
mechi za kwanza za ligi.
Mbaya zaidi mechi zote
tatu iko nyumbani ikianza
na sare ya mabao 2-2
dhidi ya Coastal Union,
1-1 dhidi ya Polisi
Morogoro na juzi 1-1
ilipokutana na Stand
United ya Shinyanga.
Usisahau Simba imeweka
rekodi mpya ya kutoka sare
mbili mfululizo dhidi ya
timu mbili zilizopanda
daraja, yaani Polisi Moro
na Stand United, hii
inaonyesha lazima jambo
lifanyike.
Hali inavyokwenda na hasa
katika mechi dhidi ya
Stand unaweza ukasoma
jambo miongoni mwa
wachezaji wa Simba, kuwa
kuna presha kubwa nyuma
yao inayowasukuma, kwamba
lazima wapate ushindi.
Kweli, viongozi
wanaonekana wamechoka na
sasa wanesukuma presha,
huenda wanalazimika kwenda
mazoezini na mazoezini ili
kuhimiza wachezaji wao
lazima washinde.
Bado utaona, Kocha Patrick
Phiri hana raha, baada ya
mechi dhidi ya Stand
alitikisa kichwa,
kuonyesha anaumia na
hakubaliani na matokeo
hayo.
Kutikisa kwake kichwa,
kitu ambacho ni nadra
kunaweza kutafsiriwa kwa
hisia tofauti lukuki.
Kwamba huenda amechoka,
anashangazwa au anfikiria
kuondoka na kurejea
nyumbani kwao.
Kwani anajaribu kufundisha
au kuelekeza
kinachotakiwa, lakini
inaonekana inashindikana
na makosa ya aina moja
yanajirudia katika mechi
tatu mfululizo, kushindwa
kuzitumia nafasi kufunga
na kuruhusa mabao ya
kusawazisha!
Kwa wanaojua rekodi zake,
akichoshwa huwa anaanga na
kuondoka zake kurejea kwao
kimyakimya, hataki makuu.
Yote yanawezekana ikawa
anapinga presha kutoka kwa
uongozi au vinginevyo.
Pia inawezekana akawa
amechoshwa na malekezo
yake kutofanyiwa kazi kama
ambavyo amekuwa akitaka na
wachezaji wake wamekuwa
wakipoteza nafasi nyingi
zaidi.
Ukipata nafasi rudia
kuangalia mechi za Simba
dhidi ya Coastal, Polisi
Moro na Stand utaona
Simba ndiyo timu
inayoongoza hadi sasa
kupoteza nafasi nyingi
zaidi za kufunga.
Kuwa na bunduki bila ya
risasi unaweza usiwe
hatari, ukazidiwa na
mwenye kisu. Ndiyo ilivyo
Simba, ina uwezo mkubwa
wa kutengeneza nafasi,
lakini hakuna wenye
uhakika wa kuitupia
wavuni, ni kupoteza muda.
Inaonyesha maelekezo yote
anayotoa Phiri yanafanya
kazi ndiyo maana Simba
imeweza kutengeneza nafasi
nyingi zaidi za kufunga
mabao, lakini wafungaji
hakuna.
Kweli wachezaji wanataka
wafundishwe kupita kiasi
namna ya kuuweka mpira
wavunini. Wangekuwa
Watanzania pekee
tungeingia kwenye hofu
labda hatuna shule za
kutosha ndiyo maana
wanapata shida. Lakini
kuna Waganda na Warundi,
vipi sasa wanashindwa?
Tena rekodi zinaonyesha
wako ambao wamefanya vema
hapo kabla ya kufunga
mabao mengi kama Emmanuel
Okwi na Amissi Tambwe,
sasa tatizo nini?
Nasisitiza, kusema eti
Simba ina kikosi kichovu
si sahihi, mpira
wanaucheza tena mzuri,
lakini wanatakiwa kufunga
na ndiyo tatizo kubwa
walilonalo.
Ndiyo maana nasisitiza
suala la presha linaweza
kuwa zuri lakini pia
linaweza kuwa baya kwa
Simba. Hivyo namna ya
kuwahimiza wachezaji
kunatakiwa kuwa na umakini
mkubwa sana, la sivyo
itakuwa ni kubomoa badala
ya kujenga. |
0 comments:
Post a Comment