Tuesday, October 07, 2014
|
kimemnasa msaidizi wa kazi za ndani
(hausigeli) akifanya biashara haramu ya
kuuza mwili kwa kisingizio cha mshahara
kiduchu.
Kushoto ni hausigeli akifanya biashara ya
uchangudoa maeneo ya Sinza jijini
Dar.Tukio hilo la aina yake liliingia
kwenye kamera za OFM maeneo ya Sinza
jijini Dar, mwishoni mwa wiki iliyopita
ambapo msichana huyo wa kazi alikutwa
kwenye harakati za kusaka wanaume ili
kuwapa penzi kwa malipo. Mara baada ya
kumnasa na kumlamba picha akiwa na
wenzake ambao nao kama yeye walikuwa
wamevaa nguo fupi yaani nusu utupu,
alianza kuangua kilio hasa alipokuwa
akihojiwa kwa nini anajihusisha na
biashara hiyo hatarishi katika maisha
yake.
“Jamani mmenipiga picha mtanipotezea
kazi yangu, jamani mimi nimeajiriwa, ni
mfanyakazi wa ndani kwa mheshimiwa
Mikocheni (Dar), nafanya kazi za ndani hii
yote ni kujitafutia riziki nje ya kazi,”
alilalama binti huyo aliyekadiriwa kuwa na
umri kati ya miaka 20 hadi 23. |
|
Baadhi ya machangudoa wakiwa
mawindoni.Binti huyo aliwaambia OFM
kwamba alifikia hatua hiyo ya kujiingiza
katika biashara hiyo ya ngono kutokana na
ugumu wa maisha huku lawama
akizielekeza kwenye mshahara kidogo wa
kazi za ndani.
“Mshahara wangu ni mdogo sana, nalipwa
shilingi elfu 50 kwa mwezi, nina watoto
wawili kijijini hivyo hautoshi. Kama vipi
nitafutieni kazi nitaacha kuuza mwili,”
alisema.
Alipoulizwa namna anavyotoka kwa bosi
wake kwenda kujiuza, hausigeli huyo
alisema kwamba huwa anakula dili na
walinzi wa bosi wake usiku wakiwa
wamelala anatoka na akirudi freshi
anawakatia walinzi chao. |
|
Machangudoa wengine wakizikimbia
kamera.Alisema kuwa yeye analala katika
vyumba vya uani kwa hiyo anapotoka
waajiri wake hao inakuwa vigumu kumsikia
kwani wanakuwa wamepitiwa na usingizi.
Aliendelea kueleza kwamba kuna siku
nyingine huwa anarudi nyumbani akiwa
amevuna fedha nyingi kuliko mshahara
wake.
“Hii kazi yangu inaniingizia kipato kikubwa
sana kuliko mshahara,” alisema hausigeli
huyo. |
HABARI ZINGINE BOFYA HAPA
0 comments:
Post a Comment