Tuesday, October 07, 2014
|
Msanii mkongwe wa muziki nchini, Prince Dully
Sykes amefunguka kuwa hakuna msanii wa Hip
Hop hapa Tanzania anayemfikia kwa
maendeleleo.
Dully ambaye anamiliki studio pamoja na vifaa
vya muziki aliongea hayo mbele ya Fid Q.
“Kwa hapa nilipofikia na uwezo na mali
nilizokuwa nazo hakuna mwana hip hop
anayenifikia. Umaskini mliokuwa nao ni mwana
hip hop gani anaweza akafikia uwezo wangu? Sio
studio tu kwani mali ni studio peke yake!Katika
mali zangu studio haipo, mimi ni mwanamuziki
lakini wanahiphop ni maskini zaidi yangu mimi,
siwezi taja mali zangu, kuna studio na home
studio, wewe (Fid Q) una home studio,” alisema
Dully kwenye maongezi ya kwenye basi la ziara
ya Fiesta ambayo yalikuwa on the record (ruhusa
kurekodiwa).
Baada ya kauli hiyo, Fid Q ameiambia Bongo5
kuwa Dully hajui utajiri anaouzungumzia huku
akidai kuwa wasanii wa muziki wa kuimba
wanapewa nafasi kubwa kwenye muziki wao na
ndio maana wanakuwa na kiburi.
“Kwanza Dully ana utajiri gani kuliko wasanii wa
Hip Hop? Mimi naona yupo kawaida sana. Sema
wasanii wengi wa muziki wa kuimba wanapewa
nafasi nyingi za kuonekana kuliko wana Hip Hop
lakini sio kusema anawazidi utajiri,” alisema Fid
Q.
Unahisi Dully ameongea ukweli? Funguka. |
0 comments:
Post a Comment