Monday, October 06, 2014

HIVI NDO JINSI MADADA WAREMBO WANAVOFANYA LAANA KWENYE CLUB ZA USIKU

NI SHEEEDAH.....MTUMISHI AVAMIA ENEO LA MAKABURI NA KUJENGA BAA

Mtaro alijikuta juzi katika wakati mgumu baada ya wananchi wanaodai ni wenye hasira kutaka kumpa kipigo kwa kitendo hicho cha kugeuza sehemu ya makaburi kuwa eneo la burudani . Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni mfanyakazi Idara ya Fedha ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, inadaiwa alianzisha biashara hiyo ya vileo katika eneo la Roben Kata ya Mkuti , mjini Masasi wiki mbili zilizopita. Tafrani iliyojitokeza juzi na kudumu kwa zaidi ya saa saba, ilikuwa ni baada ya kundi la vijana kufika eneo hilo kwa ajili ya kuchimba kaburi kwa maziko ya ndugu yao na kukuta hali tofauti . Inadaiwa walikuta baadhi ya makaburi yamejengwa sehemu za kukaa wateja, choo pamoja na banda kubwa la biashara lililosheheni vinywaji. Aidha walikasirishwa na kile kinachodaiwa kwamba ni kukuta pakiti tupu za pombe zikiwa zimetapakaa juu ya makaburi hayo. Inadaiwa pia walikutwa wateja wakipata vinywaji wakati huo saa 4 asubuhi huku baadhi wakiwa wameweka miguu juu ya makaburi; kitendo kilichoibua hasira ya vijana hao walioamua kutoa taarifa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mkuti . Mmiliki Akizungumza kwa niaba ya mmiliki, Meneja wa ‘ baa ’ hiyo , Gasper Priscus alisema waliamua kujenga kwenye eneo hilo kwa kuwa kiwanja hicho wanakimiliki. Alidai waliuziwa na mkazi wa Kitongoji cha Roben mjini Masasi, Gerald Daudi . Kwa mujibu wa meneja huyo, baada ya kuuziwa waliamua kuanza ujenzi wa baa hiyo kwa haraka kwa madai kuwa aliyewauzia, Daudi ni mgonjwa. Priscus alisema walikuwa na hofu kwamba endapo angefariki kabla ya kujenga baa hiyo , wangenyang’ anywa eneo hilo kwa kuwa limeshazungukwa na makaburi. Alikiri kwamba takribani wiki mbili sasa zimepita tangu waanze biashara hiyo ya vileo kwenye eneo hilo na kwamba wamekuwa wakipata wateja wengi hasa usiku . Akana kuuza Hata hivyo Daudi; anayedaiwa kuuza eneo hilo kwa Mtaro alikana kuliuza . Alisema aliamua kumpa eneo hilo bure kwa jinsi anavyomsaidia katika hali yake ya ugonjwa ambao umekuwa ukimsumbua kwa muda mrefu sasa . Akizunngumzia kuhusu kuondolewa kwa baadhi ya misalaba kupisha ujenzi huo, Daudi aliyekuwa akizungumza kwa taabu akiwa kitandani , alisema walikubaliana ing’ olewe mitatu pekee kutoka kwenye makaburi ya familia yao. Alisema uamuzi wa kung’ oa misalaba mingine zaidi ya 10 ni uamuzi uliofanywa na aliyemkabidhi eneo hilo. Ofisa Mtendaji Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkuti , Moza Napachili alithibitisha ofisi yake kupokea taarifa za kuwepo kwa mtu aliyejenga baa kwenye eneo la makaburi. Napachili alisema alikwenda kwenye eneo la tukio akiongozana na Mwenyekiti wa mtaa huo kutafuta suluhu ya mgogoro huo . Baadaye kilifanyika kikao baina ya Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi, Henry Kagogoro , Mtendaji wa Kata , wa Mtaa, na Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na anayedaiwa kuwa mmiliki wa baa hiyo , Mtaro . Makubaliano yaliyofikiwa na kikao hicho ni kutaifisha eneo hilo. Walikubaliana libaki chini ya Halmashauri kwa ajili ya shughuli za maziko pekee. Hivyo iliamuriwa jengo hilo la baa na vibanda , viondolewe na mhusika, kesho awasilishe taarifa Idara ya Ardhi zinazoonesha kuwa eneo hilo analimiliki kihalali . Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri alisisitiza eneo hilo la makaburi ni mali ya Halmashauri . Wateketeza kwa moto Hata hivyo wananchi waliokuwa wamefika kwenye makaburi hayo kwa ajili ya kuzika ndugu yao, waliteketeza kwa moto vibanda vitano vya kupumzikia vilivyoezekwa kwa makuti . Pia jengo la baa lilibomolewa . Polisi Kwa upande wa Polisi, ilikiri kuwa na taarifa juu ya mgogoro huo . Mkuu wa Polisi, Wilaya, Azaria Makubi alisema wanaendelea na upelelezi kuhusu tukio hilo. MKAZI wa Mtaa wa Misufini, Kata ya Nyasa, Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara , Innocent Mtaro anatuhumiwa kujenga baa katikati ya makaburi.

News Alert: Siri yafichuka: Sababu ya wabunge kucheza "kitorondo" bungeni hii hapa

Baada ya "Rasimu ya Sitta" kupitishwa na Bunge maalumu baadhi ya wabunge walilipuka kwa furaha na wengine wakakata mauno hadharani, huku mbunge wa Njombe kaskazini Deo Sanga akicheza "Kitorondo" na kukata mauno mbele ya halaiki.

Pia kuna wabunge wengine walikua wakicheza kwa kufuatisha milio ya miziki iliyokua ikirindima kupitia simu zao za mkononi.Watu wengi walihamaki kitendo cha wabunge kufurahia Rasimu hiyo hadi kufikia hatua ya kujitoa akili.

Hii hapa siri ya furaha ya Wabunge hao..

RASIMU YA WARIOBA ILIPENDEKEZA:

1. Mbunge akigombea vipindi vitatu basi, awaachie wengine.
2. Mbunge akivurunda ktk utendaji wake, wananchi wana uwezo wa kumuondoa na kuchangua mwingine.
3. Hakuna mbunge kuwa Waziri, Mkuu wa mkoa, m/kiti wa bodi ya shirika etc. (kwanini vyeo vyote mjilundikie nyie?).
4. Elimu ya mbunge iwe angalau stashahada (diploma) na kuendelea.

RASIMU YA SITTA (ILIYOPITISHWA) IMEPENDEKEZA HIVI:1. Ukomo wa Ubunge usiwe vipindi vitatu.. Hata wazee waliokaa bungeni miaka 50 kama Kingunge, waendelee tukugombea. Vijana wanaotaka kuwa viongozi labda wakajaribu kwny SACCOSS sio UBUNGE.

2. Mbunge akivurunda wananchi hawawezi kumfanya kitu chochote hadi miaka mitano iishe na mbunge apewe pensheni yake (Mil.160).

3. Ruksa Mbunge kuwa waziri, Mkuu wamkoa, DC, Mwenyekiti wa shirika, na vyeo vingine kadri anavyoweza kujilundikia. Wanaosema mbunge asiwena vyeo viwili au zaidi, wana "wivu wa kike" (according to Pius Msekwa).

4. Elimu ya Mbunge iwe kama ya Deo Sanga (mbunge Njombe Kask), yaani kujua kusoma na kuandika tu inatosha. Rasimu ya Sitta inasema si lazima mbunge awe na degree, diploma, au cheti.Si lazima mbunge awe na elimu ya sekondari. Si lazima Mbunge awe amemaliza elimu ya msingi. Hata kama alisoma akaishia darasa la 3 lakini anajua kusoma na kuandika RUKSA KUGOMBEA UBUNGE.

Sasa je katika mazingira haya wabunge wataacha kukata mauno na kucheza"kitorondo" kwa Rasimu hii kupita??JIPU LIMEPASUKA, SIWEZI KUWA ADUI KWA KUSEMA UKWELI.

Malisa GJ || Your Partner In Critical Thinking.!

HUYU NI MCHEZAJI ALIYEINGIA KWENYE ORODHA YA WACHEZAJI WA MANCHESTER UNITED MUHIMU OLD TRAFORD

KIUNGO wa zamani wa Manchester United, Park Ji-sung ametambulishwa kuwa Balozi wa klabu Old Trafford leo akiungana na aliyekuwa kocha wake, Sir Alex Ferguson. Wawili hao walifanyiwa mahojiano uwanjani kabla ya United kuanza kupepetana na Everton, na Ferguson akazungumzia enzi za Park na umuhimu aliokuwa nao Manchester. Uteuzi huo wa Park unafanya idadi ya Mabalozi wa United kufika sita, baada ya Sir Bobby Charlton, Andrew Cole, Ferguson, Denis Law na Bryan Robson.

HIVI NDO JINSI ARSENAL WENGER ALIVOTAKA KUMCHEZESHEA KICHAPO MOURINHO STARMFORD BRIDGE

Kocha wa Arsenal, Arsene Wenger (kushoto) akimsukuma mpinzani wake, Jose Mourinho wa Chelsea wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya England baina ya timu hizo leo. Chelsea imeshinda 2-0. Wenger ni Mourinho ni wapinzani wa muda mrefu.
Arsene Wenger akimfuata kocha wa Chelsea, Jose Mourinho baada ya Cahil kumchezea rafu Sanchez
Mtafaruku wa makocha huo uliteks hisia za wengi Uwanja wa Stamford Bridge, ingawa mwisho wa mchezo Wenger alikuwa mnyonge baada ya Arsenal kufungwa

HIVI NDO JINSI KICHWA CHA SANCHEZ KILIVOMPELEKA KIPA WA CHELSEA HOSPITALI APO JANA

Kipa wa Chelsea, Thibaut Courtois aliumia kichwani baada ya kugongana na Alexis Sanchez hapa dakika ya na akashindwa kuendelea na mchezo na kukimbizwa hospitali, nafasi yake akiingia Petr Cech.
Sanchez mara moja alionyesha uungwana kwa kwenda kufutilia hali ya Courtois

EPL: MATOKEO YA MACHESTER UNITED vs EVERTON HAYA HAPA

MANCHESTER United imepata ushindi wa pili mfululizo katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa mabao 2-1 Everton Uwanja wa Old Trafford jioni hii. Hali sasa ni shwari kwa kocha Louis Van Gaal baada ya ushindi huo- mshambuliaji wake wa mkopo, Radamel Falcao akifunga bao lake la kwanza tangu atue Old Trafford. Angel di Maria alitangulia kuifungia Manchester United dakika ya 26 kabla ya mkwaju wa penalti wa Leighton Baines kuokolewa na David de Gea dakika ya 45 baada ya Tony Hibbert kuchezewa rafu na Luke Shaw. Everton ilisawazisha bao hilo dakika ya 55 kupitia kwa Steven Naismith akimalizia krosi nzuri ya Baines kabla ya Radamel Falcao kuifungia bao la ushindi Manchester United dakika ya 62.

Sunday, October 05, 2014

SHUHUDIA LIVE UCHAFU UNAOFANYIKA USIKU BONGO,NI BALAA

AMAKWELI UZEE MWISHO CHELINZE, MJINI KILA MTU BEBI,CHEKI VIBABU VIKIBAMBIA MABINTI WABICHI KUMBI ZA STAREHE

MAJANGAZ HARUSI YA KWANZA KUFUNGWA NA WASHIRIKI WOTE WAKIWA WATUPU WA MNAYAMA

Kweli ukistaajabu ya Musa utayaona ya firauni,hapa bongoland na sehemu nyingi duniani kwa ujumla maharusi mara nyingihujipangia mavazi yao kwa ajili ya siku ya harusi yao huku wakitumia gharama nyingi kununulia nguo hizo kama mashela ya gharama na suti za maana na kali.Lakini huko New zealand hayo yote hayaitajiki kwan maharusi hufunga ndoa wakiwa watupu kabisa!!Hawa wanajiita Lowes’ Unclad wedding wakidai wanaonesha uhalisia katika nyanja hiyo.
Na wasimamizi wao nao mtindo ule ule!
kweli dunia it's about to end maana hivi sio vya kawaida hata kidogo...

MHITIMU WA CHUO AVUA NGUO ZOTE JUKWAANI ALIPOITWA KUPEWA CHETI ZA KUMALIZA CHUO

Wasomi wanapokutana hasa katika zoezi la kutunukiwa cheti kama kielezo cha uhitimu wa ngazi fulani kuna vitu huwezi kuvifikiria kama vitatokea hata kidogo. Katika Jack Britt High School, North Carolina, Marekani wanafunzi mmoja amewaacha hoi mamia ya watu waliohudhuria sherehe ya kutunukiwa vyeti (graduation) baada ya kupanda jukwaani kupokea cheti chake na ghafla akavua johon lake na kubaki na boxer. Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote miwili juu kama mwanamieleka anayetamba. Lakini haikuchukua round wanausalama wakamdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi. Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo alinyang’anywa diploma yake na hivyo hakukabithiwa cheti. Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa hana kielelezo cha elimu yake. “Shule yetu imefanya jitihada kubwa. Hapo zamani watu waliohudhuria walikuwa wenye vurugu wakati wa graduation. Tumefanya jitihanda kuwafanya watu waheshimu wanafunzi. Huyu kijana amechagua kutoonesha heshima kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank Till, mwalimu wa chuo hicho.

SALOON ILIYOKO SINZA..INAYOFANYA MASAJI HUKU IKIJIHUSISHA NA UTOAJI WA HUDUMA YA NGONO CHAFU HII HAPA

AMA kweli shetani anafanya hesabu zake za mwisho! Tangu mwaka 2014 uanze yapo yaliyotokea na kusisimua likiwemo la kunaswa kwa kinara wa utoaji mimba, Dk. Mambo, maeneo ya Kawe, Dar lakini hili la warembo kufumwa wakitoa dozi ya ngono linaweka historia nyingine,
Warembo wanaotoa huduma wakiwa wameficha sura zao baada ya kunaswa na OFM. Hebu sikia, saluni inayojihusisha na vitendo vya ’masaji’ lakini kumbe ngono imo ndani yake imenaswa na kufumuliwa baada ya kukutwa uchafu wa aina yake nyuma ya pazia. Saluni hiyo maarufu kuliko Miji ya Sodoma na Gomora, ipo maeneo ya Sinza ambapo kwa muda mrefu sasa imekuwa ikijihusisha na uchafu huo na kusababisha kero kwa wananchi wenye maadili yaliyotukuka.TAARIFA MEZANI

CREDIT GPL

BONGO MOVIE YAZIDI PUKUTIKA HUYU MWINGINE AJITOA NA KUSEMA MANENO HAYA MAZITO

Mrembo Mcheza Filamu za Bongo Esha Buheti Amefunguka Haya Hapa chini Kuhusu Uozo wa Kundi la Bongo Movies....

Rekodi mpya waliyoweka FC Barcelona kwenye La Liga hii hapa

Barcelonawamefanikiwa kutengeneza rekodi kadhaa usiku wa leo katika ligi kuu ya Hispania baada ya kupata matokeo chanya dhidi ya Rayo Vallecano kwenye dimba la Estadio del Rayo Vallecano. FC Barcelona ilifanikiwa kushinda mechi hiyo kwa ushindi wa magoli 2-0 – Messi na Neymar wakifunga magoli hayao. Kufuatia ushindi huo wa 2-0, Barca imefanikiwa kuweka rekodi ya nzuri kwenye safu ya ulinzi. Kikosi cha Luis Enrique sasa kimefanikiwa kuwa timu ya kwanza katika historia ya La liga kucheza mechi 7 za mwanzoni mwa ligi hiyo bila kuruhusu wavu kugushwa. Pia wakati huo huo golikipa wa timu hiyo, Mchile Claudio Bravo ameweka rekodi mpya ya katika kulinda lango lake. Bravo amevunja rekodi ya kucheza dakika nyingi bila kuruhusu wavu wake kuguswa, mpaka kufikia sasa Bravo amecheza jumla ya dakika 561 bila kufungwa goli, akivunja rekodi ya golikipa wa zamani wa Barca, Pedro Artola aliyecheza kwa dakika 560 bila kufungwa goli katika msimu wa 1977-78.

Kama ulikosa mchezo wa FC Barcelona vs Rayo Vallecano, matokeo haya hapa

Wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika ligi kuu ya Hispania mpaka sasa huku wakiongoza ligi hiyo, FC Barcelona leo walijitupa uwanjani kupambana na Rayo Vallecano kwenye dimba la Estadio del Rayo Vallecano. Huku wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi yao Champions League dhidi ya Paris Saint Germain, FC Barcelona waliingia uwanjani wakitaka kuendeleza rekodi yao kushinda mechi zao zote za La Liga. Matokeo ya mchezo huo ulioisha hivi punde ni ushindi wa 6 kwa vijana wa Luis Enrique katika mechi 7 za ligi walizocheza msimu huu. Magoli ya Lionel Messi na Neymar yaliisadia Barca kufikisha jumla ya pointi 19 katika La Liga na kuendelea kushikilia kilele cha msimamo wa ligi hiyo. Takwimu za Mechi:

Angalia trailer ya filamu mpya aliyoigiza mchezaji huyu wa Man United

Kama atakuwa hachori, au kufundisha soka la ufukweni, ama kufanya kampeni za dhidi ya ukosefu wa haki za kijamii , basi utamkuta mchezaji huyu wa zamani aliyewahi kutamba kwenye soka miaka kadhaa iliyopita akiwa anaigiza. Mchezaji wa huyu zamani wa vilabu vya Leeds na Manchester United, ‘King’ Erio Cantona ameendelea na fani yake nyingine ya uigizaji. Cantona ameonekana akiwa anaigiza kwenye movie mpya ya kifaransa iitwayo You And The Night. Cantona alianza kuigiza miaka 17 iliyopita mara tu alipotangaza kustaafu kucheza soka la ushindani, hapo chini ni filamu ambazo amewahi kuigiza nahodha huyo wa zamani wa Man United.
Pia unaweza kuangalia trailer ya filamu hii hapa chini……

Kocha huyu alalamika kunyimwa mualiko wa mvinyo na Van Gaal

Wakati wa utawala wa Sir Alex Ferguson katika klabu ya Manchester United alikuwa na utaratibu wa kuwaalika baadhi ya makocha wa timu pinzani kunywa mvinyo mara tu baada ya kumalizika kwa mchezo wowote katika dimba la Old Trafford. Lakini chini ya utawala mpya wa kocha Louis Van Gaal utaratibu huo wa Ferguson umebadilika na tayari mmoja wa makocha waliokuwa wamezoeshwa na Fergie kualikwa kunywa mvinyo ametoa malalamiko yake. Akiandika makala yake yaliyochapishwa kwenye gazeti la Evening Standard, kocha wa West Ham Sam Allardyce amesema ameshangazwa na kusikitishwa na kitendo cha kocha wa Manchester United Louis van Gaal kutomualika kunywa mvinyo baada ya mechi kati ya timu zao wikiendi iiyopita. “Siku zote nilipokuwa nikienda Old Trafford nilikuwa nikialikwa kwa ajili ya mazungumzo kidogo pamoja na kunywa mvinyo. “Huu utamaduni uliokuwepo kwa makocha wa timu pinzani, ndio maana nilishangazwa na kusikitishwa nilipotaarifiwa kwamba hakukuwa na utaratibu ule tena baada ya mechi kuisha. Niliambiwa utaratibu ule haupo tena, ikanibidi kuondoka.” - Aliandika Alladayce.

Simba bado hali tete, haya hapa matokeo yao dhidi ya Stand United na mechi zingine za VPL

Hali imezidi kuwa mbaya kwa klabu ya Simba, ikiwa haijashinda mchezo katika msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom, wana msimbazi leo walijitupa kwenye uwanja wao wa nyumbani wakiwakaribisha wageni kwenye ligi kuu Stand United. Huku ikiwa na rekodi ya kushindwa kulinda ushindi wake katika mechi mbili zilizopita – wakianza kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Coastal Union, kisha sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Morogoro, Simba leo tena walianza kuongoza kwa goli moja lilofungwa na Shabaan Kisiga katika dakika ya 35. Lakini ilivyo kawaida yao msimu huu, dakika 10 baadae beki yao ikazembea na Stand United wakapata goli la kusawazisha kupitia mchezaji na Omary Mtaki. Matokeo mengine kwenye ligi hiyo ni kama ifuatavyo: Polisi Morogoro 1-1 Kagera Sugar… FT… Coastal Union 2-1 Ndanda FC… FT… Ruvu Shooting 0-0 Mbeya City

KAMA ULIKOSA Matokeo ya Manchester City dhidi ya Aston Villa haya hapa

Siku chache baada ya kushindwa kupata matokeo chanya katika mchezo wao wa pili wa ligi ya mabingwa wa ulaya dhidi ya klabu ya AS Roma, mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Manchester City leo walisafiri mpaka Villa Park kwenda kuchuana na Aston Villa. Mchezo huo uliokuwa wa kasi umemalizika hivi karibuni huku City wakifanikiwa kuwasogolea Chelsea kwenye msimamo wa ligi kuu ya Barclays. Huku zikiwa zimebakia dakika 10 mchezo kumalizika Yaya Toure aliiandikia City goli la kwanza kabla ya Sergio Aguero kuihakikishia ushindi timu ya Manuel Pellegrini kwa goli zuri kabisa alilofunga katika dakika ya 88. Aston Villa inayofundishwa na Paul Lambert akisaidiwa na nahodha wa zamani wa Man United, Roy Keane, walijitahidi kwa kila hali kujaribu kupata matokeo mazuri dhidi ya mabingwa watetezi lakini bahati haikuwa yao, na mpaka mwamuzi anamaliza mpira City walikuwa wamewafunga nyumbani kwao kwa magoli 2-0. Timu zilizpangwa kama ifuatavyo: Aston Villa: Guzan, Hutton, Senderos, Baker, Cissokho, Cleverley, Westwood, Delph, Richardson (Grealish 71), Weimann (Benteke 61), N’Zogbia (Bacuna 71) Subs (not used): Clark, Bent, Sanchez, Given Bookings: NONE Goals: NONE Man City: Hart, Zabaleta, Kompany, Mangala, Kolarov, Milner, Fernandinho (Lampard 56), Toure, Silva (Navas 84), Dzeko (Fernando 64), Aguero Subs (not used): Sagna, Caballero, Jesus Demichelis, Jovetic Bookings: Kolarov Goals: Toure (82), Aguero (88) Referee: Chris Foy (Merseyside) Read more: http://www.dailymail.co.uk/sport/ football/article-2780485/Aston-Villa-0-2- Manchester-City-Yaya-Toure-Sergio-Aguero- earn-Manuel-Pellegrini-late- win.html#ixzz3FCgc0CEd Follow us: @MailOnline on Twitter | DailyMail on Facebook

Saturday, October 04, 2014

TAMBWE FITI KABISA KUWAVAA STAND UNITED TAIFA LE

MSHAMBULIAJI Amisi Tambwe yuko fiti
kucheza mechi ya leo, timu yake Simba SC
ikimenyana na Stand United Uwanja wa
Taifa, Dar es Salaam- lakini beki Issa
Rashid ‘Baba Ubaya’ na winga Haroun
Chanongo wataendelea kupumzika.
Daktari wa Simba SC, Yassin Gembe
ameiambia BIN ZUBEIRY jana usiku
kwamba, Tambwe alifanya mazoezi vizuri
jana na ameonyesha yuko fiti kabisa.
Tambwe aliumia goti juzi jioni mazoezini
Uwanja wa Boko Veterani na kuzua hofu
kwamba anaweza kuongeza idadi ya
majeruhi wa timu hiyo ambayo tayari
inawakosa Ivo Mapunda, Paul Kiongera,
Nassor Masoud ‘Chollo’, Baba Ubaya na
Chanongo.
“Tambwe amefanya mazoezi vizuri tu, kama
nilivyosema, hayakuwa maumivu makubwa
na tunashukuru imekuwa hivyo. Ni matarajio
yetu ataanza mechi na Stand,”amesema.
Daktari huyo wa zamani wa Mtibwa Sugar
amesema kwamba Issa na Chanongo
wameendelea na mazoezi mepesi na
kwamba hawatakuwa tayari kwa mchezo wa
leo.
Baada ya sare mbili mfululizo 2-2 na
Coastal Union ikitoka kuongoza 2-0 hadi
mapumziko na 1-1 na Polisi Moro pia
ikiongoza hadi baada ya kipindi cha kwanza,
Simba SC itajaribu kusaka ushindi wa
kwanza leo dhidi ya timu iliyopanda msimu
huu, Stand.
Tayari Stand wamekwishaonja ladha ya
ushindi katika Ligi Kuu kufuatia kushinda 1-0
katika mchezo wao uliopita dhidi ya wenyeji
Mgambo JKT mjini Tanga.
Lakini ikumbukwe Stand ilianza na kipigo
cha nyumbani cha mabao 4-1 kutoka kwa
Ndanda waliopanda nao Ligi Kuu msimu
huu.