Hali imezidi kuwa mbaya kwa klabu ya Simba,
ikiwa haijashinda mchezo katika msimu mpya
wa ligi kuu ya Vodacom, wana msimbazi leo
walijitupa kwenye uwanja wao wa nyumbani
wakiwakaribisha wageni kwenye ligi kuu Stand
United.
Huku ikiwa na rekodi ya kushindwa kulinda
ushindi wake katika mechi mbili zilizopita –
wakianza kutoka sare ya 2-2 dhidi ya Coastal
Union, kisha sare ya 1-1 dhidi ya Polisi
Morogoro, Simba leo tena walianza kuongoza
kwa goli moja lilofungwa na Shabaan Kisiga
katika dakika ya 35.
Lakini ilivyo kawaida yao msimu huu, dakika
10 baadae beki yao ikazembea na Stand United
wakapata goli la kusawazisha kupitia mchezaji
na Omary Mtaki.
Matokeo mengine kwenye ligi hiyo ni kama
ifuatavyo:
Polisi Morogoro 1-1 Kagera Sugar… FT…
Coastal Union 2-1 Ndanda FC… FT… Ruvu
Shooting 0-0 Mbeya City |
0 comments:
Post a Comment