Wasomi wanapokutana hasa katika zoezi la
kutunukiwa cheti kama kielezo cha uhitimu wa
ngazi fulani kuna vitu huwezi kuvifikiria kama
vitatokea hata kidogo.
Katika Jack Britt High School, North Carolina,
Marekani wanafunzi mmoja amewaacha hoi
mamia ya watu waliohudhuria sherehe ya
kutunukiwa vyeti (graduation) baada ya kupanda
jukwaani kupokea cheti chake na ghafla akavua
johon lake na kubaki na boxer.
Baada ya kuvua joho alinyoosha mikono yote
miwili juu kama mwanamieleka anayetamba.
Lakini haikuchukua round wanausalama
wakamdhibiti na kumuweka chini ya ulinzi.
Kwa mujibu wa The Huffington Post, kijana huyo
alinyang’anywa diploma yake na hivyo
hakukabithiwa cheti.
Hata hivyo bado anahesabiwa kama mtu aliye
maliza masomo yake na kuhitimu licha ya kuwa
hana kielelezo cha elimu yake.
“Shule yetu imefanya jitihada kubwa.
Hapo zamani watu waliohudhuria walikuwa
wenye vurugu wakati wa graduation. Tumefanya
jitihanda kuwafanya watu waheshimu wanafunzi.
Huyu kijana amechagua kutoonesha heshima
kwa wanafunzi wenzake.” Alisema Dr Frank Till,
mwalimu wa chuo hicho. |
0 comments:
Post a Comment