Barcelonawamefanikiwa kutengeneza rekodi
kadhaa usiku wa leo katika ligi kuu ya
Hispania baada ya kupata matokeo chanya
dhidi ya Rayo Vallecano kwenye dimba la
Estadio del Rayo Vallecano.
FC Barcelona ilifanikiwa kushinda mechi hiyo
kwa ushindi wa magoli 2-0 – Messi na Neymar
wakifunga magoli hayao.
Kufuatia ushindi huo wa 2-0, Barca
imefanikiwa kuweka rekodi ya nzuri kwenye
safu ya ulinzi.
Kikosi cha Luis Enrique sasa kimefanikiwa
kuwa timu ya kwanza katika historia ya La liga
kucheza mechi 7 za mwanzoni mwa ligi hiyo
bila kuruhusu wavu kugushwa.
Pia wakati huo huo golikipa wa timu hiyo,
Mchile Claudio Bravo ameweka rekodi mpya ya
katika kulinda lango lake.
Bravo amevunja rekodi ya kucheza dakika
nyingi bila kuruhusu wavu wake kuguswa,
mpaka kufikia sasa Bravo amecheza jumla ya
dakika 561 bila kufungwa goli, akivunja rekodi
ya golikipa wa zamani wa Barca, Pedro Artola
aliyecheza kwa dakika 560 bila kufungwa goli
katika msimu wa 1977-78. |
0 comments:
Post a Comment