Mtaro alijikuta juzi katika wakati mgumu baada
ya wananchi wanaodai ni wenye hasira kutaka
kumpa kipigo kwa kitendo hicho cha kugeuza
sehemu ya makaburi kuwa eneo la burudani .
Mfanyabiashara huyo ambaye pia ni
mfanyakazi Idara ya Fedha ya Halmashauri ya
Wilaya ya Masasi, inadaiwa alianzisha biashara
hiyo ya vileo katika eneo la Roben Kata ya
Mkuti , mjini Masasi wiki mbili zilizopita.
Tafrani iliyojitokeza juzi na kudumu kwa zaidi ya
saa saba, ilikuwa ni baada ya kundi la vijana
kufika eneo hilo kwa ajili ya kuchimba kaburi
kwa maziko ya ndugu yao na kukuta hali tofauti .
Inadaiwa walikuta baadhi ya makaburi
yamejengwa sehemu za kukaa wateja, choo
pamoja na banda kubwa la biashara lililosheheni
vinywaji. Aidha walikasirishwa na kile
kinachodaiwa kwamba ni kukuta pakiti tupu za
pombe zikiwa zimetapakaa juu ya makaburi
hayo.
Inadaiwa pia walikutwa wateja wakipata vinywaji
wakati huo saa 4 asubuhi huku baadhi wakiwa
wameweka miguu juu ya makaburi; kitendo
kilichoibua hasira ya vijana hao walioamua
kutoa taarifa Ofisi ya Mtendaji Kata ya Mkuti .
Mmiliki
Akizungumza kwa niaba ya mmiliki, Meneja wa
‘ baa ’ hiyo , Gasper Priscus alisema waliamua
kujenga kwenye eneo hilo kwa kuwa kiwanja
hicho wanakimiliki.
Alidai waliuziwa na mkazi wa Kitongoji cha
Roben mjini Masasi, Gerald Daudi . Kwa mujibu
wa meneja huyo, baada ya kuuziwa waliamua
kuanza ujenzi wa baa hiyo kwa haraka kwa
madai kuwa aliyewauzia, Daudi ni mgonjwa.
Priscus alisema walikuwa na hofu kwamba
endapo angefariki kabla ya kujenga baa hiyo ,
wangenyang’ anywa eneo hilo kwa kuwa
limeshazungukwa na makaburi.
Alikiri kwamba takribani wiki mbili sasa zimepita
tangu waanze biashara hiyo ya vileo kwenye
eneo hilo na kwamba wamekuwa wakipata
wateja wengi hasa usiku .
Akana kuuza
Hata hivyo Daudi; anayedaiwa kuuza eneo hilo
kwa Mtaro alikana kuliuza . Alisema aliamua
kumpa eneo hilo bure kwa jinsi anavyomsaidia
katika hali yake ya ugonjwa ambao umekuwa
ukimsumbua kwa muda mrefu sasa .
Akizunngumzia kuhusu kuondolewa kwa baadhi
ya misalaba kupisha ujenzi huo, Daudi aliyekuwa
akizungumza kwa taabu akiwa kitandani ,
alisema walikubaliana ing’ olewe mitatu pekee
kutoka kwenye makaburi ya familia yao.
Alisema uamuzi wa kung’ oa misalaba mingine
zaidi ya 10 ni uamuzi uliofanywa na
aliyemkabidhi eneo hilo.
Ofisa Mtendaji Ofisa Mtendaji wa Kata ya Mkuti ,
Moza Napachili alithibitisha ofisi yake kupokea
taarifa za kuwepo kwa mtu aliyejenga baa
kwenye eneo la makaburi.
Napachili alisema alikwenda kwenye eneo la
tukio akiongozana na Mwenyekiti wa mtaa huo
kutafuta suluhu ya mgogoro huo .
Baadaye kilifanyika kikao baina ya Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi,
Henry Kagogoro , Mtendaji wa Kata , wa Mtaa, na
Mwenyekiti wa Halmashauri pamoja na
anayedaiwa kuwa mmiliki wa baa hiyo , Mtaro .
Makubaliano yaliyofikiwa na kikao hicho ni
kutaifisha eneo hilo. Walikubaliana libaki chini ya
Halmashauri kwa ajili ya shughuli za maziko
pekee.
Hivyo iliamuriwa jengo hilo la baa na vibanda ,
viondolewe na mhusika, kesho awasilishe taarifa
Idara ya Ardhi zinazoonesha kuwa eneo hilo
analimiliki kihalali . Kaimu Mkurugenzi wa
Halmashauri alisisitiza eneo hilo la makaburi ni
mali ya Halmashauri .
Wateketeza kwa moto
Hata hivyo wananchi waliokuwa wamefika
kwenye makaburi hayo kwa ajili ya kuzika ndugu
yao, waliteketeza kwa moto vibanda vitano vya
kupumzikia vilivyoezekwa kwa makuti . Pia jengo
la baa lilibomolewa .
Polisi
Kwa upande wa Polisi, ilikiri kuwa na taarifa juu
ya mgogoro huo . Mkuu wa Polisi, Wilaya, Azaria
Makubi alisema wanaendelea na upelelezi
kuhusu tukio hilo.
MKAZI wa Mtaa wa Misufini, Kata ya Nyasa,
Halmashauri ya Mji Masasi mkoani Mtwara ,
Innocent Mtaro anatuhumiwa kujenga baa
katikati ya makaburi. |
0 comments:
Post a Comment