Wakati wa utawala wa Sir Alex Ferguson
katika klabu ya Manchester United alikuwa na
utaratibu wa kuwaalika baadhi ya makocha wa
timu pinzani kunywa mvinyo mara tu baada ya
kumalizika kwa mchezo wowote katika dimba
la Old Trafford.
Lakini chini ya utawala mpya wa kocha Louis
Van Gaal utaratibu huo wa Ferguson
umebadilika na tayari mmoja wa makocha
waliokuwa wamezoeshwa na Fergie kualikwa
kunywa mvinyo ametoa malalamiko yake.
Akiandika makala yake yaliyochapishwa
kwenye gazeti la Evening Standard, kocha wa
West Ham Sam Allardyce amesema
ameshangazwa na kusikitishwa na kitendo cha
kocha wa Manchester United Louis van Gaal
kutomualika kunywa mvinyo baada ya mechi
kati ya timu zao wikiendi iiyopita.
“Siku zote nilipokuwa nikienda Old Trafford
nilikuwa nikialikwa kwa ajili ya mazungumzo
kidogo pamoja na kunywa mvinyo.
“Huu utamaduni uliokuwepo kwa makocha wa
timu pinzani, ndio maana nilishangazwa na
kusikitishwa nilipotaarifiwa kwamba hakukuwa
na utaratibu ule tena baada ya mechi kuisha.
Niliambiwa utaratibu ule haupo tena, ikanibidi
kuondoka.” - Aliandika Alladayce. |
0 comments:
Post a Comment