Saturday, August 30, 2014

Baada ya Okwi kutangaza kujiunga na Simba,hiki ndicho walichokifanya Yanga.

Zikiwa siku chache zimepita toka klabu ya Simba kumtangaza Emmanuel Okwi kama mchezaji wao rasmi wa klabu hiyo,taarifa nyingine iliyotolewa leo na uongozi wa Yanga ni kumshitaki Okwi. Klabu ya Young Africans imemshitaki Emmanuel Okwi kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na kuwasilisha nakala kwa shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) na shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa kuingia mkataba na timu nyingine wakati akiwa bado ana mkataba wa miaka miwili na Yanga.

Posted via Blogaway

HIVI NI UMAARUFU, PESA AU MAPENZI YA KWELI YANAYOWAFANYA WADADA HAWA KUMPENDA DIAMOND??? TUJUZE

Ni kawaida ya dada zetu hapa Tz,siyo wote ila ni baadhi yao kujigonga kwa mtu yeyote pale apatapo umaarufu,haijalishi alikuwa handsome au mtu wa kawaida,ni pale tu anapoanza kupata jina ndio unaona idadi ya watu wanaongezeka si tu wadada yani hadi idadi ya marafiki huongezeka pale mtu apatapo umaarufu,ila kwa Diamond Platnumz wamembatiza hadi jina na kumuita sukari ya warembo,Jina hili limetokana na jinsi wadada zetu wanavyompenda msanii huyu tena ile zaidi ya kimuziki. Aliyempa jina la sukari ya warembo hakukosea kabisa cause hivi sasa Diamond Platnumz si yule wa zamani wa mbagala tena ambaye kila mtu alikuwa anamdharau,pale kabla hata hajatoka kulinganisha na hivi sasa. ni mfululizo wa wadada walioteyari kuuza roho zao kupata attention kutoka kwa mwanamuziki huyu,ila swali la kujiuliza ni mapenzi ya kweli au ni umaarufu tu alionao ndio kinachotengeneza sukari hiyo,unaweza kusema labda ni zile Benjamins(money) alizonazo ndio zinaongeza utamu wa sukari hiyo..well,nobody seem to know the answer…ila mbali ya hayo yote mwisho wa siku ni kukubali tu the guy anaweza. Kati ya mwanamuziki anayeongoza kuwa na ladies skendo basi huyu raisi wa wasafi hawezi kusahaulika hata kwabahati mbaya,cause for the past year tumeweza kusikia that amedate na wadada kama watatu hivi,mbali na rumors zile za hapa na pale ambazo hazina uthibitisho kwamba ni kweli au si za kweli,he has been on and off to these ladies. Ni Raisi wa wasafi,Diamond Platnumz aliyeweza kujipatia umaarufu mkubwa kutokana na kipaji chake cha kutoa hit tracks nzuri zilizoteka nyoyo za mashabiki wa kila rika na kila nchi hapa africa na nje ya africa, kokote kule wasikiapo track kali za mwanamuziki huyu,ni umaarufu uliotokana na juhudi alizonazo pamoja na kipaji chake mwenyewe ndicho kilichopelekea kupata umaarufu huu ndani ya muda mfupi tu.

Credit vibe


Posted via Blogaway

PERUZI KURASA ZA MBELE NA NYUMA ZA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI HAPA

CHEKI BALOTELLI ANAVYOFURAHIA MAISHA LIVERPOOL, UTAFIKIRI MWENYEJIII

BARUA INAYOVUNJA MKATABA WA YANGA NA OKWI HII YAPA

SIKIA HII KALI YA MANJI KUTAKA AWANUNUE WACHEZAJI WA SIMBA, HALAFU WASICHEZE LIGI

Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji, leo ametoa kali kwenye kikao chake na waandishi wa habari aliposema kwamba ana uwezo wa kuwanuanua wachezaji wa Simba, halafu wasicheze ligi na badala yake wawe wanafanya mazoezi Covo Beach tu. Manji amesema hayo wakati akipinga Simba kutangaza kumsajili mshambuliaji Emmanuel Okwi. Manji amesema suala hilo ni sawa na uhuni kwa kuwa Simba inajua Okwi ana mkataba na Yanga. “Kama itakuwa ni kufanya mambo kwa staili ya kihuni, hata mimi ninaweza kuamua kuwanunua wachezaji wa Simba sijui kina (Amissi) Tambwe na wenzake, halafu wawe wanafanya mazoezi Coco Beach tu, wasicheze ligi. “Lakini busara ni jambo jema, lakini nione kwamba ninachofanya ni kitu gani na hasara zake ni zipi. “Umesikia sisi (Yanga) tumelalamika kuhusiana na usajili wa Domayo au Kavumbagu kwenda Azam FC. Kila kitu kilikwenda kwa utaratibu. “Hata Simba wanaosema kuhusiana na suala la Okwi pia hawajui, sisi hatukuzozana na Simba, utaona Okwi wakati anakuja Yanga tulifuata utaratibu na kumalizana na SC Villa. “Simba hawakuwa na tatizo na Okwi, badala yake Etoile du Sahel ya Tunisia ambayo Yanga hatukufanya nao biashara. Hakukuwa na sehemu ambayo inatugonganisha,” alisema. “Sasa kama kuna lengo la kufanya ili kuikomoa au kuona ni kulipa kisasi, basi ni kujidanganya tu na kutaka kufanya mambo yaende kwa kukomoana ambalo si jambo zuri. “Ndiyo maana tumetoa siku saba tuwaachie TFF washughulikie madai yetu, ikishindikana, Caf, Fifa au Cas bado ni sehemu tunazoweza kwenda,” alisisitiza Manji. “Pia kusema Okwi amevunja mkataba nasi ni kujidanganya. Iko wapi barua aliyonayo yeye kwamba tumevunja naye mkataba. “Hata majina tumetuma sita, tungejua lipi la kulitoa kwa kuwa hadi Septemba 6 ndiyo mwisho wa kusajili wageni. Haraka ya nini

Posted via Blogaway

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO JUMAMOSI ZIPO HAPA

Real Madrid wamekamilisha uhamisho wa pauni milioni 20 wa Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco (Calciomercato), Arsenal wana matumaini ya kukamilisha uhamisho wa beki Sorkatis Papastathopoulos, 26, kutoka Borussia Dortmund, lakini wamesema hawatalipa pauni milioni 20 (Daily Mirror), boss wa Aston Villa Paul Lambert ametoa dau la pauni milioni 8 kumtaka kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 25, (Daily Telegraph), lakini Lambert huenda wakapata upinzani mkali kutoka Valencia, ambao nao pia wamepanda dau kwa Cleverly (Sky Sports), Danny Welbeck, 23, anajiandaa kuondoka Old Trafford, na akitajwa kwenda Tottenham kwa mkopo (Daily Star), Chelsea wanakaribia kutoa ruhusa kwa Fernando Torres, 30, kwenda Inter Milan (Times), Manchester United wameongeza bidii kumfuatilia kiungo Martin Odegaard, 15, anayechezea Stromsgodset kutoka Norway (Daily Telegraph), Valencia na Juventus wametoa dau la kutaka kumsajili Javier Hernandez, 26, kutoka Manchester United kwa kiasi cha pauni milioni 15 (Guardian), mshambuliaji Demba Ba, 29, alikaribia kujiunga na Arsenal kabla ya kusaini kwenda Besitkas ya Uturuki kutoka Chelsea kwa pauni milioni 8 (Independent), kiungo anayesakwa na Manchester United Arturo Vidal, 27, amekaririwa akisema hataki kuondoka Juventus (Daily Express), kiungo wa zamani wa Arsenal Alex Song, 26, ana matumaini ya kurejea katika Premier League na Liverpool baada ya Barcelona kuonekana kutomtaka (Daily Mirror), kiungo wa PSG Adrien Rabiot ambaye mkataba wake unaisha msimu ujao anasakwa na Roma na Arsenal (Le Parisien). Zimesalia siku mbili kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. By salim kikeke

Posted via Blogaway

Je Toni Kroos ndio kamkimbiza Alonso Madrid? Xab Alonso ajibu.

Kiungo wa kimataifa wa Spain Xabi Alonso amejiunga na klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani akitokea kwa mabingwa wa ulaya Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 5. Alonso ambaye alijunga na Real Madrid akitokea Liverpool ametambulishwa rasmi leo hii kwenye mkutano waandishi wa habari na kutoa sababu ambayo imemfanya mpaka akaamua kuondoka Santiago Bernabeu. Kiungo huyo ambaye juzi alitangaza kujiuzulu kuichezea timu ya taifa ya Hispania amesema kwamba kilichomfanya kuhama Madrid sio upinzani wa namba kama inavyodhaniwa na wengi. “Klabu haikutaka niondoke, ulikuwa uamuzi wangu mwenyewe kuondoka. Baada ya kushinda La Decima, nilihisi nahitaji changamoto mpya. Nilihisi muda wa kuondoka umefika,” Alonso aliwaambia waandishi wa habari. “Sikuamua kuondoka kwa sababu ya ujio wa Toni Kroos. Madrid wamefanya usajili mzuri sana na tungecheza wote kwa muda mwingi. Hivyo sikuondoka kwa sababu yake, nilihitaji tu changamoto mpya. “Bayern ndio lilikuwa chaguo sahih kwangu mimi.” – Alonso

Posted via Blogaway

Alichojibu Ronaldo kuhusu Di Maria kujiunga na Man Utd na kupewa jezi namba 7

Siku moja baada ya Angel Di Maria kutambulishwa rasmi kama mchezaji wa klabu ya Manchester United ya England huku akikabidhiwa jezi yenye historia kubwa ndani ya klabu hiyo (namba 7), mwanasoka bora wa ulaya na mchezaji wa zamani wa United, Cristiano Ronaldo amezungumza juu ya Di Maria kwenda Old Trafford pamoja na kupewa jezi namba 7. Ronaldo ambaye aliondoka Man United mnamo mwaka 2009 kwa ada ya uhamisho ambayo iliweka rekodi ya £80m amesema hana wasiwasi wa Di Maria kufanikiwa ndani ya United. “Uhamisho huu ni kitu kizuri kwake.” Ronaldo aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Monaco. “Manchester [United] ni moja ya klabu kubwa duniani, ni sehemu nzuri kwa Di Maria na namtakia kheri na mafanikio, Di Maria ni mchezaji mzuri sana, anastahili kuichezea United.” Alipoulizwa juu ya Di Maria kupewa jezi namba 7 aliyokuwa akivaa alipokuwa Man United, Ronaldo alisema: “Nilimwambia, ‘jezi No.7 ina maana kubwa ndani ya United, lakini nadhani ataweza kubeba uzito wa jezi kwa sababu ni mchezaji mzuri sana.” Di Maria anaweza kuanza kuichezea Man U kesho kwenye mchezo dhidi ya Burnley.b

Posted via Blogaway

Shinji Kagawa njiani kuondoka Man United – hii ndio klabu anayoenda

Wakati wa utambulisho rasmi wa Angel Di Maria jana, kocha qa man United Louis Van Gaal alithibitishqa kwamba kuna kundi la wachezaji litaondoka mpaka kufikia mwishoni mwa wiki hii. Leo hii zimetoka taarifa kwamba kiungo wa kimataifa wa Japan, Shinji Kagawa ni mmoja wa wachezaji wanaondoka kwenye klabu hiyo kabla ya kuisha kwa dirisha la usajili. Shinji anatarajiwa kujiunga na klabu yake ya zamani ya Borrusia Dortmund kwa ada ya uhamisho wa £8m. Mchezaji huyo anatarajiwa kuwasili Ujerumani leo hii tayari kwa kufanyiwa vipimo vya afya ili kukamilisha usajili wake Dortmund. Kagawa alijiunga na Man United miaka mitatu iliyopita kwa ada ya uhamisho wa £12m.

Posted via Blogaway