Monday, August 25, 2014

MESSI AANZA LA LIGA NA BAO 2, BARCA YASHINDA 3, MASCHERANO AANZA NA KADI NYEKUNDU

BARCELONA IMEITUNGUA ELCHE KWA MABAO 3-0 HUKU MSHAMBULIAJI WAKE NYOTA, LIONEL MESSI AKIPIGA MAWILI. MESSI ALIFUNGA MABAO YAKE KILA KIPINDI AKIANZA LA KWANZA KATIKA DAKIKA YA 42 NA LA PILI KATIKA DAKIKA YA 64. KABLA YA HAPO, KINDA MOHAMMED MUNIR ALIKUWA AMEIFUNNGIA BARCA BAO KATIKA DAKIKA YA 46. BARCELONA IMEICHAPA ELCHE HUKU IKIWA PUNGUFU BAADA YA BEKI WAKE JAVIER MASCHERANO KULAMBWA KADI NYEKUNDU KATIKA DAKIKA YA 44 TU. KWA USHINDI HUO MAANA YAKE, BARCELONA IMEANZA VIZURI LA LIGA CHINI YA KOCHA LUIS ENRINQUE.

VAN GAAL AMTETEA YOUNG, ASEMA HAKUJIRUSHA BANA!

Kocha Louis van Gaal amesema kiungo wake wa pembeni, Ashley Young hakujirusha makusudi kupata penalti katika mechi dhidi ya Sunderland iliyomalizika kwa sare ya mabao 1-1. Beki Wes Brown aliuondoa mguu wake wakati anakutana na Young lakini akaanguka na mwamuzi Martin Atkinson akamlamba kadi ya njano.

HUYU NI LILIAN KUTOKA MBEYA,RASMI AMETUA DAR KWAAJILI YA KUINGIA KWENYE TASNIA!!!

Wadau wa Bongo Movie
Tumpokee!!!

UNAWEZA KUZIELEZEAJE PICHA HIZI!!!! MAKUSUDI AU BAHATI MBAYA?

ANGALIA FIGO, KAREMBEU 'WALIVYOICHAFUA' KANZU YA JULIO

Figo na Karembeu, wala hawakujivunga wakiwa na mmoja wa viongozi wao wa benchi la ufundi, wakaweka saini zao hatua kwa hatua. Jambo hilo lilionekana kumfurahisha zaidi Julio ambaye alitumia dakika kadhaa kuziangalia saini hizo huku akitabasamu.
Baadhi ya wadau waliokuwa eneo hilo walikuwa akimtania kwamba atabaki na kanzu hiyo bila ya kuifua, lakini naye alitia mbwembwe kwa kuwajibu: “Hii si saini ya kwanza ya Figo, nina jezi pia ameweka saini yake, tena aliweka kule Hispania. Nililetewa na mwanangu Supa.”
Wachezaji nyota, Luis Figo na Cristian Karembeu wa kikosi cha wakongwe cha Real Madrid, wakiichafua kanzu ya beki na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwa kuweka saini zao. Wakongwe hao wawili wa Real Madrid waliokuwa hapa nchini na kikosi hicho kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven, walifanya hivyo wakati Julio alipoomba waweke saini zao kwenye kanzu yake.

Kama bado ujajiunga nasi>>>>>>>>>>>>>>> Ingia hapa 

:picha na salley jembe

Kauli ya Carlo Ancelotti kuhusu Di Maria kuaga wenzake leo hii

Sakata la usajili wa winga wa kimataifa wa Argentina Angel Di Maria kwenda klabu ya Manchester United limechukua sura mpya leo hii. Kwenye mkutano wa waandishi wa habari wa kocha wa Real madrid Carlo Ancelotti amethibitisha mchezaji huyo yupo karibuni kuhama. Di Maria leo hakufanya mazoezi na wenzake na badala yake alienda kuwaaga wachezaji pamoja na viongozi wengine wa Madrid. “Alikuja leo asubuhi, lakini hakufanya mazoezi. Uhamisho wake bado haujakamilika wote ila anakaribia kuhama kabisa. “Tunamshukuru kwa kila alichoifanyia hii klabu na tunamtakia kila kheri huko anapokwenda, uhamisho haujakamilika rasmi, ila kila kitu tumeshakubaliana,” – Ancelotti alisema. Ingawa Ancelotti hakuitaja timu anayoenda Di Maria lakini vyombo vya habari ulaya vinaripoti kwamba DI Maria atakuwa mchezaji mpya wa Man united kwa ada ya £64 million.

JAMANI JAMANI NAMNA GANI TENA??? ANATAKA NINI HUYU?

Sasa tukiposti mnasema tuna
wazalilisha ......

BAADA YA JAJA NAYE COUTINHO AFUNGUA AKAUNTI YA MAGOLI YANGA FC

Mohamed Abdallah, Zanzibar Andrey Coutinho amefanikiwa kupiga bao na kuisaidia Yanga kuifunga Shangani inayoshiriki Ligi Daraja la Pili hapa. Yanga imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, moja likiwa limesababishwa na Salum Telela ambaye alipiga krosi safi mabeki wa Shangani wakajifunga. Mechi hiyo kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa, ilikuwa nzuri nay a kuvutia. Coutinho alionekana kuwa fiti zaidi huku Mbrazili mwenzake, Jaja akibanwa. Yanga ilicheza kwa kuelewana tokea mwanzo, lakini baadaye Shangani nao walijibu mashambulizi na kuifanya mechi kuwa ya ushindani. Chini ya Marcio Maximo, Yanga itacheza mechi nyingine moja ya kirafiki Jumatano kabla ya kurejea jijini Dar.

SIMBA SC YAIJIBU YANGA SC, YAUA 2-1 AMAAN USIKU HUU

Mohamed Abdallah, Zanaibar Kikosi cha Simba kinachoongozwa na Patrick Phiri, kimeishinda Kilimani ya daraja la pili Zanzibar kwa mabo 2-1 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa. Ingawa ina kikosi kinachoundwa na Kilimani wengi kweli, Chipukizi ilionyesha soka safi na la kuvutia. Timu hiyo inasifika kwa soka la kasi na pasi nyingi ikiwa Simba wakati mgumu kwa muda mwingi. Simba ndiyo ilianza kupata bao kupitia Amissi Tambwe kwa mkwaju wa penalti lakini Kilimani wakasawazisha katika dakika ya 78. Simba walifanikiwa kupata bao la pili katika dakika ya 84 kupitia Haruna Chanongo.NA MDADISI BLOG /FESTOSAIMON

MAN UNITED, REAL MADRID ZAMALIZANA KWA DI MARIA, ANATUA LEO ENGLAND

Real Madrid imekubali kumuachia Angelo Di Maria ambaye anatua Man United kw akitita cha pauni milioni 64. Uhamisho wake utavunja rekodi na kuwa ghali zaidi England ukiupita ule wa pauni milioni 50 wakati Fernando Torred alipotua Chelsea akitokea Liverpool. Di Maria raia wa Argentina, anatarajia kutua jijini Manchester leo kwa ajili ya vipimo na kumalizana na wenyeji wake. Kocha Carlo Ancelotti wa Madrid amethibitisha kwamba mkali huyo alikwenda kuwaaga mazoezini kwamba anaondoka. Man United imekuwa ikifanya juhudi kujiimarisha baada ya kusuasua kwa msimu mzima na pia kuanza vibaya msimu mpya kwa kipigo na sare dhidi ya Swansea na Sunderland. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON