Monday, August 25, 2014

ANGALIA FIGO, KAREMBEU 'WALIVYOICHAFUA' KANZU YA JULIO

Figo na Karembeu, wala hawakujivunga wakiwa na mmoja wa viongozi wao wa benchi la ufundi, wakaweka saini zao hatua kwa hatua. Jambo hilo lilionekana kumfurahisha zaidi Julio ambaye alitumia dakika kadhaa kuziangalia saini hizo huku akitabasamu.
Baadhi ya wadau waliokuwa eneo hilo walikuwa akimtania kwamba atabaki na kanzu hiyo bila ya kuifua, lakini naye alitia mbwembwe kwa kuwajibu: “Hii si saini ya kwanza ya Figo, nina jezi pia ameweka saini yake, tena aliweka kule Hispania. Nililetewa na mwanangu Supa.”
Wachezaji nyota, Luis Figo na Cristian Karembeu wa kikosi cha wakongwe cha Real Madrid, wakiichafua kanzu ya beki na kocha wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ kwa kuweka saini zao. Wakongwe hao wawili wa Real Madrid waliokuwa hapa nchini na kikosi hicho kwa ajili ya kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven, walifanya hivyo wakati Julio alipoomba waweke saini zao kwenye kanzu yake.

Kama bado ujajiunga nasi>>>>>>>>>>>>>>> Ingia hapa 

:picha na salley jembe

0 comments:

Post a Comment