Sakata la usajili wa winga wa
kimataifa wa Argentina Angel Di
Maria kwenda klabu ya
Manchester United limechukua
sura mpya leo hii.
Kwenye mkutano wa waandishi wa
habari wa kocha wa Real madrid
Carlo Ancelotti amethibitisha
mchezaji huyo yupo karibuni
kuhama.
Di Maria leo hakufanya mazoezi na
wenzake na badala yake alienda
kuwaaga wachezaji pamoja na
viongozi wengine wa Madrid.
“Alikuja leo asubuhi, lakini
hakufanya mazoezi. Uhamisho
wake bado haujakamilika wote ila
anakaribia kuhama kabisa.
“Tunamshukuru kwa kila
alichoifanyia hii klabu na
tunamtakia kila kheri huko
anapokwenda, uhamisho
haujakamilika rasmi, ila kila kitu
tumeshakubaliana,” – Ancelotti
alisema.
Ingawa Ancelotti hakuitaja timu
anayoenda Di Maria lakini vyombo
vya habari ulaya vinaripoti
kwamba DI Maria atakuwa
mchezaji mpya wa Man united kwa
ada ya £64 million. |
0 comments:
Post a Comment