Saturday, August 23, 2014

ANGEL DI MARIA SASA ANUKIA KABISAAA! MAN UNITED

Aliachwa: Angel Di Maria hakupangwa katika kikosi cha Real Madrid kilichokabiliana na Atletico Madrid jana usiku. CARLO Ancelotti amethibitisha kuwa mchezaji anayewaniwa kwa nguvu zote na Manchester United, Angel Di Maria aliachwa katika kikosi cha jana kwenye mchezo wa marudiano wa Spanish Super Cup dhidi ya mahasimu wake, Atletico Madrid na kupoteza kombe la kwanza msimu huu kwa sababu za kimpira na si vinginevyo. “Aliachwa katika kikosi kwa sababu za kimpira” Alisema Ancelotti alipoulizwa kwanini hajampanga Muargentina huyo hata katika orodha ya wachezaji wa akiba jana uwanja wa Vicente Calderon. Kitendo cha Di Maria kutopangwa jana kinaashiria uhusiano na kocha Ancelotti umefikia hali mbaya na ni sababu tosha kwa Manchester United kumnasa kwa ada inayoaminika kuwa paundi milioni 50. Ancelotti alithibitisha kuwa nyota huyo wa Argentina katika fainali za kombe la Dunia majira ya kiangazi mwaka huu ameomba kuondoka Real Madrid. Mashabiki wa Real Madrid wameiacha klabu katika wasiwasi kwasababu wanamhitaji Di Maria kubakia, lakini Rais Florentino Perez anataka auzwe ili kuweka sawa mahesabu baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili Toni Kroos na James Rodrgiguez. Madrid walibaki katika utata mkubwa kutokana na mashabiki waliohudhuria Santiago Bernabeu siku ya jumanne kulipuka kwa shangwe wakimshangilia Di Maria baada ya kuingia uwanjani kipindi cha pili akitokea benchi. Ancelotti alithibitisha ijumaa kuwa mchezaji amekataa kusaini mkataba mpya na ameomba kuondoka.Na mdadisiblog/festosaimon

HII NDO RATIBA YA EPL WIKIENDI HII

Simba inatia raha, Phiri amchezea akili Maximo

KOCHA mwenye heshima kubwa ndani ya Simba na ambaye amekabidhiwa jukumu la kuiongoza timu hiyo msimu ujao, Mzambia Patrick Phiri, ametumia Mwanaspoti kuwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba washushe pumzi mambo ni mazuri. Amewasisitiza kwamba wasiwe na wasiwasi kwa vile kila kitu kipo sawa na heshima lazima irudi Msimbazi kwani ratiba ya Ligi Kuu Bara ameshaipata na wala haimsumbui. Katika mazoezi ya jana Ijumaa yaliyofanyika Uwanja wa Chuoni Chukwani, Phiri alisema wachezaji wake wanapokea kwa kiasi kikubwa mafunzo yake na anapenda kuona wanavyomiliki mipira, kukaba na kushambulia. Alichofanya jana ni kuwapunguzia muda wa mazoezi ambayo awali alikuwa akitumia saa nne na sasa anatumia saa tatu ili wapate muda wa kutafsiri mafunzo yake kambini na kutuliza akili. “Nafurahi kwa sababu naona wachezaji wananielewa kila ninachokihitaji, inanipa moyo sana kwamba msimu ujao tutafanya vizuri, nimetumia muda mwingi kuwafundisha jinsi ya kumiliki mipira, kukaba na kushambulia, kesho (leo Jumamosi) watafanya kidogo tu ili mwili ukae sawa tayari kwa mechi ya Jumapili dhidi ya Kilimani City (ya Daraja la Pili Zanzibar),” alisema Phiri. Akizungumzia maandalizi yake ya Ligi Kuu, alisema kuwa ameiona ratiba na mpangilio wake ni mzuri kwani watacheza mechi nyingi nyumbani katika mzunguko wa kwanza ila amesisitiza mechi yenye presha kuwa ni dhidi ya Yanga itakayochezwa Oktoba 12 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. “Ratiba imepangwa vizuri, tunatakiwa kushinda mechi zote lakini kwa uelewa wangu katika Ligi hii ya Tanzania mechi ya Yanga ina presha kubwa kwani ina mambo mengi sana hata kabla ya mechi kuchezwa, lakini tutajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema Phiri. AMCHEZEA AKILI MAXIMO Katika kile ambacho ni kuonekana kumchezea akili kocha wa Yanga, Marcio Maximo, kama wanavyofanya makocha mahiri wa Ulaya, Phiri amedai kukerwa na ujio wa Yanga mjini Unguja. Yanga ilikuwa kambini Pemba lakini leo Jumamosi inatua Unguja na Kesho itacheza na KMKM kwenye Uwanja wa Amani. Phiri amedai hajafurahia Yanga kuamua kucheza mechi hiyo dhidi ya KMKM siku ambayo wao wana mechi katika uwanja huo wa Amani, mechi ya Yanga itaanza saa 10:00 jioni wakati ya Simba itaanza saa 2:30 usiku dhidi ya Kilimani. Phiri aliliambia Mwanaspoti kwenye kambi ya timu hiyo mjini hapa akisema: “Najaribu kuangalia itakuwaje kwani sisi ndio tumeanza kuja hapa na kutoa taarifa kuwa siku ya Jumapili tutakuwa na mechi, iweje Yanga nao wanataka wacheze siku hiyo hiyo? Kama uwanja usingekuwa mmoja hapo sawa, lakini nao wanataka kucheza uwanja ambao tutautumia.Credit mwanaspoti

Habari zingine za michezo BONYA HAPA 

Panga pangua, hii ndio Yanga mpya

HII ni siri usimwambie mtu yeyote, uchune nayo hivyo hivyo kwa vile bado Marcio Maximo hajaweka wazi kikosi chake cha kwanza lakini tathmini ya Mwanaspoti imekibaini. Kwa mujibu wa mazoezi yaliyofanyika Dar es Salaam na hapa Pemba jumlisha na mechi ya kirafiki waliyocheza, ‘First Eleven’ ya Yanga itakuwa kama ifuatavyo; Kipa ni Deo Munishi ‘Dida’ kama kawaida na Juma Abdul atacheza beki ya kulia. Kushoto ni Oscar Joshua lakini Edward Manyama na Amos Abeil anaocheza nao nafasi moja ni hatari sana, Maximo anaweza akawatumia kwa kuchanganya kulingana na timu pinzani. Beki ya kati ni Kelvin Yondani ‘Vidic’ na Nadir Haroub ‘Cannavaro’, kiungo mkabaji ni Mnyarwanda Mbuyu Twite na kiungo mshambuliaji ni Hassan Dilunga. Panga pangua Mbrazili Andrey Coutinho atacheza winga ya kushoto na Mnyarwanda Haruna Niyonzima atacheza winga ya kushoto, mastraika wa kati ni Mrisho Ngassa anayecheza kama kiungo nyuma ya Genilson Santos Santana ‘Jaja’. Kwenye nafasi za mbele, kiungo, winga na straika mambo yanaweza kubadilika kulingana na aina ya timu pinzani watakayocheza nayo. Kwani wachezaji kama Simon Msuva anaweza kutumika kucheza winga ya kulia kama anataka timu icheze kwa kasi zaidi, Jerry Tegete, Hamis Kiiza raia wa Uganda, Said Bahanuzi na Hussein Javu nao wanaweza kumpeleka Ngassa pembeni, kama atataka kucheza mpira wa kutulia. Maximo amesisitiza kuwa katika mechi hizi za majaribio, anataka kuwatumia wachezaji wote ili awaone na ndivyo anavyowapa nafasi. Ametengeneza ‘First Eleven’ mbili ambazo huchuana zenyewe kwa wenyewe na hao ndiyo watatoa kikosi halisi cha kwanza ambacho mwenyewe hajakiweka wazi. “Kwa sasa nampa kila mchezaji nafasi ya kucheza, lengo ni kuwaona namna wanavyocheza na muunganiko wa kombinesheni ipi inakubali kupata kitu fulani kulingana na mechi,” alisema Maximo. Maximo alitumia muda wa takribani robo saa akizungumza na wachezaji na baadaye walifanya mazoezi ya kukimbia na baadaye mafupi ya kucheza mpira. Katika mazoezi hayo, kiungo Hassan Dilunga, alishindwa kufanya mazoezi na wenzake kwani alikuwa anasikia maumivu kwenye kidole cha mwisho cha mguu wa kulia kwani alijitonesha kwenye mechi ya juzi Alhamisi na Chipukizi. Credit mwanaspoti

Kusoma habari nyingine BONYEZA HAPA 

UCHAWI, SAFARI ZA KUZIMU NA MASWALI YA AIBU KWA WASHIRIKI WA BIBI BOMBA VYAIPONZA CLOUDS FM NA CLOUDS TV.....TCRA YAWALIMA FAINI YA MILIONI 5

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), imetoa onyo pamoja na kutoza faini ya takribani Sh milioni 5 kwa kituo cha redio na televisheni cha Clouds, kwa kukiuka kanuni za utangazaji za mwaka 2005. Wakielezea uamuzi huo jana jijini Dar es Salaam, Kamati ya Maudhui ya mamlaka hiyo ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Margaret Munyagi ilisema kuwa ukiukwaji wa kanuni hizo ulifanywa kwa nyakati tofauti na vituo hivyo. Alisema kwa upande wa kituo cha redio cha Clouds, kupitia kipindi chake cha ‘Njia Panda’ kilichorushwa hewani Juni 15 mwaka huu kati ya saa 8.00 mchana na saa 10.00 jioni kilikuwa na mada iliyohusu safari ya kuzimu ambapo maudhui yake yalijaa simulizi za kufikirika, za kishirikina na kichawi. Aidha alisema kosa lingine kituo hicho hakikufuata kanuni za Utangazaji(maudhui) za mwaka 2005 zinazowataka kuwasilisha ratiba ya vipindi vyao kwa TCRA ili viidhinishwe na vilevile kuvichapisha katika gazeti kabla ya kurushwa hewani ambapo kipindi cha Njia Panda hakikuwasilishwa kwa ajili ya kuidhinishwa. Wakati huo huo, kituo cha televisheni cha Clouds kilirusha kipindi cha ‘Bibi Bomba’ Mei 16 na Juni 6 mwaka huu kati ya saa 3.00 na saa 4.00 usiku ambacho kilikiuka kanuni za Utangazaji (maudhui) za mwaka 2005. Alisema kipindi hicho kilidhalilisha mabibi hao walioshiriki pamoja na wanawake kwa ujumla kutokana na maswali ya aibu waliyokuwa wakiulizwa na waamuzi wa shindano hilo ambayo ni kinyume na kanuni hizo. Aidha alisema kituo hicho kinatozwa faini ya Sh milioni moja na kutakiwa kuwasilisha TCRA mwongozo wa kuchuja na kusimamia maudhui yasiyofaa kabla ya kutangazwa. TCRA imesema kama Kanuni za Utangazaji zitaendelea kukiukwa hatua kali zaidi za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO JUMAMOSI ZIPO HAPA

Juventus na Roma wanataka kumsajili beki wa kati wa Manchester City Matija Nastasic, 21, huku Newcastle na West Ham wakimtaka beki wa kulia wa Man City Micah Richards, 26, (Manchester Evening News), Manchester United wanaongoza mbio za kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26 baada ya mabingwa wa Ufaransa PSG kuamua kujitoa (Daily Star), lakini Di Maria huenda asiende United kwa sababu Louis van Gaal hataki kukwaza ukuaji wa Adnan Januzaj, 19, (Daily Express), Tottenham wanajiandaa kutoa pauni milioni 11 kumchukua mshambuliaji wa QPR Loic Remy, 27, (Daily Star), Arsenal wanafikiria kupanda dau kumchukua beki wa West Ham Winston Reid, 26, ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao (Daily Star), Hull City wameongeza dau kumchukua mshambuliaji wa Blackburn Jordan Rhodes, 24 (Daily Mail), kiungo wa Manchester United Anderson, 26, huenda akahamia Sporting Lisbon kwa pauni milioni 5.5 (Daily Express), boss wa Southampton Ronald Koeman amesema kiungo wake Morgan Schneiderlin, 24 hauzwi kwa bei yoyote (London Evening Standard), beki wa QPR Rio Ferdinand, 35, anataka kuwa meneja wa England akistaafu kucheza (Daily Mail), Newcastle United wana uhakika nahodha wao msaidizi Cheick Tiote, 28 hatoondoka licha ya timu nyingi kumnyatia (Sunderland Echo), boss wa Arsenal Arsene Wenger anaamini Jack Wilshere, 22, anatolewa kafara kwa England kushindwa kufanya vizuri katika Kombe la Dunia (Sun), wakati huohuo Aaron Ramsey, 23, ana uhakika Arsenal wataweza kupambana "kwa misuli" na Manchester City na Chelsea msimu huu (Sky Sports), Barcelona wamefanya jaribio la kushangaza la kumtaka Angel Di Maria kutoka Real Madrid. Real walifikiria dau la pauni milioni 48 lakini mazungumzo ya awali yalivunjika baada ya Los Bloncos kutotaka kuwauzia mahasimu wao (Sport), Napoli wanamtazama Fabio Borini wa Liverpool, ambaye kuwasili kwa Mario Balotelli huenda kukasaidia kufanikisha uhamisho wake (Tuttosport), dau la Manchester United kumtaka Nicolas Gaitan limekataliwa na Benfica (Record), Arsenal wanafikiria kumchukua William Carvalho kutoka Sporting, huku Sami Khedira anaweza kwenda Emirates iwapo atashusha madai ya mshahara mkubwa (Daily Telegraph), AC Milan wanajiandaa kumtaka mshambuliaji wa Tottenham Roberto Soldado kuziba pengo la Mario Balotelli anayeelekea Liverpool. Spurs watamruhusu Soldado kuondoka na nafasi yake kuzibwa na Loic Remy kutoka QPR (Daily Mail), Manchester United na Zenit St Petersburg wapo tayari kupambana kumwania kiungo wa Inter Milan Fredy Guarin (Corriere dello Sport), Barcelona wanatumaini kukamilisha usajili wa Marco Reus kutoka Bayern Munich. Maafisa wa Bayern wana wasiwasi kuwa huenda mchezaji huyo tayari amekubali kujiunga na Catalans ambao huenda wakafungiwa kusajili (Mundo Deportivo). Zimesalia siku 10 kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa..

KWELI HAKUNA JIPYA HAPA DUNIANI.....EBU TAZAMA HII ENZI YA MWALIMU!!!

Siku hizi hizi social media ndio zinakuza mambo...hawa kina LULU , WEMA walikuwepo toka kitamboooo!!!

New AUDIO | Oscar nyerere Na Dr Mfyuzi Ft Ally Nipishe - Amani | Download

Wimbo huu Umeimbwa na baadhi ya waigizaji sauti nchini yani Oscar Petro maarufu kama Oscar nyerere na Shaphii Omary maarufu kama dr.mfyuzi unaosisitiza Amani ya nchi yetu Tanzania kwa kutumia sauti ya hayati Baba wa Taifa na sauti ya raisi wa awamu ya nne dr Kikwete. Wimbo una mahadhi ya kuhutubia lakini pia una chorus iliyoimbwa na Ally Nipishe toka THT. Video ipo njiani inayotarajiwa kutoka mwishoni mwa mwezi huu wa nane 2014.BONYEZA APO CHINI KUDOWNLOAD

>>›> BONYA HAPA KUDOWNLOAD <<<<<<‹<‹

HATIMAYE DIAMOND PLATINUMZ AMETANGAZA NDOA NA MCHUMBA WAKE WA MUDA MREFU WEMA SEPETU!!!!

KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti ambalo kwa mujibu wa takwimu za mauzo nchini ni wazi kwamba halina mpinzani, msanii wa muziki wa kizazi kipya Diamond Platinumz ametangaza ndoa na mchumba wake wa muda mrefu Wema Sepetu anayosema itafungwa hivi karibuni. Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa sasa, ametamka hayo alipozungumza na Mwanaspoti nyumbani kwake Sinza jijini Dar es Salaam juzi Jumatano. Alisema kuna mambo mengi yaliyomchelewesha kufikia hatua hiyo, ikiwamo maandalizi kwani amepanga mashabiki wake wahudhurie harusi hiyo. “Ndoa ni kitu cha heri na baraka, lakini kitu kinachofanya kidogo mambo yachelewe ni kwamba sisi au mimi ni mtu ninayefahamika, kwa hiyo hata ndoa yangu watu wengi wanatamani waihudhurie,” alisema Diamond. Pia amesisitiza kwamba ndoa si jambo la masihara kwani ni tendo la kiimani na ndio maana amekuwa makini katika mipango yake. “Nataka kila kitu kishuhudiwe na mashabiki, ninaweza hata kuifanyia Uwanja wa Taifa,” aliongeza. “Unajua nilishindwa kufanya mambo haya haraka kwa sababu wengi nadhani wangeamini kwamba ninafanya hivyo ili kutafuta umaarufu zaidi, tunataka tufanye kiusahihi yasije tokea mambo kama ya Instagram tunataka tuje kuwa mfano wa kuigwa.” Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo Diamond alisema: “Nilishasema ni hivi karibuni, unajua siku zote vitu vya kheri waswahili wanasema lazima uvifiche, hata Mwenyezi Mungu naye anasema anampenda mtu aliye na siri, lazima vitu vingine uvifiche ili vipate kufanikiwa. Wakati mwingine kunakuwa na husda, hasidi kwa hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza kutofanikiwa.” Taarifa kwamba Diamond hataoa zilisambaa na kudaiwa kumchefua mchumba wake Wema Sepetu ambapo katika mahojiano mkali huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’ alisema: “Kwanza sikuwahi kusema siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti hilo, nilisikitika kwa kweli na iliniuma sana, lakini nikaona nikijibu nitaonekana kwamba sina adabu, kwa sababu siku zote anayeanza huwa haonekani lakini anayemaliza. Pia siwezi kubishana na vyombo vya habari, mwisho wa siku ni watu haohao nitawategemea wanifanyie kazi zangu,” alisema. Hata hivyo Diamond alisema mchumba wake anaumizwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa mwiba kwake. “Hata hivyo magazeti yetu tumeshayazoea jinsi yanavyoandika, wakati mwingine inakuwa kama chachandu au kufurahisha baraza,” aliongeza. Kuhusu taarifa kwamba ameachana na mchumba wake huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu wengi wanasema tumeachana, lakini hatujaachana na hatuwezi kujibishana. “Sijui nikujibu nini kwa sababu kila nitakachokujibu utaona namsifia kwa sababu yule ni mchumba wangu.

HUYU NDIO KIONGOZI WA FREEMASON AFRIKA MASHARIKI, NI MTANZANIA. AFUNGUKA MENGI...HADI SWALA LA KANUMBA. INGIA HAPA

Ukisoma aliyofunguka utaogopa. Azungumzia hadi Msanii kanaumba aliyvyoingia.

Story nzima  >>>>>>ingia apa <<<<<<<<<<<<<<<<<