Saturday, August 23, 2014
|
KUPITIA Gazeti la Mwanaspoti
ambalo kwa mujibu wa takwimu za
mauzo nchini ni wazi kwamba
halina mpinzani, msanii wa muziki
wa kizazi kipya Diamond Platinumz
ametangaza ndoa na mchumba
wake wa muda mrefu Wema
Sepetu anayosema itafungwa hivi
karibuni.
Msanii huyo ghali zaidi nchini kwa
sasa, ametamka hayo
alipozungumza na Mwanaspoti
nyumbani kwake Sinza jijini Dar es
Salaam juzi Jumatano. Alisema
kuna mambo mengi
yaliyomchelewesha kufikia hatua
hiyo, ikiwamo maandalizi kwani
amepanga mashabiki wake
wahudhurie harusi hiyo.
“Ndoa ni kitu cha heri na baraka,
lakini kitu kinachofanya kidogo
mambo yachelewe ni kwamba sisi
au mimi ni mtu ninayefahamika,
kwa hiyo hata ndoa yangu watu
wengi wanatamani waihudhurie,”
alisema Diamond.
Pia amesisitiza kwamba ndoa si
jambo la masihara kwani ni tendo
la kiimani na ndio maana
amekuwa makini katika mipango
yake.
“Nataka kila kitu kishuhudiwe na
mashabiki, ninaweza hata
kuifanyia Uwanja wa Taifa,”
aliongeza.
“Unajua nilishindwa kufanya
mambo haya haraka kwa sababu
wengi nadhani wangeamini
kwamba ninafanya hivyo ili
kutafuta umaarufu zaidi, tunataka
tufanye kiusahihi yasije tokea
mambo kama ya Instagram
tunataka tuje kuwa mfano wa
kuigwa.”
Alipoulizwa tarehe ya ndoa hiyo
Diamond alisema: “Nilishasema ni
hivi karibuni, unajua siku zote vitu
vya kheri waswahili wanasema
lazima uvifiche, hata Mwenyezi
Mungu naye anasema anampenda
mtu aliye na siri, lazima vitu
vingine uvifiche ili vipate
kufanikiwa. Wakati mwingine
kunakuwa na husda, hasidi kwa
hiyo ukiviweka wazi sana vinaweza
kutofanikiwa.”
Taarifa kwamba Diamond hataoa
zilisambaa na kudaiwa kumchefua
mchumba wake Wema Sepetu
ambapo katika mahojiano mkali
huyo wa wimbo ‘Mdogo Mdogo’
alisema: “Kwanza sikuwahi kusema
siwezi kuoa, nilishtushwa na gazeti
hilo, nilisikitika kwa kweli na
iliniuma sana, lakini nikaona
nikijibu nitaonekana kwamba sina
adabu, kwa sababu siku zote
anayeanza huwa haonekani lakini
anayemaliza. Pia siwezi kubishana
na vyombo vya habari, mwisho wa
siku ni watu haohao
nitawategemea wanifanyie kazi
zangu,” alisema.
Hata hivyo Diamond alisema
mchumba wake anaumizwa na
vichwa vya habari ambavyo
vimekuwa mwiba kwake.
“Hata hivyo magazeti yetu
tumeshayazoea jinsi
yanavyoandika, wakati mwingine
inakuwa kama chachandu au
kufurahisha baraza,” aliongeza.
Kuhusu taarifa kwamba
ameachana na mchumba wake
huyo, alisema: “Hatuna tatizo watu
wengi wanasema tumeachana,
lakini hatujaachana na hatuwezi
kujibishana.
“Sijui nikujibu nini kwa sababu kila
nitakachokujibu utaona namsifia
kwa sababu yule ni mchumba
wangu. |
0 comments:
Post a Comment