Saturday, August 23, 2014
 |
Mamlaka ya Mawasiliano
Tanzania (TCRA), imetoa onyo
pamoja na kutoza faini ya
takribani Sh milioni 5 kwa
kituo cha redio na televisheni
cha Clouds, kwa kukiuka
kanuni za utangazaji za mwaka
2005.
Wakielezea uamuzi huo jana
jijini Dar es Salaam, Kamati ya
Maudhui ya mamlaka hiyo
ikiongozwa na Mwenyekiti
wake, Margaret Munyagi
ilisema kuwa ukiukwaji wa
kanuni hizo ulifanywa kwa
nyakati tofauti na vituo hivyo.
Alisema kwa upande wa kituo
cha redio cha Clouds, kupitia
kipindi chake cha ‘Njia Panda’
kilichorushwa hewani Juni 15
mwaka huu kati ya saa 8.00
mchana na saa 10.00 jioni
kilikuwa na mada iliyohusu
safari ya kuzimu ambapo
maudhui yake yalijaa simulizi
za kufikirika, za kishirikina na
kichawi.
Aidha alisema kosa lingine
kituo hicho hakikufuata kanuni
za Utangazaji(maudhui) za
mwaka 2005 zinazowataka
kuwasilisha ratiba ya vipindi
vyao kwa TCRA ili viidhinishwe
na vilevile kuvichapisha katika
gazeti kabla ya kurushwa
hewani ambapo kipindi cha
Njia Panda hakikuwasilishwa
kwa ajili ya kuidhinishwa.
Wakati huo huo, kituo cha
televisheni cha Clouds
kilirusha kipindi cha ‘Bibi
Bomba’ Mei 16 na Juni 6
mwaka huu kati ya saa 3.00
na saa 4.00 usiku ambacho
kilikiuka kanuni za Utangazaji
(maudhui) za mwaka 2005.
Alisema kipindi hicho
kilidhalilisha mabibi hao
walioshiriki pamoja na
wanawake kwa ujumla
kutokana na maswali ya aibu
waliyokuwa wakiulizwa na
waamuzi wa shindano hilo
ambayo ni kinyume na kanuni
hizo.
Aidha alisema kituo hicho
kinatozwa faini ya Sh milioni
moja na kutakiwa kuwasilisha
TCRA mwongozo wa kuchuja
na kusimamia maudhui
yasiyofaa kabla ya
kutangazwa.
TCRA imesema kama Kanuni
za Utangazaji zitaendelea
kukiukwa hatua kali zaidi za
kisheria zitachukuliwa dhidi
yao. |
0 comments:
Post a Comment