Saturday, August 23, 2014
 |
Aliachwa: Angel
Di Maria
hakupangwa
katika kikosi
cha Real Madrid
kilichokabiliana
na Atletico
Madrid jana
usiku.
CARLO
Ancelotti
amethibitisha
kuwa mchezaji
anayewaniwa
kwa nguvu zote
na Manchester
United, Angel Di
Maria aliachwa
katika kikosi
cha jana
kwenye mchezo
wa marudiano
wa Spanish
Super Cup dhidi
ya mahasimu
wake, Atletico
Madrid na
kupoteza kombe
la kwanza
msimu huu kwa
sababu za
kimpira na si
vinginevyo.
“Aliachwa
katika kikosi
kwa sababu za
kimpira”
Alisema
Ancelotti
alipoulizwa
kwanini
hajampanga
Muargentina
huyo hata
katika orodha
ya wachezaji wa
akiba jana
uwanja wa
Vicente
Calderon.
Kitendo cha Di
Maria
kutopangwa
jana kinaashiria
uhusiano na
kocha Ancelotti
umefikia hali
mbaya na ni
sababu tosha
kwa
Manchester
United kumnasa
kwa ada
inayoaminika
kuwa paundi
milioni 50.
Ancelotti
alithibitisha
kuwa nyota
huyo wa
Argentina
katika fainali za
kombe la Dunia
majira ya
kiangazi mwaka
huu ameomba
kuondoka Real
Madrid.
Mashabiki wa
Real Madrid
wameiacha
klabu katika
wasiwasi
kwasababu
wanamhitaji Di
Maria kubakia,
lakini
Rais Florentino
Perez anataka
auzwe ili
kuweka sawa
mahesabu
baada ya
kutumia kiasi
kikubwa cha
fedha
kumsajili Toni
Kroos na James
Rodrgiguez.
Madrid walibaki
katika utata
mkubwa
kutokana na
mashabiki
waliohudhuria
Santiago
Bernabeu siku
ya jumanne
kulipuka kwa
shangwe
wakimshangilia
Di Maria baada
ya kuingia
uwanjani
kipindi cha pili
akitokea
benchi.
Ancelotti
alithibitisha
ijumaa kuwa
mchezaji
amekataa
kusaini
mkataba mpya
na ameomba
kuondoka.Na mdadisiblog/festosaimon |
0 comments:
Post a Comment