Saturday, August 23, 2014
 |
HII ni siri usimwambie mtu
yeyote, uchune nayo hivyo hivyo
kwa vile bado Marcio Maximo
hajaweka wazi kikosi chake cha
kwanza lakini tathmini ya
Mwanaspoti imekibaini.
Kwa mujibu wa mazoezi
yaliyofanyika Dar es Salaam na
hapa Pemba jumlisha na mechi ya
kirafiki waliyocheza, ‘First Eleven’
ya Yanga itakuwa kama ifuatavyo;
Kipa ni Deo Munishi ‘Dida’ kama
kawaida na Juma Abdul atacheza
beki ya kulia. Kushoto ni Oscar
Joshua lakini Edward Manyama na
Amos Abeil anaocheza nao nafasi
moja ni hatari sana, Maximo
anaweza akawatumia kwa
kuchanganya kulingana na timu
pinzani.
Beki ya kati ni Kelvin Yondani
‘Vidic’ na Nadir Haroub
‘Cannavaro’, kiungo mkabaji ni
Mnyarwanda Mbuyu Twite na
kiungo mshambuliaji ni Hassan
Dilunga.
Panga pangua Mbrazili Andrey
Coutinho atacheza winga ya
kushoto na Mnyarwanda Haruna
Niyonzima atacheza winga ya
kushoto, mastraika wa kati ni
Mrisho Ngassa anayecheza kama
kiungo nyuma ya Genilson Santos
Santana ‘Jaja’.
Kwenye nafasi za mbele, kiungo,
winga na straika mambo yanaweza
kubadilika kulingana na aina ya
timu pinzani watakayocheza nayo.
Kwani wachezaji kama Simon
Msuva anaweza kutumika kucheza
winga ya kulia kama anataka timu
icheze kwa kasi zaidi, Jerry Tegete,
Hamis Kiiza raia wa Uganda, Said
Bahanuzi na Hussein Javu nao
wanaweza kumpeleka Ngassa
pembeni, kama atataka kucheza
mpira wa kutulia.
Maximo amesisitiza kuwa katika
mechi hizi za majaribio, anataka
kuwatumia wachezaji wote ili
awaone na ndivyo anavyowapa
nafasi.
Ametengeneza ‘First Eleven’ mbili
ambazo huchuana zenyewe kwa
wenyewe na hao ndiyo watatoa
kikosi halisi cha kwanza ambacho
mwenyewe hajakiweka wazi.
“Kwa sasa nampa kila mchezaji
nafasi ya kucheza, lengo ni
kuwaona namna wanavyocheza na
muunganiko wa kombinesheni ipi
inakubali kupata kitu fulani
kulingana na mechi,” alisema
Maximo.
Maximo alitumia muda wa
takribani robo saa akizungumza na
wachezaji na baadaye walifanya
mazoezi ya kukimbia na baadaye
mafupi ya kucheza mpira.
Katika mazoezi hayo, kiungo
Hassan Dilunga, alishindwa
kufanya mazoezi na wenzake kwani
alikuwa anasikia maumivu kwenye
kidole cha mwisho cha mguu wa
kulia kwani alijitonesha kwenye
mechi ya juzi Alhamisi na
Chipukizi. Credit mwanaspoti |
Kusoma habari nyingine BONYEZA HAPA
0 comments:
Post a Comment