Saturday, August 23, 2014

ANGALIA TANZANIA ELEVEN WANAVYOPIGA BATA NDANI YA SAPPHIRE COURT KABLA YA KUIVAA MADRID LEO

NSAJIGWA, NYENGE NA MASATU.
KIKOSI CHA TANZANIA ELEVEN WAKIJIACHIA KWA MISOSI YA NGUVU KWA MGAHAWA WA HOTELI YA SAPPHIRE COURT YA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAKO WAMEWEKA KAMBI KUJIWINDA DHIDI YA WAKONGWE WA REAL MADRID AMBAO WATAWAVAA LEO KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR KATIKA MECHI YA KIRAFIKI INAYOSUBIRIWA KWA HAMU KUBWA NA MASHABIKI
LUNYAMILA NA ATHUMANI CHINA.
IDDI MOSHI MNYAMWEZI NA MAXIME.
CHINA

Credit salley ally

Haya ndo matokeo ya mechi kati ya ATLETICO MADRID VS REALMADRID, super cup

Wakati wakongwe wao wakitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki leo jijini Dar es Salaam, Real Madrid imeshindwa kuonyesha kuwa wanaweza baada ya kuchapwa bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid. Kipigo hicho cha bao 1-0 katika mechi ya pili ya Super Cup, maana yake Atletico wameibuka mabingwa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ndani ya Camp Nou. Muuaji wa jana alikuwa na Mario Mandzukic ambaye amejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich ambaye alifunga bao hilo katika dakika ya 2 tu. Pamoja na juhudi za Kocha Carlo Ancelotti kumuingiza Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili, bado Madrid haikuweza kupindua matokeo. Kiungo Luca Modric alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

MSAFARA WA MWISHO WA REAL MADRID ULIVYOTUA DAR, LEO TAIFA PATAPENDEZA

Magwiji wa Real wakisubiri usafiri kuelekea Bahari Beach
Watu walijitokeza kuwapokea
Wanaelekea kwenye basi la Azam FC kwa safari ya hotelini
Msafara wa mwisho wa Real Madrid baada ya kuwasili Dar es Salaam jana jioni tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya magwiji wa Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Friday, August 22, 2014

KARIBU TANGA: MAHABA NAMNA HII KWANINI MTU UCHEPUKE?!!!!....HAPO NDIO MAANDALIZI YA FOOD...

BALOTELLI ATUA LIVERPOOL KUKAMILISHA USAJILI WAKE

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alitarajiwa kuwasili England leo mchana kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kujiunga na Liverpool baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na wawakilishi wake. Mpachika mabao huyo wa zamani wa Manchester City yuko karibu kusaini kikosi cha Brendan Rodgers na amekwenda huko kukamilisha dili hilo mara moja. Baada ya kuwasili, Balotelli alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali ya klabu hiyo, Spire Liverpool kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo zaidi vya afya katika viwanja vya Melwood vinavyotumika kwa mazoezi na klabu hiyo. Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo wa Italia hataweza kuichezea Liverpool dhidi ya klabu yake ya zamani, Manchester City Jumatatu usiku, katokana na muda wa usajili kwa leo kupita.NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

FAHAMU KIWANGO KIPYA ANACHOLIPWA DIAMOND KWA SHOW MOJA YA MZIKI HAPA TANZANIA

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako. Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo. Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Tanzania). “Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.” Babu Tale aliiambia Bongo5. Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani). “Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya. Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500). Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na tano za kitanzania. Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava. Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue waongee.

Kutana na vichekesho vya Peter Msechu na Baba Levo baada ya kukosa show.

Peter Msechu na Baba Levo ni wasanii kutoka mkoa wa Kigoma na wote wawili wana sifa ya kuwa wachekeshaji sana. Wasanii wengi wanajua kwamba ukipanda tour bus na wawili hawa basi ni kama unaangalia show ya comedy njia nzima ya safari. Peter Msechu amekuwa ana post vichekesho mbalimbali, kutana na hivi viwili kuhusiana na kazi yao baada ya kukosa show.

FIGO: NJOONI MUONE VITU VYANGU KESHO TAIFA, KAREMBEU ASEMA ATAMPA MAPANDE YA KUMWAGA AWABURUZE WATANZANIA

Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Luis Figo ameahidi burudani nzuri ya soka kesho Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam wakati magwiji wa Real Madrid ya Hispania watakapomenyana na magwiji wa Tanzania katika mchezo wa kirafiki. Akizungumza na Waandishi wa Habari mchana huu katika hoteli ya Southern Sun, Dar es Salaam, mshindi huyo wa Ballon d’Or mwaka 2000, aliyestaafu Mei 31 mwaka 2009, amesema kwamba Watanzania watafurahia kazi yake uwanjani kesho. Figo aliyepiga tuzo mbili mfululizo mwaka 2000, Mwanasoka Bora Ulaya na Dunia, amewaomba wapenzi wa soka Tanzania kujitokeza kwa wingi kesho kushuhudia burudani. “Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania, nimekwishatembea nchi kadhaa Afrika, nimefurahi kuja hapa, naipenda Afrika. Natarajia mchezo mzuri kesho, hata kwa wapinzani wetu pia, kitu muhimu ni kwamba FIFA imefurahia tukio hili,”alisema Figo. Kwa upande wake, mwanasoka bora wa Oceania mara mbili 1995 na 1998, Christian Karembeu aliyeshinda Kombe la Dunia na Ufaransa mwaka 1998, amesema kwamba atampa pasi nyingi kesho Figo afanye vitu vyake. Beki wa zamani wa kimataifa wa Hispania, Fernando Sanz Duran ni miongoni mwa wanasoka watatu waliowika Real Madrid muongo uliopita waliofika jana usiku, ambaye pia alikuwepo kwenye mkutano wa leo. “Nimefurahi kuja Tanzania, ni mara yangu ya kwanza, Watanzania watarajie burudani nzuri kutoka kwetu na wapinzani wetu,”alisema Sanz huku akimgusa begani, kocha Msaidizi wa Magwiji wa Tanzania, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’. Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England, Michael Owen aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi Kombe la Dunia mwaka 1998 Ufaransa, anatarajiwa kuwasili katika kundi la mwisho la Magalactico hao jioni ya leo. Mkurugenzi wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), Farough Baghozah ambao ndiyo wanawaleta magwiji hao nchini, amesema maandalizi yote yamekamilka na Watanzania wajitokeze kwa wingi Taifa kesho. Magalactito wa Real wamefikia katika hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach wakati timu ya Tanzania imeweka kambi Kariakoo, Dar es Salaam kikiendelea na mazoezi Uwanja wa Taifa. Kikosi hicho kinaundwa na makipa maarufu waliowahi kuwika nchini, Mwameja Mohamed na Manyika Peter, mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo, Viungo Athumani China, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo. Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda. Benchi ka Ufundi, ni Kocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa. Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro.

Aunt Ezekiel ajibu kauli ya Diamond kuhusu marafiki wa Wema ‘wapenda anasa’

Muigizaji wa filamu nchini, Aunt Ezekiel ambaye ni rafiki wa karibu wa mpenzi wa Diamond Platnumz, Wema Sepetu amezungumzia kauli ya Diamond aliyotoa hivi karibuni kuwa mpenzi wake ana marafiki wapenda starehe na anasa. Aunt ameiambia Bongo5 kuwa Wema ni mtu mzima anajua baya na jema. “Diamond alivyoongea pale hakunitaja jina, kwahiyo nikisema kwamba aliongea kwa sababu yangu nitakuwa muongo. Yeye aliongea kwa niaba ya watu ambao wako na Wema, hata kama angekuwa amenitaja jina sidhani kama angeongea kwamba yule mtu anafundishwa,” amesema Aunt. “Wema ni mtu mzima anaishi mwenyewe na ana maisha yake sidhani kama ni mtu wa kufundishwa. Wema ni mtu ambaye ana maamuzi yake, watu hawajui kuna wakati wa kazi na kuna wakati wa kuspend maisha. Kwahiyo mimi na muda wangu wa kazi na nina muda wangu waku spend.” “Sihitaji kuangalia kuna mtu anafuatilia maisha yangu kwamba eti nakuwaga na Wema. Hawanisaidii chochote. Nachotakiwa kuangalia nafanya kazi zangu na maisha yangu yanaenda mbele na sitaangalia watu wanasema nini. Mimi nina kazi zangu. Sijui kama Wema kama anahitajika kubadilika kwa sababu Diamond ndiyo anajua mapungufu ya Wema na Wema anajua ya Diamond.” Kwa upande mwingine muigizaji huyo amesema anakuja na filamu yake mpya iitwayo ‘Mwajuma Nipe’. CREDIT BONGO5