Friday, August 22, 2014

LUIS FIGO ATUA DARA TAYARI KUWASHUGHULISHA AKINA PAWASA JUMAMOSI TAIFA

Karembeu akiwa na Mkurugenzi wa kampuni ya TSN, Farough Baghozah kushoto, ambaye kampuni yake ndiyo inawaleta magwiji wa Real nchini
Nyota mwingine wa zamani wa Real Madrid, Christian Karembeu akiwa na Tuliy baada ya kuwasili nchini
Magwiji wa Tanzania wanaendelea na mazoezi Dar es Salaam kwa ajili ya mchezo huo, kulia ni Stephen Nyenge, kushoto Boniface Pawasa
Mwanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Luis Figo kushoto akiwa Said Tuliy kulia baada ya kuwasili mjini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kukichezea kikosi cha magwiji wa Real Madrid dhidi ya magwiji wa Tanzania Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Tuliy ni mmona wa Waratibu wea ziara ya magwiji hao nchini.

MOURINHO NAYE AMWAGIWA MAJI YA BARAFU, APIGA KELELE KAMA MTOTO

KOCHA WA CHELSEA, JOSE MOURINHO NAYE AMEINGIA KWENYE KALE KAMTINDO KAMA MAJI YA BARIDI BAADA YA KUMWAGIWA NA KUMWAGIWA NA KUPIGA KELELE UTAFIRIKI KAMA MTOTO. DIDIER DROGBA NDIYE ALIYEMCHAGUA KOCHA WAKE HUYO. KAMTINDO HAKO KAMEKUWA KAKIENDELEA KWA KASI KWA WACHEZAJI NA MAKOCHA KIBAO KUMWAGIWA MAJI BARIDI MAARUFU KAMA SOACKING

Thursday, August 21, 2014

JAMANI JAMANI..HIVI HAWA WANAFUNZI WALIKUA WANAONGEA NINI HADI KUFANYA HIVI?!!!

KAMA UNGEKUWA MWALIMU WA NIDHAMU UNGEWPA ADHABU GANI WANAFUNZI HAWA?

HIVI NDO VITUO VITAKAVYO UZA TIKETI ZA MECHI KATI YA WAKONGWE WA REALMADRID VS TANZANIA ELEVEN

Waratibu wa ziara ya kikosi cha Real Madrid, Kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), wametangaza sehemu ambazo tiketi za mechi inayosubiriwa kwa hamu ya wakongwe wa Tanzania Al maarufu kama Tanzania Eleven dhidi ya Real Madrid wakongwe zinapouzwa.
Wamesema vituo vinaweza kuongezeka kutokana na mahtaji ya juu ya watu lakini vituo zaidi ya 10 tayari zimeanza kuuza tiketi hizo.

TICKET   ZA REAL MADRID  ZINAPATIKANA  KATKA  VITUO VIFUATAVYO.
TSN   BAMAGA SUPERMARKET .
TSN  OIL  BAMAGA PETROL STATION.
TSN   SUPERMARKET  UPANGA .
TSN  SUPERMARKET  TEGETA.
BIG BON    MSIMBAZI.
BIG BON   SINZA.
BIG BON  TEMEKE.
BIG BON MBAGALA.
BIG BON TEGETA.
TSN SUPERMARKET TANCORT  HOUSE .
MARRY   BROWN MASAKI.
TSN   SUPERMARKET  MIKOCHENI.
TSN  OIL TABATA  KIMANGA.
ENGEN   MIKOCHENI
MARRY  BROWN MLIMANI CITY

KIBOKO YA MAN U YASAJILI BEKI WA ARGENTINA

KLABU ya Swansea City imekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 8 wa Federico Fernandez kutoka Napoli. Beki huyo wa kati alikwenda kufanyiwa vipimo vya afya wiki hii Wales na kusaini Mkataba wa miaka minne, akiweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi wa nafasi za ulinzi kusajiliwa na klabu za Wales. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliichezea Argentina katika Kombe la Dunia, ataziba pengo la beki wa kati Chico Flores aliyeondoka, kwa kucheza na Ashley Williams. Na mdadisiblog/festosaimon

#Exclusive: Tumesoma sana ya Magazeti, sasa tuisikilize sauti ya Okwi mwenyewe kuhusu kuondoka Yanga.

Mganda Emmanuel Okwi harudi tena Yanga na sasa ameweka wazi kwamba anashughulikia mipango yake kwenda kucheza soka la Ulaya >>> Okwi aachana na Yanga mchana kweupe!!!!! >>> Okwi achukizwa na ishu ya DVD ya Maximo <<<< hizo ni baadhi tu ya sentensi kwenye Magazeti mbalimbali ya Tanzania kwa wiki kadhaa ila ukweli kutoka kwa Okwi mwenyewe ni huu hapa chini.

Akiwa Kampala ameongea kwenye Exclusive interview na Bill the African ambae ni ripota wa millardayo.com na AyoTV Kampala Uganda na kusema haya >>> ‘Mimi na Yanga tulikua na makubaliano ya mkataba na hakuna ukweli kwamba Mshahara niliokua nalipwa Yanga ni mdogo, mshahara usingekua unatosha nisingekubali kusaini mkataba ‘ ‘Ni kweli kuna mambo mengi hayapo sawa kati yangu na club yangu ya Yanga ila ni mambo ya ndani ambayo nisingependa kuyazungumzia, ni mambo madogo ambayo nadhani yanaweza kuisha‘ ‘Hakuna ukweli kwamba mimi nakwenda Ulaya, sijui hata imetoka wapi na nani kaanzisha hii ya Ulaya, mimi bado ni mchezaji halali wa Yanga na huwa naongea nao karibu kila siku, hata jana nimetoka kuongea na katibu mkuu na mambo yote yanaelekea vizuri hamna shida yoyote mpaka sasa hivi‘

Kama unahitaji zaidi kupata ushahidi wa sauti yake Okwi akiongelea hi iishu bonyeza play hapa chini.  PLAY HAPA
USIKILIZE 

Credit millardayo

LIVERPOOL SASA YAGEUKIA KWA MARIO BALOTELLI

Liverpool imeanza mipango ya kumnasa Mario Balotelli kutoka AC Milan. Kocha wa Liverpool, Brendan Rogders anataka kumnsa mshambuliaji huyo kwa mkopo kuyoka Milan. Awali kocha huyo alisema hawana mpango wa kumsajili Balotelli. Hata hivyo imeelezwa AC Milan wangependa suala hilo liwe biashara ya ‘cash’ na si mkopo. Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA USOME HABARI ZINGINE 

TIMU YA ARSENAL YAPATA PIGO LINGINE KUBWA

NAHODHA wa Arsenal, Mikel Arteta atakosa mechi mbili zijazo za klabu yake baada ya kuumia kifundo cha mguu katika mchezo wa kwanza wa mchujo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Besiktas. Nyota huyo wa Arsenal alitolewa nje dakika ya 50 kwenye Uwanja wa Olympic Ataturk baada ya kuumizwa na mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba. Arsenal pia itamkosa nyota wake mwingine, Aaron Ramsey katika mchezo wa marudiano na timu hiyo ya Uturuki, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya nano kipindi cha kwanza dhidi ya Beskitas. Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI  

EFM yavunja ngome ya kipindi cha michezo cha Radio One, yawachukua Maulid Kitenge na Omary Katanga

Kipindi cha michezo cha Radio One ‘Spoti Leo’ kimepata pigo kali baada ya watangazaji wake mahiri, Maulid Kitenge na Omary Katanga kuhamia EFM 93.7 ya Dar es Salaam. Maulid Kitenge na Omary Katanga enzi wakiwa Radio One Kuondoka ghafla kwa watangazaji hao waliokifanya kipindi cha ‘Spoti Leo’ kuwa kipindi bora zaidi cha michezo nchini kutokana na umahiri wao katika kuhoji na kutangaza vipindi vya michezo, ni pigo kubwa kuwahi kutokea Radio One katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Kuziba pengo hilo, watangazaji wa michezo wa Capital FM (kituo cha radio ndugu) ndio wanaofanya kipindi cha michezo cha Radio One kwakuwa Isaac Gamba ambaye naye hufanya kipindi hicho yupo likizo. Maulid Kitenge na Omary Katanga wanaanza kutangaza kipindi cha michezo cha EFM cha nusu saa, leo Alhamis kuanza saa 1 jioni. Wasikilize Kitenge na Katanga kwenye promo ya kipindi chao EFM.

           BONYEZA HAPA           KUWASIKILIZA