Thursday, August 21, 2014

EFM yavunja ngome ya kipindi cha michezo cha Radio One, yawachukua Maulid Kitenge na Omary Katanga

Kipindi cha michezo cha Radio One ‘Spoti Leo’ kimepata pigo kali baada ya watangazaji wake mahiri, Maulid Kitenge na Omary Katanga kuhamia EFM 93.7 ya Dar es Salaam. Maulid Kitenge na Omary Katanga enzi wakiwa Radio One Kuondoka ghafla kwa watangazaji hao waliokifanya kipindi cha ‘Spoti Leo’ kuwa kipindi bora zaidi cha michezo nchini kutokana na umahiri wao katika kuhoji na kutangaza vipindi vya michezo, ni pigo kubwa kuwahi kutokea Radio One katika kipindi cha miaka ya hivi karibuni. Kuziba pengo hilo, watangazaji wa michezo wa Capital FM (kituo cha radio ndugu) ndio wanaofanya kipindi cha michezo cha Radio One kwakuwa Isaac Gamba ambaye naye hufanya kipindi hicho yupo likizo. Maulid Kitenge na Omary Katanga wanaanza kutangaza kipindi cha michezo cha EFM cha nusu saa, leo Alhamis kuanza saa 1 jioni. Wasikilize Kitenge na Katanga kwenye promo ya kipindi chao EFM.

           BONYEZA HAPA           KUWASIKILIZA 

0 comments:

Post a Comment