Thursday, August 21, 2014

HII MPYAAA..!! SIKIA HII YA INAYOMUHUSU DULLY SYKES KUIBA MKE WA MZUNGU NA KUTAKA KUMUOA, SIKILIZA NDUGU WALIVYOKUJA JUU..!!

Kama ilivyo ada makamanda wa @gossipcourt walipokua mzigoni walifanikiwa kunasa vinasaba vya sauti vikimzungumzia msanii wa mziki wa kizazi kipya u maarufu kama bongo flava alievunja ndoa ya mwanadada aliolewa na mzungu,huku wengi wakimshangaa bidada huyo kwa kuchezea bahati ati kumfanyia vituko mzungo na kuhamia kwa bongo flava huyo huku wakiponda starehe na raha kwa pesa zinazotoka kwa mzungu huyo....

 BONYEZA HAPA KUSIKILIZA 

SOMA ALICHOKISEMA ALIKIBA KUHUSU UWEZEKANO WA KUFANYA NYIMBO NA DIAMOND

Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu huenda kikatokea hivi karibuni. Collabo ya Alikiba na Diamond Platnumz mabibi na mabwana inanukia. Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha Clouds FM leo (20/8), Alikiba amesema upo uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja kama kukitokea mabadiliko. “Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata mengi tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza hicho kitu kipo. "Lakini muziki vile vile kama unavyoona kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili la ofisini, vazi hili la mpirani, hili la mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua vitu kama hivyo! alisema AliKiba. "Kwahiyo Diamond akipata vazi lake ambalo linahusiana na vazi ambalo natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya kazi kama kawaida, kwa sababu yeye anafanya kazi vizuri,” Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa kufanya show kubwa na Diamond alijibu kwa kicheko: “Wewe hujui kama watu wanasubiria (show) au unajisahaulisha.”

SOMA HAPA KIPYA ALICHOKISEMA DIVA KUHUSU PENZI LAKE KWA CRAZY GK

Ile hatua ya U boifriend na U girlfriend ikiwa imepita na kuingia katika hatua ya uchumba wa mahaba kedekede, dada yetu Diva alijikuta anamwaga chozi baada ya watu mbalimbali kumtupia maneno kwamba amempendea King Crazy Gk umaarufu wake ili abaki kupata KIKI Mjini. Diva alijikuta anatoa maneno makali ya hasira na kuangua kilio na kudai kuwa hajampendea Gk umaarufu wake sababu yeye ni Diva ni maarufu pia hapa Tanzania, hakuishia hapo alizidi kudai ya kuwa amechoshwa na watu wengi kusema ana mahusiano na Gk ambae hana Pesa na ameachana na mwanaume ambae anapesa na cheo kikubwa Tanzania. Diva:Nimechoshwa kuulizwa maswali ya Prezzo au mwanasiasa sababu huko siko tena na sina mahusiano nao zaidi ya urafiki wa kawaida wa kuongea nao kama watanzania wenzangu na pili amedai kuwa hana hisia zozote za kimapenzi na watu hao sababu yeye yuko na Mpenzi wake na anafurahia mapenzi hayo na mume wake ambae ni Mungu wa Muziki Tanzania. Diva Binti mwenye mvuto na umbo la kuvutia na mvuto wa sura ya babyface na macho ya duara alidai kuwa King Crazy Gk ni Mtu mwenye kipato kizuri tu ila sio mtu wa kujionyesha au kuishi maisha ya kujionyesha na ni mtu mtaratibu anaeishi maisha yake alioridhika nayo na anatumia pesa zake kulipia elimu na kufanya mambo yake na biashara zake binafsi tofauti na watu wanavyomfikiria. Diva la Diva alisema kuwa Hakumpendea Gk Pesa au Umaarufu wake amempenda yeye kama yeye na anachukia baadhi ya watu kumuingilia kimawazo maisha yake ya mapenzi ambayo mashabiki wengi wameonekana kuvutiwa nayo kupitia mtandao wa instagram. Na mdadisiblog/festosaimon

KIAFRIKA ZAIDI: KWAHILI HAKUNA MZUNGU ANAYEWEZA…..!!!!!

Picha: Mfahamu ‘baby mama’ wa Professor J, ‘Mama Lisa’

Black Rhyno amewahi kuoa kumzidi kaka yake Professor J lakini hiyo haimaanishi kuwa Mchawi huyo wa Rhymes hana mke mtarajiwa. Kupitia Instagram, Professor J amemweka wazi mwanamke anayeweza kushika wadhifa wa Mrs Joseph Haule. “OF COURSE ni Baba LISA na Mama LISA. …. What more can I SAY?? #MWANALIZOMBE,” ameandika Professor kwenye picha hiyo juu.

CHEKI GAZETI LA MICHEZO LA AS LA HISPANIA LILIVYOANDIKA KUHUSU UJIO WA REAL MADRID

Gazeti maarufu la michezo la AS la nchini Hispania, limetumia ukurasa mzima kuelezea ziara ya kikosi cha wakongwe cha Real Madrid. Gazeti hilo limeelezea namna kikosi hicho kinavyofanya ziara kwa mara ya kwanza barani Afrika. Madrid watacheza mechi ya kirafiki dhidi ya Tanzania Eleven ambao wameanza kujifua chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa. Mechi hiyo itapigwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Madrid wanatarajia kuanza kuwasili kesho. Kati ya wadhamini wa ziara hiyo na mechi ya kirafiki ni TSN ambao pia ni waratibu wa ziara hiyo, Hoteli ya Sapphire, Bin Slum, Gazeti la Championi na kampuni ya ndege ya Fast Jet. Na salehe ally

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 

Picha: Hii ndo hotel ambayo wachezaji waliochaguliwa kukipiga na wakongwe wa Realmadrid Agosti 23 wameweka kambi

Kikosi cha Tanzania Eleven chini ya Kocha Charles Boniface Mkwasa, kitaweka kambi kwenye hoteli maarufu ya kisasa ya Sapphire Court ya jijini Dar es Salaam. Kambi hiyo inatarajia kuanza leo na wachezaji wataingia kambini hapo kujiandaa kwa ajili ya mechi dhidi ya wakongwe wa Real Madrid itakayopigwa jijini Dar es Salaam, Jumamosi. Madrid itaongozwa na Luis Figo aliyewahi kuwa nota wa Barcelona, baadaye Real Madrid na Inter Milan. Mechi hiyo inasubiriwa kwa hamu na tayari tiketi zimeanza kuuzwa katika sehemu mbalimbali.Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI