Thursday, August 21, 2014
 |
Ulichokuwa ukisubiri kwa muda mrefu
huenda kikatokea hivi karibuni. Collabo ya
Alikiba na Diamond Platnumz mabibi na
mabwana inanukia.
Akizungumza na kipindi cha Jahazi cha
Clouds FM leo (20/8), Alikiba amesema
upo uwezekano wa kufanya kazi ya pamoja
kama kukitokea mabadiliko.
“Mawazo ya kolabo yapo, mawazo unapata
mengi tu, hiyo nimeshaisikia vilevile, na
wewe sio mtu wa kwanza kuniuliza hicho
kitu kipo.
"Lakini muziki vile vile kama unavyoona
kuna mavazi na style, vazi hili linatakiwa
liende disko hili ni vazi la beach, vazi hili la
ofisini, vazi hili la mpirani, hili la
mchangani, hili la kwenye ukumbi unajua
vitu kama hivyo!
alisema AliKiba.
"Kwahiyo Diamond akipata vazi lake
ambalo linahusiana na vazi ambalo
natakiwa nivae, hakuna tatizo tunafanya
kazi kama kawaida, kwa sababu yeye
anafanya kazi vizuri,”
Alipoulizwa kama kuna uwezekano wa
kufanya show kubwa na Diamond alijibu
kwa kicheko: “Wewe hujui kama watu
wanasubiria (show) au unajisahaulisha.” |
0 comments:
Post a Comment