Thursday, August 21, 2014
 |
Ile hatua ya U boifriend na U girlfriend
ikiwa imepita na kuingia katika hatua ya
uchumba wa mahaba kedekede, dada yetu
Diva alijikuta anamwaga chozi baada ya
watu mbalimbali kumtupia maneno
kwamba amempendea King Crazy Gk
umaarufu wake ili abaki kupata KIKI Mjini.
Diva alijikuta anatoa maneno makali ya
hasira na kuangua kilio na kudai kuwa
hajampendea Gk umaarufu wake sababu
yeye ni Diva ni maarufu pia hapa Tanzania,
hakuishia hapo alizidi kudai ya kuwa
amechoshwa na watu wengi kusema ana
mahusiano na Gk ambae hana Pesa na
ameachana na mwanaume ambae anapesa
na cheo kikubwa Tanzania.
Diva:Nimechoshwa kuulizwa maswali ya
Prezzo au mwanasiasa sababu huko siko
tena na sina mahusiano nao zaidi ya urafiki
wa kawaida wa kuongea nao kama
watanzania wenzangu na pili amedai kuwa
hana hisia zozote za kimapenzi na watu
hao sababu yeye yuko na Mpenzi wake na
anafurahia mapenzi hayo na mume wake
ambae ni Mungu wa Muziki Tanzania.
Diva Binti mwenye mvuto na umbo la
kuvutia na mvuto wa sura ya babyface na
macho ya duara alidai kuwa King Crazy Gk
ni Mtu mwenye kipato kizuri tu ila sio mtu
wa kujionyesha au kuishi maisha ya
kujionyesha na ni mtu mtaratibu anaeishi
maisha yake alioridhika nayo na anatumia
pesa zake kulipia elimu na kufanya mambo
yake na biashara zake binafsi tofauti na
watu wanavyomfikiria. Diva la Diva alisema
kuwa Hakumpendea Gk Pesa au Umaarufu
wake amempenda yeye kama yeye na
anachukia baadhi ya watu kumuingilia
kimawazo maisha yake ya mapenzi ambayo
mashabiki wengi wameonekana kuvutiwa
nayo kupitia mtandao wa instagram. Na mdadisiblog/festosaimon |
0 comments:
Post a Comment