Friday, August 15, 2014

BEKI MPYA SIMBA APEWA NYUMBA MIKOCHENI

Wakati Coastal Union wakiendelea kumlilia beki Abdi Banda, mchezaji huyo ambaye amesaini mkataba wa kuichezea Simba, amepewa nyumba ya kuishi.

Hatua hiyo imekuja siku chache tangu mshambuliaji wa Simba, Mrundi Pierre Kwizera, kupewa nyumba ya kuishi pia maeneo ya Kunduchi.

Banda amepewa jumba eneo la Mikocheni huku ikikumbukwa kuwa enzi za utawala wa Mwenyekiti Ismail Aden Rage mchezaji aliyeishi sehemu za gharama kubwa alikuwa ni straika Amissi Tambwe ambaye alipangishiwa mitaa ya Sinza.

“Mimi si mwenyeji wa Dar, viongozi wameniambia kuwa tayari wamenitafutia nyumba Mikocheni na ndani ya wiki hii ninaweza kuhamia,” alisema Banda.

Unazikumbuka movie za Bad Boys 1& 2, hii ni taarifa mpya kuhusu movie hizo

Martin Lawrence na Will Smith ndio mastaa wa movie hizi mbili ambazo zina action na comedy ndani yake. Kama wewe ni mpenzi wa hizi movie basi taarifa ikufikie kwamba Bad Boys 3 ipo kwenye maandalizi.

Akiwa kwenye interview ya TV show actor Martin Lawrence aliulizwa kuhusu plan za movie ya Bad Boys 3 ambayo imekuwa kwenye tetesi kwa muda mrefu na Martin alijibu,”Nimeongea na director jana tu na ameniambia wanafanyia kazi script hivi sasa na wanakaribia kuimaliza.

Hivi karibuni mtapata taarifa rasmi ” Martin hakuthibitisha uhusika wa star mwenzake Will Smith kwenye hiyo movie kwasababu ni bado mapema sana

PHIRI APAA NA SKWADI ZIMA LA SIMBA SC ZENJI LEO, WAKIRUDI HUKO SASA…

Na Princess Asia, DAR ES SALAAM BAADA ya kocha Mzambia Patrick Phiri kusaini Mkataba wa mwaka mmoja jana, kikosi cha Simba SC kinakwenda kambini visiwani Zanzibar leo kuweka kambi rasmi ya kujiandaa na msimu.

Rais wa Simba SC, Evans Elieza Aveva ameambia mdadisiblog jana kwamba, kikosi kinaondoka asubuhi ya leo kwenda Zanzibar na kitarejea siku chache kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu.

Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuanza Septemba 20, mwaka huu na ratiba itatoka wiki moja kabla.

Tayari SImba SC imekamilisha usajili wake na wachezaji wote walikuwa wanahudhuria mazoezi mjini Dar es Salaam.

Phiri amerejea Simba SC baada ya miaka minne tangu aondoke mwaka 2010, akirithi mikoba ya Mcroatia Zdravko Logarusic aliyetupiwa virago mwishoni mwa wiki. Haijulikani mshahara wa Phiri utakuwa kiasi gani, lakini mara ya mwisho aliondoka Simba SC akiwa analipwa dola za Kimarekani 5,000 (zaidi ya Sh. Milioni 7.5) kwa mwezi.

Kocha huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, aliyezaliwa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi za wana Simba ‘kutembea vifua wazi’.

Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi. Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.

Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji.
Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana.

Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.

Simba SC Jumapili ilivunja mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais Aveva alisema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.

Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano

Na mdadisiblog/festo saimon
 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 

NAYE AGUERO AJITIA KITANZI KIZITO MAN CITY

Bado yupo sana Etihad: Sergio Aguero amesaini mkataba mpya Manchester City wa miaka mitano

KLABU ya Manchester City imewekeza jumla ya Pauni Milioni 175 kikosini make ndani ya siku nne, kufuatia mshambuliaji Sergio Aguero kuaini Mkataba mpya wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England Alhamisi usiku.

Mshahara mpya wa Aguero wa Pauni 150,000 kwa wiki umethibitishwa baada ya kusainishwa pia mikataba mipya kwa kiungo David Silva na beki Vincent Kompany ambao watadumu Etihad hadi mwaka 2019.

City iliianza wiki kwa kutoa Pauni Milioni 32 kumsajili beki wa FC Porto, Eliaquim Mangala anayeweka rekodi ya beki ghali katika historia ya soka ya Uingereza.
Na mdadisiblog/festo saimon

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG YETU ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYEZA HAPA 

MWANASHERIA NA WAKILI MAARUFU MBEYA APANDISHWA KIZIMBANI.

Picha na Rashid Mkwinda Blog WAKILI wa kujitegemea mkoani Mbeya na mjumbe wa Mkutano mkuu wa CCM Taifa (MNEC) Sambwee Sitambala (42)amepandishwa kizimbani katika mahakama ya Hakimu mkazi Mfawidhi wilaya ya Mbeya akituhumiwa kwa makosa mawili.

Shitambala amepandishwa jana akituhumiwa kwa makosa ya kuingia kwa jinai na kujenga nyumba katika viwanja viwili namba 27 na 28 Block BB lililopo eneo la Gombe Uyole Jijini Mbeya.

Akisoma mashtaka mbele ya Hakimu mkazi mfawidhi, Gilbert Ndeuruo, wakili wa serikali, Ahmed Stambuli, alisema kuwa Shitambala anashitakiwa kwa kosa la kuingia kwa jinai kinyume cha kifungu namba 79 ya mwaka 2014 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.

Alisema kuwa mshitakiwa kwa nyakati tofauti kati ya Juni 18, 2012 na Novemba 28, 2013 aliingia na kujenga katika viwanja namba 27 na 28 ambavyo vinadaiwa kuwa ni mali ya raia wa Tanzania mwenye asili ya kiasia aliyefahamika kwa jina la Jaswinder Palsingh.

Alisema kulingana na mazingira hayo, mshitakiwa amesababisha maudhi kwa mmiliki wa kiwanja hicho Palsingh na hivyo kushitakiwa kwa kosa la jinai. Shitambala ambaye alikuwa akitetewa na Wakili wa kujitegemea Tasco Luambano alikana shitaka hilo ambapo Hakimu Ndeuruo alisema kuwa dhamana ya Mshitakiwa iko wazi ikiwa atatimiza masharti ya kuwa na mdhamini mmoja na ahadi ya fedha kiasi cha sh. milioni 1.

Kwa upande wake wakili wa serikali Stambuli alisema kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika na kwamba iko tayari kuanza kusikilizwa na kuiomba mahakama ipange tarehe ya kuanza kuisikiliza kesi hiyo.

Hakimu Ndeuruo aliahirisha kesi hiyo hadi Septemba 10 ambapo itaanza kusikilizwa rasmi.

Akizungumza nje ya mahakama mara baada ya kuahirishwa kwa kesi hiyo Wakili anayemtetea Shitambala,Luambano alisema kuwa kesi hiyo imefika hapo kutokana na maslahi ya baadhi ya watu na kuwa kisheria kesi za aina hiyo zinapaswa kusomwa katika mahakama ya Ardhi.

Alisema kuwa mteja amejenga katika eneo ambalo wamejenga watu wengine wapatao 400 na kuwa hata hivyo kesi hiyo imemhusu mteja wake pekee hali ambayo inaonesha nia mbaya iliyofanywa na mlalamikaji dhidi ya mteja wake.

Na mdadisiblog/festo saimon

DIAMOND AHANDIKA UJUMBE MZITO UNAOMLENGA MTU FULANI HAPA BONGO

Story ya ni kuhusu ujumbe mrefu aliondika Diamond kupitia ukurasa wake wa instagram. Ujumbe huo unaonekana unaenda kwa msanii fulani japokuwa hakuweka wazi ni msanii gani.

Diamond aliweka post hii na baada ya muda mfupi aliifuta lakini maneno yote yalikuwa yanasomeka hivi.

“Nafkiri ningewaona kweli Mnaakili na Mapenzi ya dhati kwa Msanii wenu… kama mngemshauri apunguze Mashoga wapenda anasa na apunguze Stareh zisizo na Faida, wenda ingemsaidia Pesa kuzitumia kwenye kufanya kazi na kuleta maendeleo badala ya kuwapa viwanda vya pombe…

Mimi kama bwana, wajibu wangu ni kuhakikisha Mpenzi wangu anakula vizuri, anavaa vizuri, analala vizuri, na kumuwezesha mtaji wa kufanyia kazi…. Waswahili wanasema Mchungaji bora anatakiwa kuhakikisha anampeleka Ng’ombe wake Kwenye Maji safi….ila yeye ng’ombe mwenyewe ndio anatakiwa aamue kunywa maji!!!!! Au mnataka nikishampa mtaji niache kufanya na show tena na kuigiza nimuigizie mie ???? Nisiende Studio nikae dukani nimuuzie mie????.. ni juhudi zako kwanza!… leo hii mimi Hata ningepewa Mamilioni ya mamilioni kama nisingekuwa na moyo wa mie mwenyewe kwanza kutaka kujituma na kupenda kufanya kazi yangu nisingefikia hapa nilipo! ….Mxieeeeeeeew!�� Kama nimekuchefua Lamba ndimu Usitapike”.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 


Posted via Blogaway

YANGA SC WAKIJUA HII, WATAMLAANI KWELI KWELI MUSONYE

Katibu wa CECAFA, Nicholas Musonye kushoto ambaye aliiondoa klabu ya Yanga SC kwenye michuano ya Kombe la Kagame kwa kutaka kuleta timu ya vijana, akizungumza na Ofisa wa Sekretarieti ya bodi hiyo, Veronica Lusiichi kulia Uwanja wa Nyamirambo, Kigali, Rwanda jioni ya leo wakati mechi za michuano hiyo zikiendelea. Azam FC ilipewa nafasi ya Yanga SC.
Ofisa mwingine wa Mamelodi, Mandla Mazibuko akifuatilia vipaji Uwanja wa Nyamirambo. Kulia ni Mtangazaji kutoka Tanzania, Ibrahim Masoud 'Maestro'
Ofisa wa Idara ya kusaka vipaji ya klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini, Russel Molefe kulia akizungumza na Mwandishi wa Habari, Somoe Ng'itu kutoka Tanzania. Yanga SC ingebahatisha kuuza nyota wake klabu hiyo kama wangewavutia wasaka vipaji hawa.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 


Posted via Blogaway

Thursday, August 14, 2014

MAHAKAMA YA SOKA YAMPUNGUZIA ADHABU LUIS SUAREZ

Mahakama ya Soka ya Kimataifa CAS, imekubali kupunguza adhabu ya kumfungia miezi minne Luis Suarez wa Barcelona baada ya kumuuma Giorgio Chiellini wa Italia wakati wa Kombe la Dunia.

CAS imetoa nafuu kwa Suarez na sasa Barcelona rasmi itamtambulisha Jumatatu na atapewa ruksa ya kufanya mazoezi na wenzake.

Mambo ambayo yamepunguzwa na yale yanayobaki kuwa adhabu ni kama yafuatayo.

Suarez ruhusa:
- Kufanya mazoezi na Barcelona.
- Kutambulishwa na Barcelona.
- Kucheza mechi za kirafiki, si zile za mashindano.
- Kucheza mechi za kirafiki za Uruguay dhidi ya Japan, Korea na Saudi Arabia katika miezi ya Septemba na Oktoba
- Kuhudhuria mechi uwanjani.
- Kuhudhuria shughuli za matangazo zinazoihusisha Barcelona.

Suarez si ruhusa:

- Kucheza mechi yoyote ya mashindano akiwa na Barca hadi Oktoba 26.
- Kuichezea Uruguay mechi yoyote hadi zifikie mechi nane.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

By mdadisiblog/festosaimon


Posted via Blogaway

TIMU YA YANGA YA ENDELEZA KUIMARISHA SAFU YA ULINZI KWA KUIPIGA BAO SIMBA KATIKA USAJILI

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM YANGA SC imefanikiwa kumpata beki chipukizi wa JKT Ruvu, Edward Charles baada ya kukamilisha taratibu zote za usajili wake kutoka timu hiyo ya Jeshi la Kujenga Taifa na kumsainisha Mkataba wa miaka mitatu.

Yanga SC kwa miezi miwili sasa imekuwa ikisotea saini ya mchezaji huyo kwa kuanzia kufuata taratibu za kuvunja mkataba wake jeshini- hadi leo ilipokamilisha.

Viongozi wa Yanga SC wakiongozwa na Francis Kifukwe leo walikuwa na kikao cha mwisho na uongozi wa JKT juu ya suala la uhamisho wa mchezaji huyo na mambo yamekwenda vizuri.

Beki huyo alikuwa pia anawaniwa na mahasimu Simba SC, ambao jitihada zao ziligonga ukuta mapema, baada ya kuambiwa wapinzani wao Yanga SC, wamepiga hatua kubwa katika kufukuzuia huduma za chipukizi huyo.

Edward sasa atajiunga na Yanga SC mara moja chini ya kocha Mbrazil, Marcio Maximo kuanza maandalizi ya msimu mpya.

Ni Maximo aliyewasukuma viongozi wa Yanga SC kufukuzia haraka saini ya mchezaji huyo baada ya kutovutiwa na uchezaji wa beki wa sasa wa kushoto wa klabu hiyo, Oscar Joshua. Edward Charles ni kati ya chipukizi waliopo timu ya taifa ya wakubwa kwa sasa, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij ambao wanainukia vizuri.

Ni mkabaji mzuri, ana nguvu, kasi- mbinu za anapokuwa na mpira na asipokuwa nao na pia hupanda vizuri kushambulia na kurudi kwa haraka. Anasifika kwa kupiga krosi nzuri pamoja na mpira iliyokufa.

 BONYEZA HAPA ILI UJIUNGE NA BLOG HII HUPATE HABARI KIRAHISI 

BREAKING NEWS: PHIRI ASAINI MKATABA WA MWAKA MMOJA KUINOA SIMBA

Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesaini mkataba wa mwaka mmoja kuifundisha Simba.

Phiri raia wa Zambia amesaini mkataba huo leo kwenyeHoteli ya Regency. Phiri ameiambia mdadisiblog, mkataba huo unampa ruhusa kuitumikia Simba kwa matumaini makubwa. “heshima ya Simba kwangu ni kubwa sana, ingawa nilikuwa nina mipango mingine, lakini nimekubali kurejea.

“Kazi haitakuwa lahisi, lakini vizuri kwamba sasa tumeingia mkataba mpya wa kazi, ninaamini mambo yatakwenda vizuri,” alisema Phiri.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI 

SPURS YASAJILI BEKI LA KULIA LA MAREKANI MIAKA MINNE

KLABU ya Tottenham imekamilisha usajili wa mwanasoka wa kimataifa wa Marekani, DeAndre Yedlin kwa Mkataba wa miaka minne. Beki huyo wa kulia mwenye umri wa miaka 21, atabaki Seattle Sounders kabla ya kujiunga na kikosi cha Mauricio Pochettino msimu wa 2015/2016. Akizungumza na tovuto ya klabu hiyo, Yedlin alisema; "Nimefurahishwa sana kuja Ligi Kuu ya England na kujishindanisha dhidi ya baadhi ya wachezaji bora duniani,".

 BONYEZA HAPA KUJIUNGA NA BLOG HII 

WAKATI PHIRI AMETUA DAR, ANGALIA LOGA ALIVYOIAGA DAR ES SALAAM

Wakati Kocha mpya wa Simba, Patrick Phiri raia wa Zambia ametua nchini, angalia aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Zdravko Logarusic alivyoliaga jiji la Dar. Kupitia mtandao wa Facebook,

Loga ametupia picha mbili huku akiandika “by by Tanzania), akimaanisha bye bye Tanzania. Loga ameiaga Tanzania kwa picha hizo, moja akiwa ndani Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) akiwa amepiga shati lake la pink na mkononi ameshikilia kinywaji aina ya Redbull.

Picha ya pili, Loga anaonekana kiwa amekaa kwenye beki, hapo ni kabla ya kuingia ndani ya uwanja huo.

Kocha huyo ameondoka na dege la Shirika la Ndege la Tukish. Kama safari yake imekwenda vizuri, tayari Loga atakuwa amewasili kwao salama.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UBONYE HAPA KUJIUNGA NASI 

Mdadisi blog/festo saimon

Vincent kompany ajitia kitanzi kizito Man city

NAHODHA wa Manchester City, Vincent Kompany amesaini Mkataba mpya wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ligi Kuu ya England.

Habari za Kompany kupewa Mkataba mpya ambao inaaminika utmfanya sasa awe analipwa Pauni 130,000 kwa wiki, zinakuja saa 24 baada ya kiungo David Silva pia kusaini Mkataba mpya utakaomuweka katika klabu hiyo mwaka 2019.

Beki huyo kivutio wa Ubelgiji, ameiongoza Man City kutwa ubingwa wa Ligi Kuu ya England mara mbili katika miaka mitatu iliyopita, pamoja na mataji ya FA na Capital One Cup. Na Kompany, mwenye umri wa miaka 28, anataka kushinda mataji mengine matatu kabla ya kuondoka Etihad.

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 

Mdadisiblog/festo saimon

BORUSSIA DORTMUND WAIFUMUA BAYERN MUNICH 2-0 NA KUTWAA SUPER CUP YA UJERUMANI

Wababe; Wachezaji wa Borussia Dortmund wakiwa na taji lao la Super Cup ya Ujerumani, baada ya kuifunga Bayern Munich mabao 2-0 jioni ya leo, wafungaji Hendrikh Mkhitaryan na Pierre- Emerick Aubameyang.

 UNAPENDA HABARI ZA KIMICHEZO ZIKUFIKIE KIRAHISI ZAID BONYA HAPA KUJIUNGA NASI 

Hii ni ishara kwamba Vidal anaweza kutua Manchester united

KIUNGO Arturo Vidal anayetakiwa na Manchester United ameonyesha ishara fulani, baada ya kusaini jezi ya shabiki wa Mashetani hao Wekundu akiwa kwenye ziara na klabu yake, Juventus nchini Australia.

Vidal, ambaye amekuwa akihusishwa na kuhamia Old Trafford kwa muda sasa baada ya nyota huyo wa Chilea kung'ara msimu uliopita, amekuwa akishawishiwa na wachezaji wenzake kubaki Italia.

Kiungo mwingine wa Juventus, Paul Pogba alisema wiki iliyopita kwamba anatumaini Vidal atabakia katika klabu hiyo, licha ya kutakiwa na United, lakini hali inaonekana kuwa tofauti baada ya kusaini jezi ya United.

 WEWE NI MWANAMICHEZO NA UNAPENDA UPATE HABARI ZA KIMICHEZO PUNDE ZINAPOTUFIKIA BONYA HAPA 

Mdadidiblog/festo saimon

JB FILAMU ZAKO NI NZURI ILA HIKI KITU KINAKERA KATIKA FILAMU ZAKO. JIREKEBISHE

Mimi sio mpenzi sana wa kuangalia filamu, ila mara chache tu huwa naangalia hasa kwenye mabasi ninaposafiri.

Kitu kinachonikera kwenye hizi Bongo movie hasa za JB ni kutumia wahusika wale wale na theme ile ile mwisho ana bore sasa.

Mfano ni huyu Shamsa Ford, huwezi kuangalia picha ya JB usimkute, tena kwenye filamu hiyo lazima ataishia kuolewa na JB. Ni kweli Shamsa ni mzuri, lakini kwani yuko pee yake kwenye filamu? Halafu kwa nini theme iwe mapenzi tu? Nachoka kabisa

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI 

Hutaamini ukiisikia sababu iliyomfanya Dogo Janja aache shule!

Rapper kutoka Arusha, Dogo Janja ameamua kuacha shule ili kusomea masomo ya muziki.

Akiongea na 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM, Janjaro amedai kuwa usumbufualiokuwa akiupata shuleni ndio sababu kubwa iliyomfanya aache shule.

“Shule ambayo mimi nimesoma nilikuwa napata matatizo kwasababu kitu kidogo ambacho mnaweza mkafanya wote lakini wewe ukaonekana chanzo. ‘Msanii mhuni, huyu hivi,” alisema rapper huyo. “Sometimes unaweza ukawa unasoma watu wengi wako dirishani wanapita wanakuangalia. Au unaweza ukakosea.. yaani wanakuwa wewe ni mtu ambaye upo sahihi all the time.

Kwa mfano labda unajua zile za kushtukizwa ‘fulani jibu swali’ kila saa unaulizwa wewe,” aliongeza. “Kwahiyo unakuwa hakuna pale Uabdul, unakuwa unaweka Ujanjaro Udogojanja.

Kwasababu unajua ile kushtukizwa kila saa unakuwa unahisi kama mwalimu anakuandama sana. Au kwenye mtihani, mnaweza mkawa mnafanya wote mtihani lakini mwalimu anakuja kukusimamia wewe, anakukazia kinoma.” Nini mtazamo wako kuhusiana na sababu hiyo ya Dogo Janja iliyomfanya aache shule?

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA SUPPORT YAKO KWA KUBONYEZA HAPA 

ANGALIA BALE ALIVYOTOA PASI MARIDADI KWA RONALDO ALIYEFUNGA BAO DHIDI YA SEVILA

BONGE LA PASI ALILOTOA BALE KWA RONALDO.

JEURI YA FEDHA SIMBA SC, PHIRI AFIKISHIWA HOTELI LA BEI MBAYA DAR, ATAIGHARIMU KLABU SH 400,000 KWA USIKU MMOJA TU

Hoteli la bei chafu; Kocha Patrick Phiri kulia akisaini kitabu cha kuingi chumba katika hoteli ya Regency. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Collins Frisch

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM KOCHA Patrick Phiri amefikishiwa kwenye hoteli ambayo gharama ya chumba chake ni dola za Kimarekani 120 (karibu Sh. 200,000 za Tanzania) kwa siku- na wakala wake pia, amechukuliwa chumba cha hivyo.

Maana yake, malazi ya Phiri katika hoteli ya Regency, Dar es Salaam pamoja na wakala wake yataigharimu Simba SC wastani wa Sh. 400,000 kwa siku. Phiri anaweza kusaini Mkataba kesho na baada ya hapo wakala wake atarejea Zambia, naye kuendelea kuishi katika hoteli hiyo- na atapewa usafiri pia.

Haijulikani mshahara wa Phiri utakuwa kiasi gani, lakini mara ya mwisho aliondoka Simba SC akiwa analipwa dola za Kimarekani 5,000 (zaidi ya Sh. Milioni 7.5) kwa mwezi. Phiri amepokewa mchana wa leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kuwekwa kwenye gari la wazi juu akipitishwa mitaa ya Jiji la Dar es Salaam ili manazi wa timu hiyo wamuone, kabla ya kufikishwa Regency Hotel.

Kocha huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, kesho anatarajiwa kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake hiyo ya zamani, Simba SC, akirithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki.

Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi za wana Simba ‘kutembea vifua wazi’.

Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.

Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.

Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji. Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana. Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.

Simba SC Jumapili ilivunja mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.

Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane. Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE TUWEKAPO MTANDAONI