Wednesday, August 13, 2014
KIPENZI CHA WANA SIMBA SC, PATRICK PHIRI ALIPOWASILI DAR LEO KUREJESHA ENZI ZA UFALME MSIMBAZI
Kibonde, Gardner wapandishwa kizimbani kwa kosa la kusababisha ajali na kutoa lugha za matuzi
![]() |
| Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na mwenzake Gardner G Habash (wa pili kulia) wakielekea kizimbani. |
Mtangazaji wa kipindi cha jioni cha Clouds FM, Jahazi, Ephraim Kibonde na mtangazaji wa
kipindi cha jioni cha Times FM ‘Maskani’, Gardner Habash, leo wamepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau
amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.
Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura. Kibonde na Gadner wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena
Source:Global Publisher
BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI
DANTE, BOATENGE MABISHOO KINOMA, ONA WALICHOFANYA WAKATI WA KUPIGA PICHA
Mabeki wa Beyern Munich, Dante na Boateng wameonyesha wenyewe ni bonge ya mabisho. Wakati wakipiga picha ya pamoja ya kikosi, mabeki hao walizivuta jezi kwa nyuma, eti kisa zibane miili yao na SIX PAC zitokeee! Utaona picha inavyoonyesha namna mabeki hao walivyo mabishoo na wanavyotaka kuteka watoto, hahaha!
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA JIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA
TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni.
TFF imesema uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao wanautambua, na wataendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.
“Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji.
TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu,”. “Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake,”.
“Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi,”imesema taarifa ya TFF.
Na mdadidiblog/festo saimon
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI
Martino ni kocha mpya Argentina
Argentina imemteua aliyekuwa kocha wa Barcelona Gerardo Martino kuiongoza timu ya taifa baada ya kung'atuka kwa kocha wa zamani Alejandro Sabella.
Martino, 51, alifurushwa kutoka Barca mwisho wa msimu uliyopita baada ya kushindwa kushinda taji lolote kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2007.
Aliwahi kuwa meneja wa Paraguay kati ya mwaka wa 2006 na 2011 alipowaongoza kufuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia la 2010 .
kocha wa zamani Sabella aliondoka baada ya kushindwa kwa bao moja kwa nunge na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil.
Martino alimrithi kocha wa zamani wa Braca Tito Vilanova mwezi Julai 2013,Camp Nou baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka 2 .
Katika kipindi hicho Barca ilisajili ushindi katika mechi 40 kati ya 59 alizokuwa kocha lakini wakashindwa kusajili ushindi wowote wa tuzo la bara ulaya. Argentina imemteua aliyekuwa kocha wa Barcelona Gerardo Martino kurithi nafasi yake Alejandro Sabella Barcelona ilishindwa na Atletico Madrid katika hatua ya robo fainali ya kombe la mabingwa barani Afrika.
The Catalans walishindwa tena na vibonde wao Real Madrid katika fainali ya kuwania kombe la Copa del Rey. Punde baada ya kuondoka kwake Camp Nou Barcelona,ilimteua Luis Enriqueas kurithi nafasi yake. Atajulishwa rasmi hapo kesho (Alhamisi) kama mkufunzi wa Argentina.
Ebola:Canada kutoa chanjo ya majaribio
Serikali nchini Canada inase ugonjwa wa Ebola magharibi mwa Afrika ambao hadi sasa umewaua zaidi ya watu 1,000.
Hatua hii ni baada ya shirika la afya duniani kusema ni sawa kimaadili kutumia dawa ambayo bado infanayiwa majaribio kutibu wagonjwa katika hali ya dharura.
Waziri wa afya nchini canada Rona Ambrose amesema kuwa nchi hiyo imetengeneza karibu dosi 500 za dawa hio lakini haijafanyiwa majaribio kwa binadamu.
Wataalamu wanaonya kuwa huenda ikachukua hadi miezi sita kuunda kiwango cha dawa ambacha kinaweza kutumiwa. Kamapuni moja wa kimarekani ambayo ilikuwa imetengeneza dawa za majaribio inasema kuwa kwa sasa kiwango cha dawa ilicho nacho ni kidogo.
Van Gaal awaonyesha Chicharito, Nani mlango wa kutokea Man United
SIKU chache kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya England na kufungwa kwa pazia la usajili katikia ligi hiyo, Kocha wa Manchester United, Louis van Gaal amewaeleza wachezaji sita akiwamo beki wa kulia Rafael kwamba wanaweza kuchapa mwendo.
Marouane Fellaini, Wilfried Zaha, Nani, Shinji Kagawa na kinda yosso Will Keane pia wamevunja 'ndoa' na kikosi hicho cha Van Gaal na hilo limefanyika wakati United ikijifua katika Uwanja wa mazoezi wa Carrington Jumamosi mchana. Inaeleweka kuwa Mholanzi huyo amewaambia Fellaini, Zaha, Nani na Keane klabu hiyo itasikiliza ofa kwao baada ya kuwaweka sokoni rasmi.
Rafael, alishangaa kusikia jina lake likiwa katika orodha hiyo na kwamba pia anaweza kulazimisha kuondoka wakati huu klabu hiyo ikisaka beki wa kulia.
Kagawa atatumika lakini kaelezwa ataanzia benchi nyuma ya Ander Herrera na Juan Mata. Kiungo Anderson na mshambuliaji Javier Hernandez pia nao tayari wanajua kwamba United itasikiliza ofa endapo zitawasili mezani kwao. Southampton, Inter Milan, Tottenham, Atletico Madrid na Juventus zote zimeonyesha nia ya kumsajili Mmexico huyo, wakati Napoli itakuwa tayari kumsajili Fellaini kama dili hilo litakubalika na United. Newcastle inaongoza katika vita ya kumsajili Zaha, huku Crystal Palace, West Ham na Nottingham Forest nazo zikihitaji huduma yake.
Cardiff City imeulizia uwezekano wa kumsajili kwa mkopo Keane ambaye ni pacha wa beki Michael, lakini United inahitaji kumtazama zaidi kabla ya kukamilisha dili hilo.
Kwa sasa United ipo sokoni ikisaka mabeki wapya wawili baada ya kushindwa kumsajili beki wa kati wa Arsenal, Thomas Vermaelen ambaye juzi alijiunga rasmi na Barcelona Mabingwa hao wa zamani wamejipanga kufanya vyema katika msimu huu baada ya msimu uliopita kuboronga na kumaliza kwenye nafasi ya katikati tofauti na mazoea yao.
Eliaquim Mangala ajiunga rasmi na Man City kutoka Porto.
Manchester City imefanikiwa kumsajili beki raia wa Ufaransa Eliaquim Mangala kutoka klabu ya FC Portokwa ada ya paundi milioni 32.. Beki huyo mwenye umri wa miaka 23 mesaini mkataba wa miaka 5 kuichezea klabu hiyo.
Mkali wa movie Robin William akutwa amefariki ndani ya nyumba yake
Robin William ni star aliyeanza kupata mafanikio akifanya kazi kama stand up comedian na baadae kuanza kuonekana kwenye movie.
Akiwa na miaka 63 Robin amefariki dunia kwa kifo ambacho hadi sasa hakijajulikana chanzo chake lakini tetesi zinasema kuna uwezekanao kwamba Robin alijiua.
Mwili wake umekutwa nyumbani kwake huko Tiburon California na watu wa karibu wanasema alikuwa anasumbuliwa na msongo wa mawazo hivi karibuni.
Enzi za uhai wake aliwai kushiriki kwenye movie kama The Fisher King,Good will Hunting,Jumanji,Popeye na nyingine.
Pia alishinda tuzo kama Academy,Golden Globe,Emmy,Grammy na nyinginezo kwa wakati tofauti.
Ushahidi mwingine wa Chris Brown na Rihanna wapo karibu kurudiana
Baada ya siku moja tu Chris Brown ku-post poster la tour ya Rihanna na Eminem kwenye instagram, Chris Brown ameonekana kuendelea kuongeza ukaribu zaidi na Rihanna.
Japokuwa picha haipo clear sana lakini inaonyesha Chris Brown alivyokwenda back stage ambapo alikuwepo Rihanna kwenye moja ya show za tour hiyo.
Picha haionyeshi vizuri lakini kuna mashahidi wengi wanasema kwamba Chris Brown alikuepo backstage akiwa na Tyga na welienda kwa ajili ya Rihanna.
Hii ndio klabu kubwa nchini Uingereza ambayo Rihanna ameripotiwa kutaka kuinunua
Moja ya watu maarufu waliokumbwa na joto kubwa la soka wakati wa michuano ya kombe la dunia, alikuwa ni mwanamuziki Rihanna.
Alikuwa akituma tweets karibia kwenye michezo yote na mwishoni alienda kuhudhuria fainali ya michuano hiyo iliyopigwa kwenye dimba la Maracana kati ya Ujerumani dhidi ya Argentina.
Siku kadhaa nyuma gazeti la Daily Mail la Uingereza liliripoti kwamba staa huyo alikuwa anajiandaa kununua hisa kwenye moja ya vilabu vikubwa nchini Uingereza, lakini hawakutaja jina la timu. Lakini leo hii Jumanne, gazeti moja huko Catalunya liitwalo El Mundo Deportivo limethibitisha kwamba Rihanna anataka kununua hisa nyingi kwenye klabu ya Liverpool.
Rihanna amewahi kuripotiwa kwamba anaishabikia klabu ya Liverpool, jambo ambalo inawezekana El Mundo Deportivo wamemhusisha na ununuzi wa klabu hiyo ya Anfield.
Liverpool kwa sasa inamilikiwa na mmiliki wa makampuni ya American Fenway Sports Group John W. Henry.
LOGARUSIC HAKUPEWA NAFASI YA KUFANYA KAZI YAKE
Simba SC wanajua sababu za msingi kwa nini walimtimua kocha Zdravko Logarusic kwa sababu ni wao wenyewe ndiyo walimuajiri, wao wanajua sababu za msingi kwa nini walikuwa na Loga, hilo ni juu yao kwa sisi ambao tupo nje ya klabu hatewezi kujua sababu hasa ya kufutwa kazi kwa Mcroatia huyo ambaye tayari alifanya kazi kwa kipindi cha nusu msimu wakati Simba ilipomaliza katika nafasi ya nne msimu wa 2013/14.
Kwa mtazamo wa haraka tu unaqwweza kupata sababu ambazo zimevunja mahusiano kati ya Simba na Loga.
Kwa nini Logarusic ametimuliwa Simba? Sababu zipo nyingi,
KIPIGO CHA MABAO 3-0 KUTOKA KWA ZESCO KATIKA ‘SIMBA DAY’
Haileti maana, na wala si kigezo cha kumuhukumu Logarusic kutokana na mchezo huo kwa sababu tangu mwaka 2009, Tamasha hilo lilipoanzishwa Simba imekuwa ni timu ya kufungwa tu. Haijawahi kushinda, vipi leo Logarusic aondolewe kwa sababu za matokeo mabaya katika mchezo huo dhidi ya Zesco ya Zambia. Simba kupteza mchezo huo haikuwa ‘ stori’.
MAHUSIANO MABAYA KATI YA LOGA NA WACHEZAJI
Kuna namna yake unaweza kulitazama suala hili, kiufundi na kiuweledi. Mahusiano kati ya kocha na wachezaji yanakujaje?. Nitatolea mfano nchi za wenzetu ambao soka linaendeshwa kitaalamu.
Mfano ni Luis Van Gaal, anatengeneza orodha ya wachezaji ambao anataka kuwa nao na kuipeleka kwa utawala, pia anaweka orodha ya wachezaji Fulani ambao wanakuwa huru kutafuta timu hata kama wana mikataba.
Marouane Fellaini, ni mfano mzuri katika hili kwa kuwa amepewa ruhusa ya kutafuta timu ambayo anaqweza kucheza. Van Gaaal anafanya hivyo kwa sababu baadhi ya wachezaji hao hawahitaji katika mfumo wake. Mfumo wake wa ufundishaji unawakataa wachezaji hao na hivyo inapelekea moja kwa moja wakose nafasi.
Turudi nyumbani, mfano ni Loga ni wachezaji wangapi ambao amegombana nao? Kwanini inakuwa hivyo? Kuna mazingira ambayo yanatengenezwa na viongozi wenyewe wa klabu ambao wamejiiingiza katika utamaduni husiokuwepo katika soka la kisasa kumsajilia mwalimu wachezaji Loga tayari amefanya kazi Simba kwa muda tangu alipochukua nafasi ya Abdallah King Kibadeni, mwishoni mwa mwaka uliopita.
Simba haikufanya vizuri chini yake, ilifanya vibaya. Moja ya matatizo ya Simba kufanya vibaya msimu uliopita ni kitendo cha uongozi uliokuwepo kufanya usajili na kufanya makocha kushindwa kuweka ,mbinu zao kwa sababu wachezaji wanaosajiliwa si wale ambao wanakuwa wakihitajika moja kwa moja.
Nafikiri, Simba walitakiwa kufikiria kabla ya kumpa mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Kama walifikia uamuzi huo basi wangemuacha afanye usajili ili baadae mwalimu aweze kuwajibishwa kutokana na matokeo ya uwanjani Huwezi kunipa kazi bila vitendea kazi! Niwezeshe kila kitu kisha kaa pembeni nifanye kazi yangu. Lakini kwa Logan a Simba haikuwa hivyo.
Alikuwa akiletewa wachezaji na kuwakataa kutokana na kuwaona hawawezi kuendana na mbinu zake. Loga pia ana ‘ pointi’ ya msingi. NI wakati wa kujifunza kuhusu ‘ soka la kitaaalamu’.
UONGOZI MPYA
Nafikiri haukuwa na mipango na Logarusic japokuwa walimpatia mkataba wa mwaka mmoja, kufukuzwa kwake Juzi kumethibisha jambo hilo ambalo awali liliripotiwa katika mtandao huu.
Loga alipewa mkataba mpya baada ya kuwa nchini kwa wiki mbili, na habari za kutimuliwa kwake zilipoanza kuenea uongozi ukaamua kumpa mkataba ili kuzima uvumi hu. Lakin siku zote ‘ Muda unaongea’ na LOga ameingia katika ‘ taiming’ za wasio mtaka na kuwa muhanga wa kwanza wa mechi za ‘ Simba Day’.
SAID MOURAD ALIPOTEA ‘ MABOYA’ MARA NYINGI KATIKA SARE YA 2-2 YA AZAM FC DHIDI YA ATLABARA
Atlabara walifanya shambulizi zito katika lango la Azam FC katika dakika ya 77 lakini golikipa chipukizi Aishi Manula alifanya kazi kubwa akazima jaribio la timu hiyo ya Sudan Kusini kupata bao la tatu.
Azam ilizidiwa katika eneo la kiungo na kufanya sagu ya ulinzi kuyumba kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha pili. Atlabara walipata kona mbili dhidi ya nne za Azam lakini walionekana kuwa hatari zaidi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kila walipokwenda katika lango la Azam.
Kocha, Patrick Omog aliwaingiza kwa mpigo washambuliaji Hamis Mcha na Didier Kavumbagu baada ya kufungwa bao la pili katika dakika ya 58. Nahodha wa Atlabara , Martin Bony alipiga kiufundi mpira uliookolewa vibaya na walinzi wa Azam ambao uliangukia karibu yake na kufumua shiti kali la kifundi mbali kabisa na kipa Manula ambaye alijitahidi kuufuata bila mafanikio yoyote. Omog alimuanzisha Said Mourad katika nafasi ya ulinzi wa kati akichukua nafasi ya David Mwantika na mlinzi huyo alipotea ‘ maboya’ mara kadhaa kiasi cha kufanya kutooneka kwa ule ubora wa Aggrey Morris ambao umeonekana katika michezo miwili ya mwanzo walipotoka suluhu-tasa na Rayon Sports na siku ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMKM.
Manula ilibidi atoke katika eneo lake la hatari hili kuiokoa timu yake isifungwe katika dakika ya mwisho ya mchezo. Azam ilicheza kama mabingwa wa Bara ili kupata walau pointi moja katika mchezo huo ambao walisumbuliwa na wachezaji warefu wenye nguvu na maarifa wa Atlabara, na mshambulizi aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Muhaiti, Leonel Saint, Mrundi, Kavumbagu akafunga bao lake la kwanza katika mchezo wa tatu tangu aliposajiliwa kutokea Yanga SC katikati ya mwaka huu.
Kavumbagu alimalizia vizuri pasi ya Kipre Tcheche kutoka katika winga ya kulia na kuisawazishia Azam zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika. Pasi maridadi ya kupenyeza iliyopigwa na kiungo Salum Abubakary ilikuja baada ya hali ya kujiamini kuanza kurejea kwa wachezaji wa timu hiyo ambao walisukumwa nyuma kwa dakika 25 za kipindi cha pili katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
Azam ingeweza kushinda mchezo ho kama kiungo Himid Mao angekuwa makini katika dakika za nyongeza baada ya kuwekewa pasi ‘ murua’ na Kipre lakini akapiga nje pembeni ya ‘ engo’ na kuinyima timu yake ushindi ambao ungewavusha vizuri katika hatua ya robo fainali. Ukitoa makosa ya kiuchezaji katika ngome ya kati, nafasi ya kiungo ilijitahidi kuhimili mashambulizi na kasi ya wapinzani wao.
Kipre Boluo alifunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza na muda wote alifanya kazi yaker vizuri katika eneo la kiungo wa ulinzi.
Azam imefikisha pointi tano baada ya kucheza michezo mitatu, Atlabara na KMKM ambao walilazimisha sare ya kufunga bao 1-1 ya Adama City ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza siku ya leo wamefikisha pointi mbili kila timu ikiwa na michezo mitatu. Azam itamaliza mchezo wa mwisho kwa kucheza na Adama City siku mbili zijazo na matokeo ya sare au ushindi yataivusha timu hiyo katika robo fainali.
Omog alionekana kutopendezwa na matokeo hayo lakini atakuwa ameona mapungufu mengi katika timu yake hasa wakati inapokuwa ikishambuliwa.
AZam wanatengeneza nafasi za kufunga lakini bado wanatakiwa kuongeza umakini zaidi ili kuweza kufunga mabao kama walivyofanya dhidi ya KMKM siku mbili zilizopita. Michuano hii ya 40 imekuwa na kiwango kizuri kutoka kwa timu nyingi.
Timu zimeonekana kucheza kwa kasi huku mifumo yao ya kiuchezaji ikionekana. Azam ni timu mojawapo zinazipewa nafasi ya kushinda ubingwa wa michuano hiyo kutokana na mchezo wake wa kasi wanapovuka nusu ya uwanja kuelekea eneo la hatari la timu pinzani.
Mabao sita waliyofunga katika michezo mitatu ni wastani mzuri kwa safu ya mashambulizi lakini wanatakiwa kunoa zaidi makali yao na kuongeza umakini katika ufungaji kama wanataka kutwaa ubingwa huo ambao tayari umetua nchini mara 11.
MAXIMO AANZA KUANGALIA ALICHONACHO KIIZA
Mshambuliaji Mganda, Hamisi Kiiza, ameanza rasmi mazoezi na klabu yake chini ya kocha mkuu wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo ambaye anaangalia uwezo wa mchezaji huyo pamoja na wale wengine ambao wote walikuwa wakizitumikia timu zao za taifa.
Wachezaji ambao walikuwa timu za taifa za nje ni pamoja na Emmanuel Okwi, Haruna Niyonzima na Hamis Kiiza na wale wa Tanzania Kelvin Yondani, Mrisho Ngassa, Simon Msuva, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Oscar Joshua.
Straika huyo ameanza mazoezi rasmi klabuni hapo siku ya Jumatatu akitokea nchini kwao Uganda na kocha wa timu hiyo anataka kupima uwezo wa mchezaji huyo na kama ataridhishwa, ataendelea naye.
Uongozi wa Yanga umemtaka kocha Maximo kuangalia uwezo wa Waganda hao wawili kati ya Kiiza na Okwi ili wajue nani wa kumuacha kwa jinsi alivyowaona kwa kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni imezidi na kufikia 6 hadi sasa huku ikiwa imebaki nafasi moja pekee ya mchezaji mmoja wa nje kuendelea kuitumikia klabu hiyo ambapo ni lazima mmoja tu afungashiwe virago.
Aidha, straika huyo alikuwa akifanya mazoezi kwa bidii huku mara kadhaa akionekana kuwa makini na alichokuwa akielekezwa na kocha ikiwa ni pamoja na kuzungumza naye mambo kadhaa katika mazoezi hayo.
VAN GAAL AMPA ROONEY UNAHODHA MAN UNITED
MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa England, Wayne Rooney ametuliwa kuwa Nahodha wa kikosi cha Manchester United na kocha Louis van Gaal.
Mholanzi huyo amevutiwa shughuli ya mpachika mabao huyo wa England tangu aanze kazi Old Trafford na anaamini atakuwa chaguo sahihi kuwa kiongozi wa wachezaji wenzake katika timu. "Kwangu, wakati wote muhimu chaguo la Nahodha," amesema Van Gaal katika tovuti ya klabu hiyo.
EVERTON YASAJILI WINGA MGHANA WA CHELSEA
| Anakwenda: Winga wa Chelsea na Ghana, Christian Atsu anatarajiwa kujiunga na Everton kwa mkopo wa muda mrefu |
KLABU ya Everton imekubali kumsajili kwa mkopo wa muda mrefu kiungo wa Chelsea, Christian Atsu, kwa mujibu wa kocha Roberto Martinez.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ghana sasa anakwenda kupiga kazi Goodison Park kwa msimu wote wa 2014/2015, kitu ambacho sasa Martinez amethibitisha. Utaratibu wa mkopo umefikiwa baina ya timu hizo mbili, huku kigali cha kufanya kazi kikibaki kuwa kitu pekee kinachomchelewesha Atsu kuwa mchezaji wa tano kusajiliwa na Everton msimu huu.
UNAIKUMBUKA ILE PICHA YA COUTINHO NA MWANAFUNZI WA LOYOLA HIKI NDO KINACHOENDELEA SASA
Uongozi wa Shule ya Sekondary ya Loyola ya Mabibo jijini Dar es Salaam, umewazuia waandishi wa habari kuhudhuria mazoezi ya Yanga.
Waandishi wamezuiwa a uongozi wa Loyola, kisa kikiwa ni kupiga picha ya yule binti aliyeomba sahihi ya mshambuliaji wa Yanga, Coutinho.
Binti huyo alimfuata Coutinho na kumuomba aweke saini kwenye mkono wake, naye kafanya hivyo, huku waandishi wakijinafasi kwa picha. Siku iliyofuata, picha za binti huyo zilijaa kwenye magazeti na mitandao.
Hali ambayo ikaonyesha kuukasirisha uongozi wa shule ambao ukazuia waandishi kuhdhuria mazoezi!
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO HUU NA TUNAOMBA SUPPORT YAKO KWA KUBONYA HAPA
NI PATRICK PHIRI, KOCHA MPYA WA SIMBA SC
Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam, Alikuja akaondoka bila kuaga, alirudi akaondolewa kwa sababu, sasa anarejea tena kwa mara ya tatu klabuni Simba SC kama mkufunzi mkuu wa idara ya ufundi.
Namzungumzia, kocha raia wa Zambia, Patrick Phiri ambaye anatua nchi leo akitokea kwao kujiunga na Simba kwa mara ya tatu katika kipindi cha miaka kumi’. Phiri ameandaliwa mkataba wa miaka miwili na atasaini mara baada ya kuafikiana kuhusu mambo binafsi.
Ni kocha mzuri ambaye wachezaji wengi hupenda kufanya naye kazi. Mahitaji ya lazima ya timu ni kupata ushindi kadri inavyotakiwa lakini hilo litawezekana kama mahusiano ya kijamaa yataboreshwa kati ya uongozi na kocha, kwa maana ya kumuachia majukumu yote ya ufundi mwalimu.
Mara ya kwanza, Phiri aliondoka na hakutaka kurejea kuifundisha timu hiyo alipotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka, 2004 na ilikuja kugundulika kuwa mwalimu huyo alichukizwa na kitendo cha baadhi ya viongozi kumuingilia katika majukumu yake ya upangaji wa timu na kumchagulia wachezaji wa kuwatumia.
Tabia hiyo bado ipo na inaendelea kuwahukumu makocha wengi klabuni Simba na hata, Mcroatia, Zdravko Logarusic ameondoka kwa sababu hizo.
Heshima ya mtu inategemea jitihada zake za ufanyaji wa kazi na kutimiza majukumu yake. Kupendana, kuheshimiana kindugu, viongozi wanatakiwa kuwaamini walimu ambao wamekuwa wakipewa kazi na kuwaacha wafanye kazi yao.
Simba wanatakiwa kuishi maisha ya kijamaa ambayo kila mtu, mchezaji, kiongozi na benchi la ufundi anatakiwa kujua wajibu wake wa uwepo klabuni. Anaijua Simba, amewahi kufanya kazi, na ana mafanikio makubwa, ni sababu tatu ambazo, Zacharia Hans Poppe amesema zimewashawishi kumrejesha kocha huyo bora wa Zambia, mwaka, 1999.
Ni ukweli ulio wazi kuwa rekodi ya Phiri ndani ya uwanja ni bora pengine kuliko walimu wote ambao wamewahi kufanya kazi klabuni hapo. Phiri alichukua nafasi ya Mkenya, James Siang’a mwaka, 2004 na aliweza kuifanya timu hiyo kuwa imara katika mashambulizi huku akiwatumia wachezaji wa nafasi ya kiungo katika safu ya mashambulizi. Shaaban Kisiga, Athumani Machuppa, Nico Nyagawa, Mussa Hassan Mgosi nyota hao walikuwa wachezaji wa kutegemewa katika ufungaji.
Phiri ambaye amewahi kucheza michuano ya AFCON, 1978 na 1982 pia amewahi kushiriki michuano hiyo kama kocha mkuu wa Zambia, mwaka, 2008 nchini Ghana ni mtu asiyeishiwa sababu za kwenda nyumbani mara kwa mara hali ambayo imekuwa ikiathiri utendaji wa timu ndani ya uwanja.
Mara ya mwisho alipoondoka klabuni, Simba alichukizwa na kitendo cha kuingiliwa katika majukumu yake na hivyo kuamua kutoongeza mkataba baada ya kufanya kazi kwa miaka miwili mfululizo na kuwa kocha aliyekaa kwa muda mwingi klabuni hapo katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.
Trott Moloto alidumu kwa mwezi mmoja baada ya kuchukua nafasi ya Phiri mapema, 2005.







































