![]() |
Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na mwenzake Gardner G Habash (wa pili kulia) wakielekea kizimbani. |
Mtangazaji wa kipindi cha jioni cha Clouds FM, Jahazi, Ephraim Kibonde na mtangazaji wa
kipindi cha jioni cha Times FM ‘Maskani’, Gardner Habash, leo wamepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau
amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.
Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura. Kibonde na Gadner wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena
Source:Global Publisher
BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI
0 comments:
Post a Comment