Atlabara walifanya shambulizi zito katika lango la Azam FC katika dakika ya 77 lakini golikipa chipukizi Aishi Manula alifanya kazi kubwa akazima jaribio la timu hiyo ya Sudan Kusini kupata bao la tatu.
Azam ilizidiwa katika eneo la kiungo na kufanya sagu ya ulinzi kuyumba kwa kiasi kikubwa katika kipindi cha pili. Atlabara walipata kona mbili dhidi ya nne za Azam lakini walionekana kuwa hatari zaidi ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kila walipokwenda katika lango la Azam.
Kocha, Patrick Omog aliwaingiza kwa mpigo washambuliaji Hamis Mcha na Didier Kavumbagu baada ya kufungwa bao la pili katika dakika ya 58. Nahodha wa Atlabara , Martin Bony alipiga kiufundi mpira uliookolewa vibaya na walinzi wa Azam ambao uliangukia karibu yake na kufumua shiti kali la kifundi mbali kabisa na kipa Manula ambaye alijitahidi kuufuata bila mafanikio yoyote. Omog alimuanzisha Said Mourad katika nafasi ya ulinzi wa kati akichukua nafasi ya David Mwantika na mlinzi huyo alipotea ‘ maboya’ mara kadhaa kiasi cha kufanya kutooneka kwa ule ubora wa Aggrey Morris ambao umeonekana katika michezo miwili ya mwanzo walipotoka suluhu-tasa na Rayon Sports na siku ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya KMKM.
Manula ilibidi atoke katika eneo lake la hatari hili kuiokoa timu yake isifungwe katika dakika ya mwisho ya mchezo. Azam ilicheza kama mabingwa wa Bara ili kupata walau pointi moja katika mchezo huo ambao walisumbuliwa na wachezaji warefu wenye nguvu na maarifa wa Atlabara, na mshambulizi aliyetokea benchi kuchukua nafasi ya Muhaiti, Leonel Saint, Mrundi, Kavumbagu akafunga bao lake la kwanza katika mchezo wa tatu tangu aliposajiliwa kutokea Yanga SC katikati ya mwaka huu.
Kavumbagu alimalizia vizuri pasi ya Kipre Tcheche kutoka katika winga ya kulia na kuisawazishia Azam zikiwa zimesalia dakika nne mchezo kumalizika. Pasi maridadi ya kupenyeza iliyopigwa na kiungo Salum Abubakary ilikuja baada ya hali ya kujiamini kuanza kurejea kwa wachezaji wa timu hiyo ambao walisukumwa nyuma kwa dakika 25 za kipindi cha pili katika mchezo huo uliokuwa mkali na wa kusisimua.
Azam ingeweza kushinda mchezo ho kama kiungo Himid Mao angekuwa makini katika dakika za nyongeza baada ya kuwekewa pasi ‘ murua’ na Kipre lakini akapiga nje pembeni ya ‘ engo’ na kuinyima timu yake ushindi ambao ungewavusha vizuri katika hatua ya robo fainali. Ukitoa makosa ya kiuchezaji katika ngome ya kati, nafasi ya kiungo ilijitahidi kuhimili mashambulizi na kasi ya wapinzani wao.
Kipre Boluo alifunga bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza na muda wote alifanya kazi yaker vizuri katika eneo la kiungo wa ulinzi.
Azam imefikisha pointi tano baada ya kucheza michezo mitatu, Atlabara na KMKM ambao walilazimisha sare ya kufunga bao 1-1 ya Adama City ya Ethiopia katika mchezo wa kwanza siku ya leo wamefikisha pointi mbili kila timu ikiwa na michezo mitatu. Azam itamaliza mchezo wa mwisho kwa kucheza na Adama City siku mbili zijazo na matokeo ya sare au ushindi yataivusha timu hiyo katika robo fainali.
Omog alionekana kutopendezwa na matokeo hayo lakini atakuwa ameona mapungufu mengi katika timu yake hasa wakati inapokuwa ikishambuliwa.
AZam wanatengeneza nafasi za kufunga lakini bado wanatakiwa kuongeza umakini zaidi ili kuweza kufunga mabao kama walivyofanya dhidi ya KMKM siku mbili zilizopita. Michuano hii ya 40 imekuwa na kiwango kizuri kutoka kwa timu nyingi.
Timu zimeonekana kucheza kwa kasi huku mifumo yao ya kiuchezaji ikionekana. Azam ni timu mojawapo zinazipewa nafasi ya kushinda ubingwa wa michuano hiyo kutokana na mchezo wake wa kasi wanapovuka nusu ya uwanja kuelekea eneo la hatari la timu pinzani.
Mabao sita waliyofunga katika michezo mitatu ni wastani mzuri kwa safu ya mashambulizi lakini wanatakiwa kunoa zaidi makali yao na kuongeza umakini katika ufungaji kama wanataka kutwaa ubingwa huo ambao tayari umetua nchini mara 11.
0 comments:
Post a Comment