Thursday, August 28, 2014

PICHAZ: K LYINN NI MREMBO WA KUZALIWA …TAZAMA PICHA HIZI!!

Q-Jay kusikika tena kwenye bongo fleva baada ya ukimya mrefu toka aokoke

Baada ya miaka kadhaa tangu mwimbaji wa R&B Joseph Kelvin Mapunda aka Q-Jay wa Wakali Kwanza kutangaza kuacha game ya bongo fleva, anatarajiwa kusikika tena kwenye muziki huo katika wimbo mpya. Q-Jay ni miongoni mwa wasanii watakaosikika kwenye wimbo mpya wa Dj Aaron unaotarajiwa kutoka Ijumaa (Agosti 29). Dj Aaron amewashirikisha Banana Zorro, Barnaba na Q- Jay katika wimbo huo uitwao ‘Peace One Day’, ambao ni wa kuhamasisha amani. Miaka kadhaa iliyopita Q-Jay aliyewahi kufanya vizuri na nyimbo kama ‘Sifai’, aliamua kuachana na muziki wa kidunia baada ya kuokoka na kutangaza kuwa atakuwa akifanya muziki wa gospel.

Ungana na familia ya habari kwa ku BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO ALHAMISI ZIPO HAPA

Arsenal wapo tayari kutoa dau la pauni milioni 50 kumtaka Edinson Cavani kutoka Paris St-Germain, kutokana na Olivier Giroud kuwa na uwezekano wa kutocheza kwa muda mrefu kutokana na jeraha la mguu (Daily Express), Arsenal pia wanamtaka Danny Welbeck, 23, kutoka Manchester United, kuziba nafasi ya Giroud, lakini Man U wanasita kumuuza Welbeck (Daily Mail), boss wa Arsenal vilevile anataka kumchukua kwa mkopo Radamel Falcao, 28, kutoka Monaco, na pia Loic Remy, 27, ambaye anapatikana kwa pauni milioni 8.5 kutoka QPR (the Guardian), boss wa Manchester United Louis van Gaal anafikiria kutaka kumsajili kiungo wa Liverpool Joe Allen, 24, kwa kutoa pauni milioni 20, (Daily Star), United wanafanya mazungumzo ya kumsajili Daley Blind, 24, huku kipa wa zamani wa Man U, Edwin van der Sar akiwa Manchester kukamilisha uhamisho wa beki huyo wa Ajax (Daily Star), Manchester United pia wanafikiria kumtoa Shinji Kagawa, 25, au Javier Hernandez, 26, kama chambo katika mkataba wa kumchukua kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, (Independent), Real Madrid watatumia kiasi kikubwa cha fedha za mauzo ya Angel Di Maria, kumnunua mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao (Le Sport), AC Milan wamethibitisha kuwa wanataka kuwasajili Fernando Torres, 30, na kiungo Marco van Ginkel, 21 kutoka Chelsea (Daily Express), AC Milan wamechoka kumsubiri Torres kuamua anataka nini na wamempa makataa, huku wakijiandaa kuanza kumfuatilia Roberto Soldado, 29, kutoka Tottenham au Fabio Borini, 23, wa Liverpool (Inside Futbol), Tottenham wanajiandaa kukamilisha usajili wa beki wa Sevilla Federico Fazio, 27, baada ya kulipa pauni milioni 8 za kipengele cha ununuzi (Daily Telegraph), Spurs pia wanafikiria kumfuatilia kiungo kutoka Cameroon Alexandre Song, 26, ambaye ameambiwa anaweza kuondoka Barcelona bure (the Times), boss wa QPR Harry Redknapp yuko tayari kupanda dau kwa kiungo wa West Ham Mohammed Diame, 27, (Daily Mirror), Alvaro Arbeloa anataka kuondoka Real Madrid kabla ya dirisha la usajili halijafungwa (El Chiringuito), Manchester United wanajiandaa kutoa dau jipya la pauni milioni 33.4 kwa Juventus kumtaka Arturo Vidal (Gazzetta dello Sport), Real Madrid watapambana na Barcelona na Atletico Madrid kutaka kumsajili Marco Reus kutoka Borussia Dortmund (AS), Hatem Ben Arfa anataka kubakia Newcastle licha ya meneja Alan Pardew kutompanga (Newcastle Evening Chronicle), Arsene Wenger anataka kumsajili mshambuliaji wa zamani wa Birmingham City, Nikola Zigic ambaye ni mchezaji huru (www.zurnal.rs). Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Zimesalia siku tano kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Source salim kikeke

Posted via Blogaway

AY na Diamond wadai watahakikisha Chidi Benz anasimama vizuri kimuziki

AY amedai kuwa kuwa yeye na Diamond watahakikisha Chidi Benz anasimama vizuri baada ya kuyumba hapo awali. AY ameiambia Bongo5 kuwa kama ilivyo kawaida yake kumsaidia msanii mmoja kila mwaka, mwaka huu atahakikisha Chidi anakaa pazuri. “Huwa nina uhakika wa kufanya comeback nzuri tu, sio kwamba ninavyomsupport Chidi tunapata faida yoyote. Kila mwaka huwa ninampick mtu mmoja, so mimi na Diamond tuliamua kuwekeza kwenye audio pamoja na kufanya naye video pamoja kwa gharama zetu sisi. Kama unavyoona promotion yake, mpaka sasa hivi tupo kwenye process ya kufanya video. Bado hatujajua tutafanya wapi video ila tupo kwenye maandalizi ya mavazi, location na mambo mengine,”amesema AY. Hivi karibuni Chidi Benz alitoa wimbo ‘Mpaka Kuchee’ aliowashirikisha AY na Diamond.

Kama bado ujajiunga nasi BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

HIZI 3D TATOO LAZIMA UZITAZAME KWAMAKINI...VINGINEVYO UTADHANI UONGO!!!!

‘ HUU NDIYO UBORA WA KWANZA WA YANGA SC’

Na Baraka Mbolembole, Dar es Salaam, Tayari, Yanga SC imecheza michezo miwili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya kandanda Tanzania Bara ambayo inataraji kuanza kutimua vumbi lake, 20 Septemba.IKiwa katika wiki ya pili ya michezo yote miwili dhidi ya timu za Chipukizi ya Pemba ambayo waliichapa kwa bao 1-0 lililofungwa na mshambulizi mpya, Geilson Santos ‘ Jaja’. Mchezo wa pili timu hiyo ilishinda kwa mabao 2-0 dhidi ya Shanghani FC ya Unguja Haruna Niyonzima amerejea katika kiwango chake cha juu na mchezaji huyo wa kimataifa wa Rwanda tayari ameonekana ‘ muhimili wa sehemu ya kiungo’ kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira kwa muda mrefu bila kuupoteza na kuchezesha timu kwa pasi za uhakika. Maximo anaonekana kutafuta mchezaji ambaye atacheza nafasi ya kiungo wa chini-namba sita. Mbuyu Twite amekuwa akichezeshwa katika nafasi hiyo na hajamuangusha mwalimu wake. Salum Telela anaonekana kuyashinda majeraha na mchezaji huyo wa nafasi ya kiungo anaweza kurudishwa nyuma zaidi katika nafasi ya beki wa kulia. Telela amechezshwa katika nafasi ya ulinzi katika michezo iliyopita ili kupisha vipaji zaidi katika nafasi ya kiungo. Nguvu na Twite zimefanya, Niyonzima kucheza kwa uhuru mkubwa katika eneo la mashambulizi, huku akisaidiwa na SAimon Msuva, Mrisho Ngassa, na Andrey Coutinho. Maximo yupo katika wakati mgumu bila shaka, kwa sababu wachezaji wote wameonyesha viwango vya juu katika maandalizi Yanga watakuwa timu yenye kasi msimu ujao, tofauti na ilivyozoeleka kwa sababu wachezaji ambao Maximo anao katika nafasi ya kiungo wote ni wenye kasi, wajanja, na watulivu hata pale mpira unapokuwa ukimilikiwa na wachezaji wa timu pinzani. Yanga wapo katika mchakato wa kutafuta mechi zaidi za kirafiki na habari zilizopo ni kwamba wanafanya mipango ya kucheza na timu za St. George ya Ethiopia, Gor Mahia ya Kenya au Zesco ya Zambia, kama watapata michezo walau miwili dhidi ya timu hizo itakuwa na faida kubwa kwa mwalimu Maximo ambaye hawezi kusema moja kwa moja kuwa tayari timu yake imeimarika kwa kuzifunga timu hizo za madaraja ya chini huko Zanzibar. Mechi hizo zinawezekana kumsaidia Maximo kujua wachezaji wake wameiva namna gani katika suala la uvumilivu, mbinu, na ufundi wanapokutana na timu ngumu, na anaweza kuitimia mechi ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC kupima kikosi chake cha kwanza. Maximo anaitengeneza Yanga kwa kutumia wachezaji wa nafasi ya kiungo, kwani amekuwa akiwachezesha viungo watano na mshambulizi mmoja katika michezo ya kirafiki. Kwa nini asifanye hivyo wakati anao wachezaji wengi wenye maarifa binafasi ya ufungaji . Alipokuwa kocha wa Taifa Stars, Maximo alikuwa akipendelea zaidi kutimia mfumo wa 4-5-1 kwa lengo la kudhibiti mechi na kutafauta ushindi wa aina yoyote, alipata wakati mgumu kutokana na kukosa wachezaji wazuri katika eneo la katikati ya uwanja na sehemu ya mashambulizi kutokana na kukosa wachezaji sahihi wa kucheza katika mfumo huo. Mfumo huo ameuleta Yanga . Niyonzima alikuwa akitumika zaidi kama kiungo mchezesha timu akitokea upande wa kushoto na kuingia hadi katikati ya uwanja chini ya makocha Ernie Brants na Hans Van Der Pluijm, ila atarudishwa katika eneo la kati kwa sababu, Ngassa Coutinho wanauwezo wa kutimiza majukumu hayo. Msuva anacheza upande mmoja tu, upande wa kulia, faida kubwa kutoka kwa kiungo huyo ni kucheza soka la kupanda na kushuka, huku akitengeneza mabao kwa mipira ya krosi, na wakati mwingine akifunga mwenyewe, Coutinho anacheza kushoto zaidi, ni mwepesi na ana kasi. Ngassa ana uwezo wa kucheza kila upande sehemu ya mashambulizi, na Maximo amekuwa akimtumia zaidi kama mshambulizi wa pili akicheza nyuma ya Jaja. Kwa maana hiyo sehemu ya kiungo ya Yanga itakuwa na wachezaji wa kubadilika badilika katika uchezaji wao uwanjani. Timu nyingi zipata wakati mgumu dhidi ya Yanga, kiufundi wanatakiwa kuongeza umakini na namna ya kulazimisha matokeo wakati mechi inapokuwa ngumu huku wakicheza katika utulivu wao. Kama unataka kuifunga Yanga SC msimu ujao jipange vizuri kuthibiti eneo lao la kiungo.

Habari zingine  BOFYA HAPA 


Posted via Blogaway

COUTINHO APIGA BONGE LA BAO YANGA SC IKIICHAPA KMKM 2-0 AMAAN

Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR YANGA SC imemaliza ziara yake ya kisiwani Unguja kwa ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, Uwanja wa Amaan, Zanzibar usiku huu. Mabao ya Yanga SC hii leo yamefungwa na Mbrazil, Andrey Coutinho na mzalendo Hussein Javu, moja kila kipindi. Lakini lilikuwa ni bao la Coutinho lililosisimua zaidi usiku huu, akifumua shuti la umbali wa mita 25 baada ya kupata pasi maridadi ya Mrisho Ngassa dakika ya 44. Bao la pili pia lilipatikana dakika ya 89 na ushei baada ya Javu kufumua shuti la mbali pia, ambalo kipa wa KMKM hakuliona. Kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya Shangani, na leo pia kocha Mbrazil, Marcio Maximo alibadili kikosi kizima kipindi cha pili, akimuacha mchezaji mmoja tu, Kevin Yondan. Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Amos Abel ambao waliingia kipindi cha pili, baadaye walitolewa na nafasi zao kuchukuliwa na Said Bahanuzi, Edward Charles na Javu. Tegete alikosa mabao mawili ya wazi baada ya pasi nzuri za Simon Msuva akiwa ndani ya eneo la sita na bila shaka hilo ndilo lililomfanya Maximo amrejeshe benchi. Kwa mara nyingine, mshambuliaji Mbrazil, Geilson Santana ‘Jaja’ ameshindwa kufurukuta huku Coutinho akiendelea kudhihirisha ubora wake. Huo unakuwa mchezo wa tatu kwa ujumla Yanga SC kucheza visiwani hapa na inashinda mechi zote, 1-0 dhidi ya Chipukizi Uwanja wa Gombani, Pemba na 2-0 dhidi ya Shangani Uwanja wa Amaan pia. Yanga SC inatarajiwa kuondoka kesho mjini hapa kurejea Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wa Ngao ya Jamii, dhidi ya Azam FC Septemba 13, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Deo Munishi ‘Dida’/Juma Kaseja dk46, Salum Telela/Said Juma dk46, Oscar Joshua/Amos Abel dk46/ Edward Charles dk70, Nadir Haroub ‘Cannavaro’/Rajab Zahir dk46, Mbuyu Twite/ Omega Seme dk46, Mrisho Ngassa/Simon Msuva dk46, Hassan Dilunga/Nizar Khalfan dk46, Geilson Santana ‘Jaja’/Jerry Tegete dk46/ Said Bahanuzi dk70, Haruna Niyonzima/ Hamisi Thabiti dk46 na Andrey Coutinho/ Hamisi Kiiza/Hussein Javu.

Posted via Blogaway

SANCHEZ AIPELEKA ARSENAL MAKUNDI LIGI YA MABINGWA ULAYA

BAO pekee la Alexis Sanchez limeipa ushindi wa 1-0 Arsenal katika mchezo wa marudiano hatua ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa Uwanja wa Emirates usiku huu. Kwa matokeo hayo, timu ya Arsene Wenger inasonga mbele hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 1-0, baada ya sare ya 0-0 awali katika mchezo wa kwanza Uturuki. Wenyeji walilazimika kucheza pungufu ya mchezaji mmojka kwa dakika 15 za mwisho, baada ya Matheiu Debuchy kutolewa nje kwa kadi ya pili ya njano. The Gunners wanakwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 17 mfululizo baada ya ushindi huo. Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Monreal, Flamini, Oxlade-Chamberlain, Cazorla, Wilshere, Ozil/Chambers dk76 na Sanchez. Besiktas: Zengin, Koybasi, Franco, Gulum, Motta, Hutchinson, Ozyakup, Kavlak/Uysal dk76, Pektemek/Tosun dk87, Ba, Sahan/Tore dk60.

 KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZA KIMICHEZO ZIKUFIKIE KIRAHISI 


Posted via Blogaway