Na Mahmoud Zubeiry, ZANZIBAR
YANGA SC imemaliza ziara yake ya kisiwani
Unguja kwa ushindi wa mabao 2-0 katika
mchezo wa kirafiki dhidi ya KMKM, Uwanja wa
Amaan, Zanzibar usiku huu.
Mabao ya Yanga SC hii leo yamefungwa na
Mbrazil, Andrey Coutinho na mzalendo
Hussein Javu, moja kila kipindi.
Lakini lilikuwa ni bao la Coutinho lililosisimua
zaidi usiku huu, akifumua shuti la umbali wa
mita 25 baada ya kupata pasi maridadi ya
Mrisho Ngassa dakika ya 44.
Bao la pili pia lilipatikana dakika ya 89 na
ushei baada ya Javu kufumua shuti la mbali
pia, ambalo kipa wa KMKM hakuliona.
Kama ilivyokuwa katika mchezo dhidi ya
Shangani, na leo pia kocha Mbrazil, Marcio
Maximo alibadili kikosi kizima kipindi cha pili,
akimuacha mchezaji mmoja tu, Kevin Yondan.
Jerry Tegete, Hamisi Kiiza na Amos Abel
ambao waliingia kipindi cha pili, baadaye
walitolewa na nafasi zao kuchukuliwa na Said
Bahanuzi, Edward Charles na Javu.
Tegete alikosa mabao mawili ya wazi baada ya
pasi nzuri za Simon Msuva akiwa ndani ya
eneo la sita na bila shaka hilo ndilo
lililomfanya Maximo amrejeshe benchi.
Kwa mara nyingine, mshambuliaji Mbrazil,
Geilson Santana ‘Jaja’ ameshindwa kufurukuta
huku Coutinho akiendelea kudhihirisha ubora
wake.
Huo unakuwa mchezo wa tatu kwa ujumla
Yanga SC kucheza visiwani hapa na inashinda
mechi zote, 1-0 dhidi ya Chipukizi Uwanja wa
Gombani, Pemba na 2-0 dhidi ya Shangani
Uwanja wa Amaan pia.
Yanga SC inatarajiwa kuondoka kesho mjini
hapa kurejea Dar es Salaam kwa maandalizi ya
mchezo wa Ngao ya Jamii, dhidi ya Azam FC
Septemba 13, mwaka huu Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Kikosi cha Yanga SC leo kilikuwa; Deo Munishi
‘Dida’/Juma Kaseja dk46, Salum Telela/Said
Juma dk46, Oscar Joshua/Amos Abel dk46/
Edward Charles dk70, Nadir Haroub
‘Cannavaro’/Rajab Zahir dk46, Mbuyu Twite/
Omega Seme dk46, Mrisho Ngassa/Simon
Msuva dk46, Hassan Dilunga/Nizar Khalfan
dk46, Geilson Santana ‘Jaja’/Jerry Tegete dk46/
Said Bahanuzi dk70, Haruna Niyonzima/
Hamisi Thabiti dk46 na Andrey Coutinho/
Hamisi Kiiza/Hussein Javu. |
0 comments:
Post a Comment