Thursday, August 28, 2014
 |
| BAO pekee la Alexis Sanchez limeipa ushindi
wa 1-0 Arsenal katika mchezo wa marudiano
hatua ya mchujo kuwania kupangwa kwenye
makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya uliopigwa
Uwanja wa Emirates usiku huu.
Kwa matokeo hayo, timu ya Arsene Wenger
inasonga mbele hatua ya makundi kwa ushindi
wa jumla wa 1-0, baada ya sare ya 0-0 awali
katika mchezo wa kwanza Uturuki.
Wenyeji walilazimika kucheza pungufu ya
mchezaji mmojka kwa dakika 15 za mwisho,
baada ya
Matheiu Debuchy kutolewa nje kwa kadi ya
pili ya njano.
The Gunners wanakwenda hatua ya makundi
ya Ligi ya Mabingwa kwa mara ya 17 mfululizo
baada ya ushindi huo.
Kikosi cha Arsenal kilikuwa: Szczesny,
Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Monreal,
Flamini, Oxlade-Chamberlain, Cazorla,
Wilshere, Ozil/Chambers dk76 na Sanchez.
Besiktas: Zengin, Koybasi, Franco, Gulum,
Motta, Hutchinson, Ozyakup, Kavlak/Uysal
dk76, Pektemek/Tosun dk87, Ba, Sahan/Tore
dk60. |
KAMA BADO UJAJIUNGA NASI BONYA HAPA ILI KILA NIKIPATA HABARI ZA KIMICHEZO ZIKUFIKIE KIRAHISI
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment