Thursday, August 28, 2014
 |
AY amedai kuwa kuwa yeye na Diamond
watahakikisha Chidi Benz anasimama vizuri
baada ya kuyumba hapo awali.
AY ameiambia Bongo5 kuwa kama ilivyo
kawaida yake kumsaidia msanii mmoja kila
mwaka, mwaka huu atahakikisha Chidi anakaa
pazuri.
“Huwa nina uhakika wa kufanya comeback
nzuri tu, sio kwamba ninavyomsupport Chidi
tunapata faida yoyote. Kila mwaka huwa
ninampick mtu mmoja, so mimi na Diamond
tuliamua kuwekeza kwenye audio pamoja na
kufanya naye video pamoja kwa gharama zetu
sisi. Kama unavyoona promotion yake, mpaka
sasa hivi tupo kwenye process ya kufanya
video. Bado hatujajua tutafanya wapi video ila
tupo kwenye maandalizi ya mavazi, location na
mambo mengine,”amesema AY.
Hivi karibuni Chidi Benz alitoa wimbo ‘Mpaka
Kuchee’ aliowashirikisha AY na Diamond. |
Kama bado ujajiunga nasi BOFYA HAPA
Posted via Blogaway
0 comments:
Post a Comment