| Na Baraka
Mbolembole,
Dar es Salaam,
Tayari, Yanga
SC imecheza
michezo miwili
ya kujiandaa na
msimu mpya
wa ligi kuu ya
kandanda
Tanzania Bara
ambayo
inataraji
kuanza
kutimua vumbi
lake, 20
Septemba.IKiwa
katika wiki ya
pili ya michezo
yote miwili
dhidi ya timu
za Chipukizi ya
Pemba ambayo
waliichapa kwa
bao 1-0
lililofungwa na
mshambulizi
mpya, Geilson
Santos ‘ Jaja’.
Mchezo wa pili
timu hiyo
ilishinda kwa
mabao 2-0
dhidi ya
Shanghani FC
ya Unguja
Haruna
Niyonzima
amerejea katika
kiwango chake
cha juu na
mchezaji huyo
wa kimataifa
wa Rwanda
tayari
ameonekana ‘
muhimili wa
sehemu ya
kiungo’
kutokana na
uwezo wake wa
kumiliki mpira
kwa muda
mrefu bila
kuupoteza na
kuchezesha
timu kwa pasi
za uhakika.
Maximo
anaonekana
kutafuta
mchezaji
ambaye
atacheza nafasi
ya kiungo wa
chini-namba
sita. Mbuyu
Twite amekuwa
akichezeshwa
katika nafasi
hiyo na
hajamuangusha
mwalimu wake.
Salum Telela
anaonekana
kuyashinda
majeraha na
mchezaji huyo
wa nafasi ya
kiungo
anaweza
kurudishwa
nyuma zaidi
katika nafasi ya
beki wa kulia.
Telela
amechezshwa
katika nafasi ya
ulinzi katika
michezo
iliyopita ili
kupisha vipaji
zaidi katika
nafasi ya
kiungo. Nguvu
na Twite
zimefanya,
Niyonzima
kucheza kwa
uhuru mkubwa
katika eneo la
mashambulizi,
huku
akisaidiwa na
SAimon Msuva,
Mrisho Ngassa,
na Andrey
Coutinho.
Maximo yupo
katika wakati
mgumu bila
shaka, kwa
sababu
wachezaji wote
wameonyesha
viwango vya
juu katika
maandalizi
Yanga
watakuwa timu
yenye kasi
msimu ujao,
tofauti na
ilivyozoeleka
kwa sababu
wachezaji
ambao Maximo
anao katika
nafasi ya
kiungo wote ni
wenye kasi,
wajanja, na
watulivu hata
pale mpira
unapokuwa
ukimilikiwa na
wachezaji wa
timu pinzani.
Yanga wapo
katika
mchakato wa
kutafuta mechi
zaidi za kirafiki
na habari
zilizopo ni
kwamba
wanafanya
mipango ya
kucheza na
timu za St.
George ya
Ethiopia, Gor
Mahia ya Kenya
au Zesco ya
Zambia, kama
watapata
michezo walau
miwili dhidi ya
timu hizo
itakuwa na
faida kubwa
kwa mwalimu
Maximo
ambaye hawezi
kusema moja
kwa moja kuwa
tayari timu
yake
imeimarika kwa
kuzifunga timu
hizo za
madaraja ya
chini huko
Zanzibar.
Mechi hizo
zinawezekana
kumsaidia
Maximo kujua
wachezaji wake
wameiva
namna gani
katika suala la
uvumilivu,
mbinu, na
ufundi
wanapokutana
na timu
ngumu, na
anaweza
kuitimia mechi
ya Ngao ya
Jamii dhidi ya
Azam FC
kupima kikosi
chake cha
kwanza.
Maximo
anaitengeneza
Yanga kwa
kutumia
wachezaji wa
nafasi ya
kiungo, kwani
amekuwa
akiwachezesha
viungo watano
na mshambulizi
mmoja katika
michezo ya
kirafiki. Kwa
nini asifanye
hivyo wakati
anao wachezaji
wengi wenye
maarifa
binafasi ya
ufungaji .
Alipokuwa
kocha wa Taifa
Stars, Maximo
alikuwa
akipendelea
zaidi kutimia
mfumo wa
4-5-1 kwa
lengo la
kudhibiti mechi
na kutafauta
ushindi wa aina
yoyote, alipata
wakati mgumu
kutokana na
kukosa
wachezaji
wazuri katika
eneo la katikati
ya uwanja na
sehemu ya
mashambulizi
kutokana na
kukosa
wachezaji
sahihi wa
kucheza katika
mfumo huo.
Mfumo huo
ameuleta
Yanga .
Niyonzima
alikuwa
akitumika zaidi
kama kiungo
mchezesha
timu akitokea
upande wa
kushoto na
kuingia hadi
katikati ya
uwanja chini ya
makocha Ernie
Brants na Hans
Van Der Pluijm,
ila atarudishwa
katika eneo la
kati kwa
sababu, Ngassa
Coutinho
wanauwezo wa
kutimiza
majukumu
hayo.
Msuva
anacheza
upande mmoja
tu, upande wa
kulia, faida
kubwa kutoka
kwa kiungo
huyo ni
kucheza soka la
kupanda na
kushuka, huku
akitengeneza
mabao kwa
mipira ya
krosi, na
wakati
mwingine
akifunga
mwenyewe,
Coutinho
anacheza
kushoto zaidi,
ni mwepesi na
ana kasi.
Ngassa ana
uwezo wa
kucheza kila
upande sehemu
ya
mashambulizi,
na Maximo
amekuwa
akimtumia
zaidi kama
mshambulizi
wa pili
akicheza
nyuma ya Jaja.
Kwa maana
hiyo sehemu ya
kiungo ya
Yanga itakuwa
na wachezaji
wa kubadilika
badilika katika
uchezaji wao
uwanjani.
Timu nyingi
zipata wakati
mgumu dhidi
ya Yanga,
kiufundi
wanatakiwa
kuongeza
umakini na
namna ya
kulazimisha
matokeo
wakati mechi
inapokuwa
ngumu huku
wakicheza
katika utulivu
wao. Kama
unataka
kuifunga Yanga
SC msimu ujao
jipange vizuri
kuthibiti eneo
lao la kiungo. |
0 comments:
Post a Comment