Tuesday, August 26, 2014

Lingine linalosemwa kwenye uhusiano wa Wema Sepetu na Diamond Platnumz.

Ukubwa wa majina yao unawafanya kila inapoitwa leo kuzungumziwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na uhusiano wao wa kimapenzi huku stori nyingi zimekuwa zikitoka zinazowahusu. Wiki chache inasemekana uhusiano huu haukuwa kwenye hali nzuri baada ya mashabiki wa Wema kuanza kampeni ambayo ilikua ikimtaka Diamond Platnumz amrejeshe Wema aliyekua akicheza filamu kama zamani. Mezani kwa Soudy Brown leo ni kuhusu isue hii ambayo kwa sasa inasemekana Diamond na Wema wameachana tena ingawa si mara ya kwanza ila uhakika wa stori tunaungana na Soudy Brown kumsikiliza Wema akizungumzia hili.bonyeza play kusikiliza

>>>>>>>>>> play hapa <<<<<<<<<<<<<<<<<\\\\
Crd millardayo

HUU NDO MSIMAMO WA LIGI KUU YA UINGEREZA (EPL)

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI ULAYA YA LEO JUMANNE ZIPO HAPA

Manchester United wamekamilisha majadiliano na Real Madrid na watalipa pauni milioni 63.9 na kuvunja rekodi ya Uingereza kumnunua winga Angel Di Maria (Sky Sports), mchezaji huyo kutoka Argentina huenda akafikia kuuzwa kwa pauni milioni 72, milioni 60 zikilipwa mwanzo na milioni 12 baadaye (Daily Mirror), Juventus wataanza mazungumzo na Arsenal kuhusu Lukas Podolski. Juventus wanamtaka kwa mkopo lakini Arsenal wanataka kumuuza (Daily Telegraph), boss wa Real Madrid Carlo Ancelotti amesema Sami Khedira, 27, hatoondoka licha ya kufuatiliwa na Arsenal, Bayern Munich na Manchester United (Guardian), meneja wa Everton Roberto Martinez amesema bado anaweza kumsajili Samuel Eto'o, 33, au Danny Welbeck, 23, katika wiki ya mwisho ya dirisha la usajili (Times), boss wa Arsenal Arsene Wenger amemuulizia beki mkabaji wa Brazil Luiz Gustavo, 27, anayechezea Wolfsburg (Daily Mirror), Southampton wamepanda dau kwa winga wa Tottenham Andros Townsend, 23, (ESPN FC), meneja wa Southampton Ronald Koeman yuko tayari kuanza kumfuatilia tena winga wa Norwich Nathan Redmond, 20, (Sun), Liverpool watalazimika kuchukua hatua za haraka kumsajili Radamel Falcao, 28, wakati Juventus wakimtaka mshambuliaji huyo wa Monaco kwa mkopo (Daily Star), Fernando Torres hatoondoka Chelsea bila ya mkataba wa kitita cha pauni milioni 8.5 kutolewa. Roma wanamtaka mshambuliaji huyo (Sun), Sunderland wamekuwa na mazungumzo na winga wa zamani wa Chelsea, Salomon Kalou, 29, ambaye pia anatazamwa na Arsenal, Liverpool na Everton (Daily Express), boss wa Sunderland ana matumaini ya kupata jibu iwapo mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini, 23, atajiunga nao au la (Sunderland Echo), West Ham wamemuulizia beki wa Manchester City Micah Richards, 26, ambaye anaonekana huenda akaondoka City wiki hii (Sun), QPR wamehusishwa na kipa wa Reading Alex McCarthy, 24, (Daily Star), AC Milan wanamtaka Samuel Eto'o na Fernando Torres kuziba pengo la Mario Balotelli (Gazetta dello Sport), Juventus wana nafasi kubwa ya kumshawishi Radamel Falcao kujiunga nao kwa mkopo wa mwaka mmoja (Gazetta dello Sport), Lukas Podolski huenda akasaini mkataba wa miaka mitatu na Wolfsburg na watalipa euro milioni 12 kumsajili kutoka Arsenal (L'Equipe). Zimesalia siku saba kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.credit salim kikeke

BREAKING NEWZ:::PENZI LA WEMA NA DIAMOND TENA BAAAASI WAMEBWAGANA VIBAYA SANA SOMA HAPA

Habari zilizotukia hivi punde ni kwamba wema na diamond wameacahana rasimi leo asubuh,akiongea na kituo kimoja cha redio wema kwa masikitiko akionekana mwenye majonzi alisema please i dont like to talk about it

Stay tune kwa habari zaidi
Source:mzalendohuru.blogspot.com

MASOGANGE AWATUKANA WANAUME MATUSI MAZITO WANAOMPELEKEA HABARI ZAKE KWA JAMAA YAKE WA SAUZI

Kama mnavyojua AGNES MASOGANGE kwasasa yupo BONGO na Yule jamaa yake yupo SAUZI..sasa kutokana na taarifa za kile ambacho MASOGANGE anakifanya hapa mjini kumfikia jamaa yake huko SAUZI kupitia jamaa ambao wanampa ripoti zote kutoka hapa BONGO na hivyo kupelekea kuhatarisha penzi la MASOGANGE na huyo jamaa…MASOGANGE AMEAMUA KUFUNGUKA Kupitia ukurasa wake wa INSTAGRAM aliweka picha hiyo na kuandika kama unavyoona hapa!!!

BALOTELLI ALIVYOSHUHUDIA LIVERPOOL YAKE IKITESWA NA TIMU YAKE YA ZAMANI USIKU HUU ETIHAD

Vijana wapya: Mshambuliaji mpya wa Liverpool, Mtaliano Mario Balotelli akiwa na mchezaji mwingine mpya wa klabu hiyo, Adam Lallana jukwaani Uwanja wa Etihad wakati wa mechi dhidi ya wenyeji, Manchester City. Mwingine chini mbele ni gwiji wa klabu, Kenny Dalglish. Man City imeshinda 3-1.

HIKI NDO KITU KINACHOKWAMISHA BEKI MPYA KUANZA KAZI MAN UNITED

BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo hajacheza mechi yoyote kutokana na kwamba bado hajapata kibali cha kufanyia kazi nchini Uingereza. Louis van Gaal alitarajia kumtumia Rojo katika mchezo waliomaliza kwa safe ya kufungana bao 1-1 na Sunderland Jumapili, lakini sasa atamsikilizia katika mchezo wa genii dhidi ya Burnley Jumamosi. Beki huyo mwenye umri wa miaka 24, amekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 16 Man United wiki iliyopita, lakini atalazimika kusubiri hadi patine kibali cha kufanyia kazi. Rojo anaingia kwenye orodha ndefu ya wachezaji wanaokosekana uwanjani kwa sasa United, wengine wakiwa ni Luke Shaw, Michael Carrick, Marouane Fellaini, Jesse Lingard, Rafael da Silva na Ander Herrera ambao wote ni majeruhi. Van Gaal anatarajiwa kuendelea kuwapa nafasi wachezaji chipukizi usiku wa Jumanne kama Michael Keane na Tyler Blackett katika kikosi cha kwanza kwenye mchezo huo.

YANGA YAINGIZA MILIONI 7 ZANZIBAR, SIMBA MILIONI 3

Yanga imeingiza mapato mengi zaidi katika mechi yake ya kirafiki dhidi ya Shangani iliyopigwa jana kwenye Uwanja wa Amaan mjini hapa. Katika mechi hiyo iliyomalizika kwa Yanga kushinda kwa mabao 2-0, mapato yaliyopatikana ni Sh milioni 7 na ushee. Lakini wapinzani wake Simba wameingiza Sh milioni 3 tu katika mechi yao ya kirafiki iliyopigwa jana hiyo na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kilimani. Yanga ndiyo ilianza kucheza halafu mashabiki wote wakatolewa nje na kuanza kuingia upya kushuhudia mechi ya pili ambayo ilikuwa ya Simba. Ingawa mapato hayo yamekuwa yakifanywa siri kubwa na Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), lakini SALEHJEMBE limeng’amua kila kitu kuwa Yanga wameingiza mapato mengi zaidi. Kiingilio katika mechi hizo ilikuwa ni Sh 2,000 na 5,000.credit salehjembe

TIMU ZA ENGLAND ZAENDELEZA KUFANYA USAJILI WAO WA NGUVU,NA HII NDO TIMU AMBAYO ETOO ANATUA LEO HII

Samuel Eto’o anatarajia kutua leo hii na kufanya vipimo kabla ya kumalizia usajili wake na Everton. Imeelezwa mazungumzo na kila kitu kimeshakamilika ili Eto’o atue Everton. Lakini taarifa nyingine zimeeleza, Everton imemtaka Eto’o kupunguza kiwango cha mshara. Mshahara wake akiwa Chelsea msimu uliopita ulikuwa ni pauni 130,000 kwa wiki.