Sunday, August 24, 2014

RAIS KIKWETE ALIVYOJUMUIKA NA MAGWIJI WA REAL MADRID NA TANZANIA BAADA YA KUKABIDHI KOMBE TAIFA JANA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete (kushoto) akimkabidhi Kombe Nahodha wa magwiji wa Real Madrid ya Hispania, baada ya kuwafunga magwiji wa Tanzania mabao 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jioni ya leo.
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na magwiji wa Tanzania
Rais Kikwete akifuatilia mchezo jukwaani
Nahodha wa Real Madrid akiinua juu Kombe lao jana
Rais Kikwete katika picha ya pamoja na magwiji wa Real Madrid
Rais Kikwete akumkabidhi mpira Reuben De La Red baada ya kufunga mabao yote ya Real Madrid

Credit bin zubery

KAMA UNAHISI USHAWAHI KUONA VIDEO CHAFU, BASI HUJAWAHI KUKUTANA NA HII.

zingekuwa zinatengenezwa hapa kwetu tzee, ungekuta serikali imeshazifungia, hii ni kutokana na maadili ya kwenye video hiyo, ila hii hapa ni zaidi ya maadili, na kama unahisi ulishawahi kuona video chafu basi kaa hapa uitizame hii mpya kabisa inaitwa “Pombe yangu”, ni video ya muziki kutoka huko nchini Kenya. Hii video imepata hits 12000 ndani ya masaa matatu tu.

ENZI ZA MADISKO YA SHULE: HEHEHE INAKUKUMBUSHA WAPI HII?!!!!

Zilikuwa nouma kweli hasa kwa
masela waliokosa mademu
wakucheza nao!!!

MAMBO YA KOKO BICHI....JAMANI JAMANI TUTACHOMWA VIBAYA HUKO MOTONI

Jamaa waki naniliuu ndani ya
maji!!!!

Saturday, August 23, 2014

FIGO AWAPA RAHA WATANZANIA REAL MADRID IKIIFUMUA TANZANIA MABAO 3-1 MBELE YA JK

MSHAMBULIAJI Reuben de La Red amefunga mabao matatu peke yake, magwiji wa Real Madrid wakiiangusha Tanzania Eleven 3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. De la Red alimfunga bao moja Mwameja Mohamed kipindi cha kwanza na kipindi cha pil akamtungua mara mbili Manyika Peter, wakati bao pekee la Stars, Real walijifunga wenyewe kupitia kwa Roberto Rojas. Rais wa Jamhuri ya Muungani wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alimkabidhi mpira De La Red baada ya mechi kabla ya kuwakabidhi Kombe Real Madird kwa ushindi huo. Katika mchezo huo, ambao wachezaji waliingia na kutoka, Real Madird walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 10, De La Red akimalizia pasi ya Luis Figo. Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia kwa kiungo Christian Karembeu, aliyezuia shambulizi la Tanzania na kuanzisha shambuizi zuri lililozaa matunda, akiuvuka msitu wa wachezaji wa wenyeji kwa umahiri mkubwa. Tanzania Eleven ilisawazisha dakika ya 45 baada ya kona ya Mecky Mexime kuzua kizaa langoni mwa Real na Roberto Rojas akajifunga katika harakati za kuokoa baada ya Kali Ongala kuuparaza kwa kichwa. Kipindi cha pili, De la Red alifunga bao kwa pili kwa penalti dakika ya 81 baada ya yeye mwenyewe kuchezewa rafu na Habib Kondo kwenye eneo la hatari. Awali ya hapo, Figo alimtoka vizuri beki Mecky Mexime na kuingia hadi kwenye eneo la hatari akiwa kwenye nafasi ya kufunga akampasia De La Red ambaye alipiga nje. De la Red alikamilisha hat trick yake dakika ya 88 baada ya kuwazidi maarifa mabeki wa Tanzania Eeleven. Wachezaji wa timu zote mbili wanatarajiwa kula chakula cha usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu baadaye. Na mdadisiblog/festosaimon

HAYA NDO MATOKEO YA EPL KATI YA CHELSEA VS LEICESTER

MSHAMBULIAJI Diego Costa ameendelea kung’ara Chelsea baada ya jioni hii kuiwezesha The Blues kushinda mechi ya pili mfululizo Ligi Kuu ya England kwa kuichapa Leicester City mabao 2-0 Uwanja Stamford Bridge. Costa alifunga bao la kwanza dakika ya 62, kabla ya Eden Hazard kufunga la pili dakika ya 77. Diego Costa alimpisha mkongwe Didier Drogba dakika ya 80 huku akipigiwa makofi wakati anatoka nje. Kikosi cha Chelsea kilikuwa; Courtois, Ivanovic, Cahill, Terry, Azpilicueta, Matic, Fabregas, Oscar/Willian dk70, Hazard, Schurrle/Ramires dk64 na Costa/ Drogba dk80. Leicester City; Schmeichel, De Laet, Konchesky, Morgan, Hammond/Taylor-Fletcher dk73, King, Schlupp, Mahrez/Albrighton dk68, Nugent na Ulloa/Wood dk84. Na mdadisiblog/festosaimon

SAMUEL ETO’O AMTEGA PABAYA MARIO BALOTELLI,

Anakwenda Merseyside? Mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto’o anaweza kujiunga na Liverpool. MCAMEROON, Samuel Eto’o yuko tayari kukamilisha usajili wa ghafla kujiunga na Liverpool. Mario Balotelli aliwasili Merseyside jana kujaribu kukamilisha uhamisho wa paundi milioni 16 kujiunga Anfield, lakini kama dili litashindikana, nafasi yake itachukuliwa na Mcameroon. Inafahamika kuwa mshambuliaji huyo wa zamani wa Chelsea alipimwa afya na Liverpool akiwa mjini Paris jana ijumaa. Eto’o mwenye miaka 33 ambaye anaishi mji mkuu wa Ufaransa, amekubali dili la miezi 12 (mwaka mmoja) kujiunga na Liverpool na anasubiri kupanda ndege kwenda kusaini mkataba. Eto’o aliripotiwa kuvutiwa na Everton kwa siku chache zilizopita, lakini kigezo cha kucheza ligi ya mabingwa kimemfanya aichague Liverpool.Na mdadisiblog/festosaimon

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA UJIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 

ANGEL DI MARIA SASA ANUKIA KABISAAA! MAN UNITED

Aliachwa: Angel Di Maria hakupangwa katika kikosi cha Real Madrid kilichokabiliana na Atletico Madrid jana usiku. CARLO Ancelotti amethibitisha kuwa mchezaji anayewaniwa kwa nguvu zote na Manchester United, Angel Di Maria aliachwa katika kikosi cha jana kwenye mchezo wa marudiano wa Spanish Super Cup dhidi ya mahasimu wake, Atletico Madrid na kupoteza kombe la kwanza msimu huu kwa sababu za kimpira na si vinginevyo. “Aliachwa katika kikosi kwa sababu za kimpira” Alisema Ancelotti alipoulizwa kwanini hajampanga Muargentina huyo hata katika orodha ya wachezaji wa akiba jana uwanja wa Vicente Calderon. Kitendo cha Di Maria kutopangwa jana kinaashiria uhusiano na kocha Ancelotti umefikia hali mbaya na ni sababu tosha kwa Manchester United kumnasa kwa ada inayoaminika kuwa paundi milioni 50. Ancelotti alithibitisha kuwa nyota huyo wa Argentina katika fainali za kombe la Dunia majira ya kiangazi mwaka huu ameomba kuondoka Real Madrid. Mashabiki wa Real Madrid wameiacha klabu katika wasiwasi kwasababu wanamhitaji Di Maria kubakia, lakini Rais Florentino Perez anataka auzwe ili kuweka sawa mahesabu baada ya kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili Toni Kroos na James Rodrgiguez. Madrid walibaki katika utata mkubwa kutokana na mashabiki waliohudhuria Santiago Bernabeu siku ya jumanne kulipuka kwa shangwe wakimshangilia Di Maria baada ya kuingia uwanjani kipindi cha pili akitokea benchi. Ancelotti alithibitisha ijumaa kuwa mchezaji amekataa kusaini mkataba mpya na ameomba kuondoka.Na mdadisiblog/festosaimon

HII NDO RATIBA YA EPL WIKIENDI HII

Simba inatia raha, Phiri amchezea akili Maximo

KOCHA mwenye heshima kubwa ndani ya Simba na ambaye amekabidhiwa jukumu la kuiongoza timu hiyo msimu ujao, Mzambia Patrick Phiri, ametumia Mwanaspoti kuwaambia mashabiki wa timu hiyo kwamba washushe pumzi mambo ni mazuri. Amewasisitiza kwamba wasiwe na wasiwasi kwa vile kila kitu kipo sawa na heshima lazima irudi Msimbazi kwani ratiba ya Ligi Kuu Bara ameshaipata na wala haimsumbui. Katika mazoezi ya jana Ijumaa yaliyofanyika Uwanja wa Chuoni Chukwani, Phiri alisema wachezaji wake wanapokea kwa kiasi kikubwa mafunzo yake na anapenda kuona wanavyomiliki mipira, kukaba na kushambulia. Alichofanya jana ni kuwapunguzia muda wa mazoezi ambayo awali alikuwa akitumia saa nne na sasa anatumia saa tatu ili wapate muda wa kutafsiri mafunzo yake kambini na kutuliza akili. “Nafurahi kwa sababu naona wachezaji wananielewa kila ninachokihitaji, inanipa moyo sana kwamba msimu ujao tutafanya vizuri, nimetumia muda mwingi kuwafundisha jinsi ya kumiliki mipira, kukaba na kushambulia, kesho (leo Jumamosi) watafanya kidogo tu ili mwili ukae sawa tayari kwa mechi ya Jumapili dhidi ya Kilimani City (ya Daraja la Pili Zanzibar),” alisema Phiri. Akizungumzia maandalizi yake ya Ligi Kuu, alisema kuwa ameiona ratiba na mpangilio wake ni mzuri kwani watacheza mechi nyingi nyumbani katika mzunguko wa kwanza ila amesisitiza mechi yenye presha kuwa ni dhidi ya Yanga itakayochezwa Oktoba 12 Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam. “Ratiba imepangwa vizuri, tunatakiwa kushinda mechi zote lakini kwa uelewa wangu katika Ligi hii ya Tanzania mechi ya Yanga ina presha kubwa kwani ina mambo mengi sana hata kabla ya mechi kuchezwa, lakini tutajipanga kuhakikisha tunafanya vizuri,” alisema Phiri. AMCHEZEA AKILI MAXIMO Katika kile ambacho ni kuonekana kumchezea akili kocha wa Yanga, Marcio Maximo, kama wanavyofanya makocha mahiri wa Ulaya, Phiri amedai kukerwa na ujio wa Yanga mjini Unguja. Yanga ilikuwa kambini Pemba lakini leo Jumamosi inatua Unguja na Kesho itacheza na KMKM kwenye Uwanja wa Amani. Phiri amedai hajafurahia Yanga kuamua kucheza mechi hiyo dhidi ya KMKM siku ambayo wao wana mechi katika uwanja huo wa Amani, mechi ya Yanga itaanza saa 10:00 jioni wakati ya Simba itaanza saa 2:30 usiku dhidi ya Kilimani. Phiri aliliambia Mwanaspoti kwenye kambi ya timu hiyo mjini hapa akisema: “Najaribu kuangalia itakuwaje kwani sisi ndio tumeanza kuja hapa na kutoa taarifa kuwa siku ya Jumapili tutakuwa na mechi, iweje Yanga nao wanataka wacheze siku hiyo hiyo? Kama uwanja usingekuwa mmoja hapo sawa, lakini nao wanataka kucheza uwanja ambao tutautumia.Credit mwanaspoti

Habari zingine za michezo BONYA HAPA