Saturday, August 23, 2014
 |
MSHAMBULIAJI Reuben de La Red
amefunga mabao matatu peke
yake, magwiji wa Real Madrid
wakiiangusha Tanzania Eleven
3-1 Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
De la Red alimfunga bao moja
Mwameja Mohamed kipindi cha
kwanza na kipindi cha pil
akamtungua mara mbili Manyika
Peter, wakati bao pekee la Stars,
Real walijifunga wenyewe kupitia
kwa Roberto Rojas.
Rais wa Jamhuri ya Muungani wa
Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete
alimkabidhi mpira De La Red
baada ya mechi kabla ya
kuwakabidhi Kombe Real Madird
kwa ushindi huo.
Katika mchezo huo, ambao
wachezaji waliingia na kutoka,
Real Madird walikuwa wa kwanza
kupata bao dakika ya 10, De La
Red akimalizia pasi ya Luis Figo.
Mpira uliozaa bao hilo, ulianzia
kwa kiungo Christian Karembeu,
aliyezuia shambulizi la Tanzania
na kuanzisha shambuizi zuri
lililozaa matunda, akiuvuka msitu
wa wachezaji wa wenyeji kwa
umahiri mkubwa.
Tanzania Eleven ilisawazisha
dakika ya 45 baada ya kona ya
Mecky Mexime kuzua kizaa
langoni mwa Real na Roberto
Rojas akajifunga katika harakati
za kuokoa baada ya Kali Ongala
kuuparaza kwa kichwa.
Kipindi cha pili, De la Red
alifunga bao kwa pili kwa penalti
dakika ya 81 baada ya yeye
mwenyewe kuchezewa rafu na
Habib Kondo kwenye eneo la
hatari.
Awali ya hapo, Figo alimtoka
vizuri beki Mecky Mexime na
kuingia hadi kwenye eneo la
hatari akiwa kwenye nafasi ya
kufunga akampasia De La Red
ambaye alipiga nje.
De la Red alikamilisha hat trick
yake dakika ya 88 baada ya
kuwazidi maarifa mabeki wa
Tanzania Eeleven.
Wachezaji wa timu zote mbili
wanatarajiwa kula chakula cha
usiku na Mheshimiwa Rais Ikulu
baadaye. Na mdadisiblog/festosaimon |
0 comments:
Post a Comment