Wednesday, August 06, 2014

BAADA YA TIMU YA YANGA KUTOLEWA KWENYE MICHUANO YA CECAFA UNGOZI WA YANGA WATOA KAULI NZITO

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu akiongea na waandishi wa habari leo makao makuu ya klabu ya Yanga, kushoto kwake ni Kocha Mkuu Marcio Maximo na afisa habari Baraka Kizuguto

Uongozi wa klabu ya Young Africans leo umefanya mkutano na waandishi wa habari juu na kusema kilichofanywa na waandaji wa michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kuiondoa timu isishiriki ni cha kushangaza sana na kinadidimiza soka kwa ujumla.

Katibu Mkuu wa Young Africans Bw Beno Njovu amesema walipata barua ya mwaliko wa kushiriki mashindano tarehe 25/7/2014 na kudhibitisha kushiriki michuano hiyo kwa kuandika barua iliyokwenda TFF na kisha wao kuiwasilisha kwa CECAFA. “Baada ya kudhibitisha kushiriki michuano hiyo tuliambiwa na CECAFA tutume orodha ya wachezaji na viongozi ambao watasafiri kuelekea nchini Rwanda kwenye michuano hiyo ili waweze kuandaa tiketi za ndege na sehemu ya malazi kitu ambacho tulitimiza” alisema Beno.

Lakini katika hali ya kushangaza jana tulipokea barua kutoka TFF ikisema CECAFA imetuondoa kwenye mashindano hayo kwa kushindwa kukidhi vigezo na kuiteua timu ya Azam kuchukua nafasi yetu “aliongeza Beno.”

Kanuni za CECAFA zipo wazi kuwa wachezaji wanaopaswa kushiriki michuano hiyo ni lazima wawe na leseni za kucheza mpira kutoka kwa chama husika, jambo ambalo ambalo orodha tuliyowapelekea wachezaji wote wataichezea Yanga msimu huu wa 2014/2015.

Kocha Marcio Maximo alianza maandalizi ya kikosi ambacho kingekwenda kushiriki michuano hiyo ambayo ilipaswa kuanza ijumaa tarehe 8/8/2014 kwa Yanga kufungua dimba la wenyeji timu ya Rayon FC . Kikosi ambacho kocha mkuu alikichagua kwenda kwenye michuano ya Kagame kilikua na jumla ya wachezaji 20, 15 wakiwa kutoka timu ya kikosi cha wakubwa na wachezaji watano wakitoka kikosi cha pili U20 chini ya kocha Leonado Neiva ambaye amekua na wachezaji hao kwa takribani mwezi mmoja.

Lakini walichokiamua CECAFA ni kuiondoa klabu ya Yanga na kuipa nafasi timu nyingine kwa kusema kikosi kilichopelekwa hawakubaliani nacho na hata kocha mkuu Marcio Maximo haendi, hao ndo tulipojua ya kuwa wanataka majina ya watu na sio timu.

Zifuatazo ni sababu za Kiufundi ambazo Yanga ilizipelekea CECAFA kuhusu kikosi hicho kutojumuisha wachezaji wa timu za Taifa.

a) Ripoti ya kocha aliyeondoka Yanga msimu uliopita Hans ilitoa maelekezo ya kupunguza wachezaji tisa (9) na wachezaji wawili kujiunga na klabu ya Azam hivyo kufanya kikosi kupungua wachezaji 11 kutoka katika idadi ya wachezaji 30 wa msimu uliopita.

b) Wachezaji 10 wa Yanga wamekuwa na majukumu ya timu za Taifa za Tanzania (Taifa Stars), Rwanda na Uganda tangu Aprili 19, 2014 mpaka mwanzoni mwa Agosti, takribani miezi mitatu wamekuwa kambini bila kupata muda wa kupumzika.

c) Benchi la Ufundi la Yanga ni jipya kuanzia kocha mkuu Maximo na wasaidizi wake watatu Leonardo Neiva, Salavatory Edwarda na Shadrack Nsajigwa hivyo wanahitaji muda wa kuwajua wachezaji waliokuwa kwenye timu ya Taifa ndo maana hawakuwajumuisha kwenye kikosi cha kwenda Kigali Rwanda.

d) Baadhi ya wachezaji wanahitaji Vibali vya kufanyia kazi nchini, uhamisho wa Kimataifa (ITC) ili waweza kushiriki michuano ya Kagame, na moja ya kanuni za CECAFA mchezaji anayeshiriki mashindano hayo ni lazima awe na leseni ya kucheza mpira kwa ligi ya ndani.

e) Katika wachezaji 20 waliochaguliwa kushiriki michuano ya Kagame, wachezaji 6 wamepandishwa moja moja katika kikosi cha wakubwa msimu huu hivyo kufanya idadi ya wachezaji wa U20 kuwa watano tu.

f) Wachezaji walikokuwa kambini Taifa Stars kwa takribani miezi mitatu bila ya kupumzika, daktari alipendekeza wapate japo siku kumi na nne (14) za kupumzika ili miili yao iweze kupoa na kuanza upya tena maandalizi ya msimu mpya.

g) Yangga tunaamini hakuna mtu yoyote zaidi ya Kocha Mkuu anayeweza kutupangia kikosi cha kwanza, sababu yeye ndio anayekaa na wachezaji mda wote na kujua ubora wa wachezaji wake.

Chanzo: Tovuti ya Yanga sc

Habari zingine zipo hapa  BONYEZA HAPA 

TIMU YA SIMBA YA ENDELEZA USAJILI WAO KWA KUMSAJILI MCHEZAJI WA COASTAL UNION

Aliyekuwa beki wa zamani wa Coastal Union, Abdi Banda (kushoto) amesaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Simba sc

WEKUNDU wa Msimbazi wamefanikiwa kumsajili beki wa kushoto wa Coastal Union Abdi Banda baada ya kumuweka kwenye rada zake kwa muda mrefu. Nyota huyo kinda mwenye uwezo wa kucheza nafasi zote za ulinzi, lakini beki ya kushoto ndio mahala pake haswaa , alisaini mkataba wa miaka mitatu jana na mara moja atajiunga na kikosi cha Simba kinachofanya mazoezi chini ya kocha mkuu, Mcroatia, Zdravko Logarusic.

 BONYEZA HAPA KWA HABARI NYINGINE ZA KUSISIMUA 

PICHA:AJALI MBAYA YAUA ABIRIA;IHANDA MBOZI!

Picha ya gari aina ya Coaster Likiwa lime halibiwa vibaya Mashuhuda wa Ajali hiyo wamesema kuwa chanzo cha Ajali hiyo ni Dereva wa Gari kubwa aliye kua amehama Njia na Kuhuamia Upande Usio wake.

Jambo lililo mpoteza Uelekeo Dereva wa Coaster na Hatimaye Kupata Ajali hiyo,Amabyo Taarifa za Awali Zilithibitisha kuwa hakuna abiria aliye Fariki eneo la tukio lakini kuna Taarifa Mpya kuwa walio kuwa Majeruhi Wame anza kufariki walipo Pelekwa Kwenye vituo Vya Afya kupewa Huduma.

Picha Na Maelezo:Asante Andrew Senka

 BONYEZA HAPA KUSOMA HABARI NYINGINE 

Hiki ndicho alichojibu Davido kuhusu beef yake na Wiz Kid.

Kwenye internet kulikuwa na tetesi kuhusu Wasanii wa Nigeria Wiz Kid na Davido kuwa na beef ambayo ilichangiwa sana na post za wasanii hawa kwenye social media zikionyesha kama kila mtu anajaribu kumpiga kijembe mwenzake japokuwa hakuna aliyewahi kumtaja mwenzake moja kwa moja.

Davido akiwa kwenye tour zake anazofanya Marekani amekutana na Sahara TV ambao wamemuuliza kuhusu hilo beeef kati yao na kujibu hivi >>> ‘sio beef, niko nae poa na ni shabiki wake… na nilikua nae kwenye ndege moja wakati nakuja Marekani’

Kama bado ujajiunga nasi ili kila tukipata habari zikufikie kirahisi punde niziwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

HII NDO KALI YA MWAKA SIKILIZA MWALIMU MKUU ALIVOWAHAMRISHA WANAFUNZI WA MZOMEE MZAZI WA MWANAFUNZI WA SHULE HIYOO

Si hali ya kawaida kwa Mwalimu Mkuu kuwaamrisha wanafunzi kuzomea mtu na haswa mama wa mtoto ambaye pia anasoma shule hiyo hiyo,idara ya Hekaheka ina stori jinsi Mwalimu Mkuu alivyowaambia wanafunzi kumzomea mama huyo.

Hapa kaongea mama aliyezomewa,mtoto wake pia pamoja na Mwalimu ambaye alipigiwa simu ingawa ushirikiano wake haukuwa mzuri

Bonyeza play kusikiliza  PLAY HAPA 

Source millardayo

JE WAJUA DIAMOND PLUTNUMZ KAPANIA KUFANYA NINI TAREHE 14 SEPTEMBER?KISA HIKI APA

DIAMOND ASEMA HIVI >>>" LONDON!!!!!! you Better be ready for this one!... @AfricaUnplugged Sep14th O2 Academy Brixton.. I said O2 ACADEMY BRIXTON!!!!... [ Honestly Nimebahatika kufanya show nyingi sana Uk, lakini kiukweli show hii nimeipania sana.

Nia na Lengo langu kubwa ni kuuonesha Ulimwengu kuwa ni kias gani East Africa tumejaaliwa uwezo kwenye sanaa ya Muziki...Tafadhari kama ni mkazi wa UK ama una ndugu ama jamaa neishi UK, naomba umfikishie ujumbe huu ili kwa pamoja tareh 14/09/2014 tujumuike pale O2 Academy na kushuhudia burudani nzuri toka kwa mtoto wenu @diamondplatnumz akiwa na Rafiki zake toka # NIGERIA" KAA MKAO WA KULA BURUDANI TOKA KWA CHIBU DANGOTE

 KWA MENGINE MENGI GUSA LINK HII 

HII KALI: Liverpool yazidi kumwaga pesa kwenye usajili

LIVERPOOL, ENGLAND

LIVERPOOL! Achana na moto wao. Wamepania kweli kweli mwaka huu. Imetumia pesa nyingi na sasa inataka matumizi hayo yavuke Pauni 100 milioni.

Baada ya kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu uliopita, lakini ikifanikiwa kufuzu kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya, sasa imekuwa bize kwenye kukisuka kikosi chake na kumwaga pesa kama njugu kuhakikisha hilo linatimia.

Baada ya kuwanasa wachezaji sita hadi sasa, miamba hao wa Anfield wamemtuma Mkurugenzi wao, Ian Ayre, kwenda kumaliza dili za kuwanasa wakali wawili; Alberto Moreno na Javi Manquillo, kitendo kitakachowafanya kutimiza Pauni 100 milioni katika matumizi ya usajili kwa mwaka huu pekee.

Imeelezwa kwamba Liverpool imekubali kutoa Pauni 20 milioni kumsajili Moreno anayechezea Sevilla na ikijadili mkopo wa kumchukua beki wa kulia wa Atletico Madrid, Manquillo, lakini mkataba wake ukiwa na kipengele cha kulipa Pauni 6 milioni kama watavutiwa naye na kutaka kumbeba kwa jumla.

Hadi sasa Liverpool imetumia pesa nyingi kwenye usajili. Imemnasa Rickie Lambert kwa Pauni 4 milioni kutoka Southampton kabla ya kuivamia tena klabu hiyo na kumnasa Adam Lallana kwa Pauni 25 milioni.

Kisha ilitumia Pauni 10 milioni kumnasa staa wa Bayer Leverkusen, Emre Can kabla ya kwenda na Pauni 20 milioni za kumnasa Lazar Markovic kutoka Benfica.

Wakati mashabiki wa timu hiyo wakidhani kwamba Liverpool itakuwa imefunga kazi, kocha Brendan Rodgers alifungua tena pochi lake na kutoa Pauni 20 milioni kumnasa Dejan Lovren kutoka Southampton.

Fowadi mwenye asili ya Kenya, Divock Origi, ametua Liverpool kwa Pauni 10 milioni kutoka Lille, lakini mchezaji huyo aliyeamua kuchukua uraia wa Ubelgiji atabaki kwa mkopo kwenye klabu yake hiyo ya Ufaransa hadi mwakani.

Hadi sasa, Liverpool imetumia karibu Pauni 90 milioni kwa nyota hao Lallana, Lambert, Lovren, Emre Can, Markovic na Origi huku ikiwa imeuza mchezaji mmoja tu, Luis Suarez, kwa Pauni 75 milioni.

Kama bado ujajiunga nasi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi punde niziwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

Audio: Nuh Mziwanda afunguka mazito kuhusu mstakabali wa yeye na shilole na tatoo alizojichora

Stori ya Nuh Mziwanda kujichora tatoo yenye jina la Shilole ilisambaa sana na wengi walikua wakijiuliza siku ikitokea wameachana itakuaje hasa upande wa Nuh ambaye ndiye aliyejichora tatoo hiyo.

Maelezo ya Nuh Mziwanda yamedai kuwa sababu zilizosababisha waachane ni msg
ambayo aliikuta kwenye simu ya Shilole ambayo inasemekana ilitumwa na mwanaume,Nuh alipomwambia Shilole apige
alionekana kunikanyanga.

Nuh Mziwanda kaongea na Soudy Brown kwenye You heard na kazungumza mambo mengi ambayo yametokea kwenye uhusiano wao.
Bonyeza play kusikiliza  PLAY HAPA 
Source clouds fm

Kama bado ujajiunga nasi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi punde niziwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

Semzaba: Niliandika Ngoswe nikiwa kidato cha pili

napotaja majina kumi ya waandishi mahiri wa vitabu nchini, jina la Edwin Semzaba haliwezi kukosekana.

Huyu ni mwandishi, mwigizaji na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ni mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Vitabu nchini (UWAVITA). Kitabu chake cha Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe, ni miongoni mwa vitabu vilivyompatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kikiwa miongoni mwa vitabu vilivyodumu kwa zaidi ya miongo miwili kama kitabu cha kiada kwa shule za sekondari, kitabu cha Ngoswe kwa kiasi kikubwa kimekuwa na mchango katika kujenga fasihi ya Mtanzania.

Mwandishi wetu Maimuna Kubegeya alifanya mahojiano naye hivi karibuni kuhusu maisha yake kama mtunzi na msanii.

Swali: Ni lini hasa ulinza kazi ya uandishi na nini hasa kilikuvutia kuingia kwenye tasnia hiyo?
Semzaba: Nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana kusoma vitabu. Hii ilitokana na ukweli kuwa baba na mama yangu walikuwa walimu hivyo, nyumbani kwetu kulikuwa na vitabu vingi vya hadithi. Jambo hili lilichangia kunihamasisha kupenda kusoma. Hivyo hadi nafika darasa la nne nilijikuta nina uwezo wa kuandika hadithi fupi na mashairi.

Darasa la tano niliweza kuandika barua kwa Kiingereza. Wakati naingia darasa la saba nilikuwa na uwezo mkubwa wa kuandika na kupangilia maneno.

Swali: Unakumbuka ni vitabu gani ulianza kusoma

Semzaba: Hadithi ya Alan Quatermain (Msolopagazi), Mashimo ya Mfalme Suleimani, Alfu Lela Ulela ni miongoni mwa vitabu vya mwanzo nilivyowahi kusoma. Hivi vilikuwa vikitumika shuleni lakini kwa kuwa vilikuwa vikiugusia ujio wa mtu mweupe Afrika baadaye viliondolewa.

Kama bado ujajiunga nasi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi punde niziwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

MSICHANA ALIYEPIGWA NA MTOTO WA RAIS OBAMA ATOAKAULI YA MWAKA.!

Mtoto wa kike wa rais wa  Marekani, Maria Obama mwenye umri wa miaka 16 alimpiga/alimgonga kwa bahati mbaya msichana aliyefahamika kwa jina la Bridget Truskey walipokuwa katika tamasha kubwa la muziki la Lollapalooza nchini Marekani.


Msichana huyo amewashangaza watu baada ya kuonesha kufurahishwa sana na tukio hilo  kutokana na umaarufu wa Malia Obama.

Truskey ametweet sentensi kadhaa kuonesha furaha yake huku maelezo yakionesha kuwa haamini kilichotokea.

“I got (accidentally) kicked by Malia Obama today at Lollapalooza. No lie. Malia. Obama. It was awesome.
#lollapalooza.”

Ni kweli msichana huyo ana sababu ya kufurahi kwa kuwa amekuwa maarufu pia kupitia tukio hilo.

Kama bado ujajiunga nasi ili kila tukipata habari zikufikie kirahisi  BONYEZA HAPA 

Tuesday, August 05, 2014

REAL MADRID YAINASA SAINI YA KIPA SHUJAA WA COSTA RICA KEYLOR NAVAS

MABINGWA wa Ulaya, Real Madrid wamemsajili mlinda mlango na shujaa wa Costa Rica katika fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu nchini Brazil, Keylor Navas.

Navas amekubali kusaini mkataba wa miaka sita na sasa anaingia katika ushindani na kipa Iker Casillas kwasababu kuna dalili kuwa kipa mwingine Diego Lopez anasepa zake.

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao rasmi wa klabu ya Real Madrid jana jioni inasomeka: “Real Madrid CF na Levante UD zimefikia makubaliano juu ya uhamisho wa Keylor Navas, ambaye atajifunga klabuni kwa misimu sita ijayo””Mchezaji atatambulishwa jumanne, Agosti 5, saa 7:00 mchana (saa za Hispania) kwenye uwanja wa Bernabeu, baada ya kuchukuliwa vipimo vya afya”.

Kama bado ujaungana nasi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi BONYEZA HAPA 

HAWA SITA WANAACHWA KATIKA USAJILI WA LOUIS VA GAAL

Louis van Gaal anaweza kuwaacha katika usajili wake wachezaji sita ambao ni Nani, Anderson, Marouane Fellaini, Shinji Kagawa, Javier Hernandez na Wilfried Zaha. Wachezaji hawa wanasubiri maamuzi ya Van Gaal wakati wowote kutoka sasa.

Kama bado ujaungana nasi ili kila tukipata habari zikufikie kirahisi  BONYEZA HAPA 

MANCHESTER CITY KWA VIKOSI HIVI WANA NAFASI YA KUTETEA UBINGWA EPL

Manchester City nawapa nafasi nyingine ya kutetea ubingwa wao – ubora wa kikosi chao ni mkubwa – hivi ni vikosi vyao viwili tofauti ambavyo vinaweza kupambana na timu yoyote na wakapata matokeo! Unadhani timu gani itawasimamisha wasitwae uchampion wa 3 wa EPL

Kama bado ujaungana nasi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi punde tuziwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

Trafiki FEKI Aibua Mazito.....Akutwa na Leseni 40, Radio Call na Pea 7 za Jeshi la Polisi

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, jana imelitolea ufafanuzi sakata la kukamatwa kwa askari 'feki' wa Kikosi cha Usalama Barabarani (trafiki), katika kata ya Chamazi, Mbagala Majimatitu, Wilaya ya Temeke, jijini humo.

Mtuhumiwa huyo, Bw. Robson Emmanuel (30), alikamatwa Agosti 2 mwaka huu, akijifanya Ofisa wa Polisi katika kikosi hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Kamanda wa kanda hiyo, Kamishna Suleiman Kova, alisema mtuhumiwa aliwahi kuwa mwajiriwa wa jeshi hilo kuanzia mwaka 2000 akiwa na namba F2460 lakini alifukuzwa kazi kwa fedheha Machi 3 mwaka 2014, Kibaha, mkoani Pwani akiwa na cheo cha Stesheni Sajenti.

"Katika uchunguzi wetu, tumebaini mtuhumiwa alikuwa akijitambulisha kama askari, hivyo alifanikiwa kuwatapeli wananchi wengi na kujipatia kiasi kikubwa cha fedha kwa njia za udanganyifu," alisema.

Aliongeza kuwa, mtuhumiwa huyo alikamatwa akiwa amevaa sare za jeshi hilo na cheo cha Stesheni Sajenti pia alikutwa na gari aina ya Cresta namba T 723 BAK yenye rangi nyeupe ambayo alilitumia kuzunguka maeneo mbalimbali ya jiji hilo na kutapeli.

"Katika gari hilo, polisi walipekua na kukuta radio call moja yenye namba GP380 aina ya Motorola, leseni za udereva 40, stakabadhi mbili za Serikali zenye namba A0531562 na A1672464, police loss report mbalimbali, kofia, beji, ratiba ya mabasi yaendayo mikoani na vitu vingine mali ya Jeshi la Polisi.

"Pia mtuhumiwa alipekuliwa nyumbani kwake ambapo polisi walikuta sare za jeshi hilo rangi ya kaki pea nne, pea tatu ambazo ni sare za Kikosi cha Usalama Barabarani, koti moja la mvua la kikosi hicho, reflector 8 za kuongozea magari, kofia, mikanda ya jeshi na vyeo vitatu vya Stesheni Sajenti," alisema Kamishna Kova.

Katika hatua nyingine, Kamishna Kova alisema jeshi hilo linawashikilia majambazi wawili kwa tuhuma za kujihusisha na unyang'anyi wa kutumia silaha katika maeneo mbalimbali ya jiji hilo.

Alisema watuhumiwa hao walikamatwa Julai 30 mwaka huu, eneo la Makumbusho Kijitonyama kutokana na msako mkali wa jeshi hilo.

"Watuhumiwa hawa baada ya kupekuliwa majumbani mwao, walikamatwa na bastola mbili, moja aina ya Grock 17 yenye namba B019259 iliyotengenezwa nchini Czech ikiwa na risasi 13 ndani ya magazine, nyingine aina ya Chinese iliyofutwa namba zake ikiwa na risasi moja ndani ya magazine," alisema.

Aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Fredy Steven (25), ambaye ni mfanyabiashara, mkazi wa Kiwalani na Irene Nyange (36), mfanyabiashara na mkazi wa Kijitonyama ambapo uchunguzi unakamilishwa ili watuhumiwa waweze kufikishwa mahakamani wakati wowote.

Kama bado ujaungana nasi ili kila tukipata habari zikufikie punde tuziwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

MSALITI WA UKAWA HUYU HAPA

Wakati wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wa kususia vikao vinavyotarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, mmoja wa wajumbe wake jana aliripoti bungeni na kujiandikisha.

Mjumbe huyo, Clara Mwatuka ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa 6:30 mchana akiwa ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).

CUF ni moja ya vyama vinavyounda Ukawa, pamoja na Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wametangaza kwamba wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki vikao vya Bunge hilo.

Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Bwanausi.

Awali, alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu kuwapo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha bungeni.

AY azungumzia wanachokifanya White House, wanatumbuiza leo (usiku kwa Washington)

Rapper Ambwene Yessaya ambaye yupo jijini Washington DC, Marekani pamoja na wasanii wengine, leo wanatumbuiza mbele ya viongozi mbalimbali wa Marekani na Africa.

Show hiyo inafanyika kwenye ukumbi wa Newseum mjini DC. Hiyo juu  ndio stage ambayo AY na wenzake watatumbuiza “Jana (juzi) ilikuwa ni tour ya kwenda white house na nini, kuelezewa mambo ya mule ndani na baadaye usiku tukafanya rehearsal mpaka usiku wa manane,”

AY aliiambia Bongo5 jana. “Leo (jana) sasa ndo kila kitu, watu tunakutana kwaajili ya kujadili na baada ya hapo tutafanya show leo usiku. Chochote kitakachojadiliwa nitawajuza. Kesho pia ni kuna mkutano mwingine, pia viongozi mbalimbali marais wako hapa wanawasili na mwenyeji mkuu yuko hapa, kesho pia kutakuwa kuna dinner white house,” alisema.

Source bongo 5

Kama bado ujaungana nasi ili kila habari tuzipatapo zikufikie punde tuziwekapo mtandaoni BONYEZA HAPA 

TFF YAANIKA HADHARANI: MUSTAKABALI WA YANGA WA KUSHILIKI AU KUTOSHILIKI KWENYE KOMBE LA KAGAME

Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam BAADA ya Yanga sc kuenguliwa kushiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati , maarufu kama Kombe la Kagame, kwa kugoma kupelekea kikosi cha kwanza kama walivyoagizwa, Shirikisho la soka Tanzania TFF, limesema klabu hiyo ina haki kutoshiriki mashindano kama inaona haijajiandaa.

Afisa habari na mawasiliano wa TFF, Boniface Wambura Mgoyo amezugumza na Mtandao huu mchana huu na kueleza kuwa klabu inapokuwa bingwa, hakuna kanuni inayoibana kwamba lazima ishiriki mashindo fulani, bali kama wanaona hawapo tayari wanaweza kuwasiliana na TFF, halafu klabu nyingine inatafutwa.

“Tunachosema ni kwamba klabu inapokuwa bingwa sio kwamba kuna kanuni zinailazimisha kucheza mashindano.

Kwahiyo ikiona kwamba haijajipanga kwa mashindano, bado ina haki ya kutuandikia sisi kuwa hawapo tayari kushiriki mashindano na tunatafuta timu nyingine inayokwenda kwenye mashindano,” alifafanua Wambura. Hata hivyo, Shirikisho la soka Tanzania limeichagua Azam fc kwenda kushiriki mashindano hayo na tayari limeshawaandikia barua baada ya mawasiliano ya pande zote kwenda barabara.

“Ni kweli , CECAFA waliwapa Yanga muda wa kuthibitisha kikosi chao, lakini muda umekwisha, maana yake sasa CECAFA wamefanya uamuzi wa kuwatoa katika michuano ya Kagame kwa uamuzi wa kupeleka kikosi cha pili au mchanganyiko kinyume na kanuni za mashindano. Na hii ililenga kupunguza hadhi ya mashindano,” alisema Wambura.

“Kwahiyo CECAFA wakaiondoa Yanga na badala yake sisi tukawaomba watupe hiyo nafasi kwa kutafuta timu nyingine ambayo itatuwakilisha kwa maana ya Tanzania bara, tukasema lazima tuwe na uwakilishi kwenye mashindano hayo na tumewapa nafasi Azam.” “Tumeshawaandikia barua baada ya kuzungumza nao na ndio watatuwakilisha kwenye mashindano yanayotarajia kuanza Agosti 8 “Cha msingi cha kuelewa ni kwamba kila mashindano yana kanuni zake na taratibu zake.

Kila mashindano lazima uwe na sifa ya kushiriki, ukishakuwa na sifa, unatakiwa kufuata kanuni kama zinavyoelezeka” Aidha, Wambura alisema TFF hawahusiki kwa lolote kuhusu maamuzi hayo kwasababu wao sio sehemu ya waandaaji wa mashindano.

“Sisi kama TFF hatupo kwenye hayo mashindano na waliohusika kuwatoa Yanga ni waandaji wa mashindano, kwahiyo sisi hatuna lingine la kufanya isipokuwa kuwakumbusha watu kuwa wanapokwenda kucheza mashindano wazingatie kanuni na wasitunge kanuni zao, wanatakiwa kufuata kanuni za waandaaji”

Kama bado ujaungana nasi ili kila tukipata habari zikufikie punde tuziwekapo mtandaoni BONYEZA HAPA 

MANCHESTER CITY WAJIBU HOJA YA MFARANSA ASERNE WENGER

Wanajiamini: Man City hawaamini kama wamevunja sheria ya matumizi ya fedha baada ya kumsajili Lampard kwa mkopo.

MANCHESTER City wanajiamini kuwa hawajavunja sheria ya matumizi ya fedha baada ya kumchukua kwa mkopo Frank James Lampard. Kiungo huyo mwenye miaka 36 alisaini miaka miwili kuitumikia klabu ya New York City-moja ya klabu inayomilikiwa na Manchester City.

Lakini timu hiyo ya Marekani haitacheza ligi mpaka mwezi wa tatu mwakani, kwahiyo Lampard atacheza ligi kuu nchini England kwa mkopo mpaka januari mwakani.

Mkataba mpya: Kiungo huyu alijiunga na New York FC kwa mkatana wa miaka miwili baada ya kuachiwa na Chelsea. Kocha wa Asernal, Mfaransa Aserne Wenger aliibua wasiwasi mwishoni mwa wiki alipohoji kama mkataba wa mkopo wa Lampard upo sahihi na umeendana na sheria ya matumizi ya fedha (FFP) ambayo inaitaka klabu kutotumia fedha nyingi kuliko mapato yake.

Man City walishindwa kufuata sheria ya UEFA ya matumizi ya fedha msimu uliopita na sasa wanatakiwa kujumuisha wachezaji watano wazawa katika kikosi cha wachezaji 21 kitakachoshiriki UEFA msimu ujao ampao Lampard atakuwa miongoni mwao.
Hata hivyo, City ambao wanakaribia kuvunja tena sheria mwaka huu, wanaamini kwamba hawajavunja sheria ya matumizi ya fedha ya UEFA baada ya kumsajili Lampard.

Sheria za UEFA zinaelezea kuwa mkataba wa mkopo wa Lampard unaingia katika sheria ya matumizi ya fedha kwasababu Man city watakuwa wanamlipa posho kiungo huyo wa zamani wa Chelsea.

Arsene Wenger ameibuka wasiwasi kuhusiana na dili la Lampard

Kama bado ujajiunga nasi ili  habari zikufikie kirahisi  punde tuwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

HII MPYA KABISA!: YANGA SC HAWATASHIRIKI KOMBE LA KAGAME 2014, WAGOMA KUBADILI KIKOSI

Na festo saimon TAARIFA Mpya asubuhi hii! Yanga hawatashiriki michuano ya klabu bingwa kwa ukanda wa Afrika mashariki na kati, maarufu kwa jina la Kombe la Kagame inayotarajia kuanza kutimua vumbi Agosi 8 mwaka huu,, mjini Kigali, Rwanda.

Hii imetokana na Yanga kugoma kubadili kikosi chao kama walivyotakiwa na CECAFA leo hii. Taarifa zinaeleza kuwa Yanga wamekomaa na kikosi B kama walivyopanga wakati CECAFA wamewataka kwenda na kikosi B. Awali ilielezwa kuwa Yanga wanatakiwa kubadilisha kikosi hicho kufikia alfajiri ya kesho na kama haitafanya hivyo, basi timu itatolewa kwenye mashindo.

Kwa mana hiyo, mabingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara, Azam fc wanaweza kupewa nafasi hiyo kama ilivyoelezwa awali.

Kama bado ujajiunga nami ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi BONYEZA HAPA