Tuesday, August 05, 2014

MANCHESTER CITY WAJIBU HOJA YA MFARANSA ASERNE WENGER

Wanajiamini: Man City hawaamini kama wamevunja sheria ya matumizi ya fedha baada ya kumsajili Lampard kwa mkopo.

MANCHESTER City wanajiamini kuwa hawajavunja sheria ya matumizi ya fedha baada ya kumchukua kwa mkopo Frank James Lampard. Kiungo huyo mwenye miaka 36 alisaini miaka miwili kuitumikia klabu ya New York City-moja ya klabu inayomilikiwa na Manchester City.

Lakini timu hiyo ya Marekani haitacheza ligi mpaka mwezi wa tatu mwakani, kwahiyo Lampard atacheza ligi kuu nchini England kwa mkopo mpaka januari mwakani.

Mkataba mpya: Kiungo huyu alijiunga na New York FC kwa mkatana wa miaka miwili baada ya kuachiwa na Chelsea. Kocha wa Asernal, Mfaransa Aserne Wenger aliibua wasiwasi mwishoni mwa wiki alipohoji kama mkataba wa mkopo wa Lampard upo sahihi na umeendana na sheria ya matumizi ya fedha (FFP) ambayo inaitaka klabu kutotumia fedha nyingi kuliko mapato yake.

Man City walishindwa kufuata sheria ya UEFA ya matumizi ya fedha msimu uliopita na sasa wanatakiwa kujumuisha wachezaji watano wazawa katika kikosi cha wachezaji 21 kitakachoshiriki UEFA msimu ujao ampao Lampard atakuwa miongoni mwao.
Hata hivyo, City ambao wanakaribia kuvunja tena sheria mwaka huu, wanaamini kwamba hawajavunja sheria ya matumizi ya fedha ya UEFA baada ya kumsajili Lampard.

Sheria za UEFA zinaelezea kuwa mkataba wa mkopo wa Lampard unaingia katika sheria ya matumizi ya fedha kwasababu Man city watakuwa wanamlipa posho kiungo huyo wa zamani wa Chelsea.

Arsene Wenger ameibuka wasiwasi kuhusiana na dili la Lampard

Kama bado ujajiunga nasi ili  habari zikufikie kirahisi  punde tuwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

0 comments:

Post a Comment