Wednesday, August 06, 2014

Semzaba: Niliandika Ngoswe nikiwa kidato cha pili

napotaja majina kumi ya waandishi mahiri wa vitabu nchini, jina la Edwin Semzaba haliwezi kukosekana.

Huyu ni mwandishi, mwigizaji na mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Pia ni mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Vitabu nchini (UWAVITA). Kitabu chake cha Ngoswe Penzi Kitovu cha Uzembe, ni miongoni mwa vitabu vilivyompatia umaarufu mkubwa ndani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Kikiwa miongoni mwa vitabu vilivyodumu kwa zaidi ya miongo miwili kama kitabu cha kiada kwa shule za sekondari, kitabu cha Ngoswe kwa kiasi kikubwa kimekuwa na mchango katika kujenga fasihi ya Mtanzania.

Mwandishi wetu Maimuna Kubegeya alifanya mahojiano naye hivi karibuni kuhusu maisha yake kama mtunzi na msanii.

Swali: Ni lini hasa ulinza kazi ya uandishi na nini hasa kilikuvutia kuingia kwenye tasnia hiyo?
Semzaba: Nikiwa mdogo nilikuwa napenda sana kusoma vitabu. Hii ilitokana na ukweli kuwa baba na mama yangu walikuwa walimu hivyo, nyumbani kwetu kulikuwa na vitabu vingi vya hadithi. Jambo hili lilichangia kunihamasisha kupenda kusoma. Hivyo hadi nafika darasa la nne nilijikuta nina uwezo wa kuandika hadithi fupi na mashairi.

Darasa la tano niliweza kuandika barua kwa Kiingereza. Wakati naingia darasa la saba nilikuwa na uwezo mkubwa wa kuandika na kupangilia maneno.

Swali: Unakumbuka ni vitabu gani ulianza kusoma

Semzaba: Hadithi ya Alan Quatermain (Msolopagazi), Mashimo ya Mfalme Suleimani, Alfu Lela Ulela ni miongoni mwa vitabu vya mwanzo nilivyowahi kusoma. Hivi vilikuwa vikitumika shuleni lakini kwa kuwa vilikuwa vikiugusia ujio wa mtu mweupe Afrika baadaye viliondolewa.

Kama bado ujajiunga nasi ili kila nikipata habari zikufikie kirahisi punde niziwekapo mtandaoni  BONYEZA HAPA 

0 comments:

Post a Comment