Monday, August 25, 2014

Maximo aizuga vibaya timu ya Simba

YANGA walikuwa kambini mjini Pemba lakini juzi Jumamosi wakatua Unguja na jana Jumapili wakakipiga na Shanghani mchana kwenye mechi ya kirafiki katika Uwanja wa Amani. Ujio wa Yanga Unguja kiufundi ni faida pia kwa Simba ambayo imeweka kambi yake eneo la Mbweni ikifanya mazoezi Uwanja wa Chuoni. Yanga itapata nafasi ya kuisoma Simba kwenye mechi zake za kirafiki mpaka mazoezini na Simba nao hivyohivyo. Lakini Kocha Marcio Maximo ameshitukia hali hiyo na kutamka kwamba anafanya mambo yake kwa akili sana na hakuna timu yoyote itaweza kusoma mbinu zake kwani hatazitumia hadharani kwa muda wote atakaokuwa Unguja. Kocha huyo ambaye timu yake ina wachezaji wawili raia wa Brazil, alisema kwamba anafanya mambo kwa umakini sana na hata mbinu zake za maangamizi atawapa wachezaji katika mazingira ya siri. Anamaanisha kwamba hata Simba au Azam wakiangalia mechi yake yoyote ya kirafiki kwa sasa haitawasaidia. “Unajua tunakwenda kwenye ushindani kucheza ligi, kila mtu anataka kujua una mbinu gani hivyo suala hilo niko makini nalo sana, sitaki watu wagundue mbinu zangu, ”alisema Maximo ambaye bado hajatangaza kumuacha mchezaji wake ghali wa kigeni, Mganda Emmanuel Okwi licha ya kuchelewa. Keshokutwa Jumatano, Yanga itacheza mechi nyingine ya kirafiki dhidi ya Shangani na baada ya hapo, watarudi Dar es Salaam kucheza mechi mbili ngumu. Yanga awali ilicheza na Chipukizi na Shanghani. Katika hatua nyingine, Mbrazili Andrey Coutinho amewavutia zaidi mashabiki wa Pemba. Kocha Mkuu wa Chipukizi ya Pemba iliyofungwa na Yanga bao 1-0, amesema yeye ni Coutinho tu kwenye kikosi hicho na kilichomvutia zaidi ni namna anavyotumia akili kupenya sehemu ngumu. Coutinho anachezesha timu vizuri, pasi zake zenye macho zilimfanya Mbrazili mwenzake, Genilson Santos Santana ‘Jaja’ ang’ae kwenye mechi yao na Chipukizi ya Pemba. Mchezaji huyo mwenye mwili mdogo, ana kasi na alishirikiana vizuri na Mrisho Ngassa, Mnyarwanda Haruna Niyonzima katika kuchezesha timu. Kwenye Uwanja wa Gombani, kila alipokuwa akiunasa mpira zilisikika kelele za mashabiki zikimshangilia. Credit mwanaspoti

HII NDO TOFAUTI NA BAADHI YA WATU WANAVYO MCHUKULIA ….LULU

"Pepo ipo miguuni mwa mama yako....usifanye mchezo na mama. Hata wakifika followers wengi kama wa Beyoncé. Mama ni mama. Haina ubishi wala usupa star. Nimefurahi kumkuta @officiallulumichael akiwa anampaka mama yake mafuta na kumvalisha viatu. Mwenyezi mungu akuongezee dogo. Kesho massage" ….by @glammadam INSTAGRAM

New AUDIO | BenPol - Twapendana | Download hapA

<<<<<<<<< BONYEZA HAPA KUDOWNLOAD >>>>>>>>>

PAKA JEUSI LAKATIZA UWANJANI CAMP NOU, BARCA YAUA 3-0 LA LIGA

BARCELONA imeanza vyema La Liga kufuatia ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Elche Uwanja wa Camp Npu usiku wa kuamkia leo. Katika mchezo huo, kiungo wa Barca Javier Mascherano alitolewa nje kwa kadi nyekundu kipindi cha kwanza, kocha mpya Luis Enrique akiiongoza timu kwa mara ya kwanza, alionyesha mwanzo mzuri. Lionel Messi aliifungia Barca bao la kwanza baada ya kuwazidi ujanja mabeki sita Elche, kabla ya kinda Munir El Hadaddi kufunga la pili, mabao yote kipindi cha kwanza. Nyota wa Argentina, Lionel Messi alifunga bao lake la pili na la tatu la kuhitimisha ushindi wa Barca baada ya jitihada binafsi kipindi cha pili. Paka mweusi alikatiza Uwanja wa Camp Nou mwanzoni tu mwa mchezo na kusababisha mechi isimame kwa muda ili aondoke.

JUX AKANUSHA TUHUMA ZILIZOSAMBAA MTANDAONI KUWA ANATOKA NA VANESSA

Jux amekanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi na msanii mwenzake Vanessa Mdee na kudai kuwa Vanessa ni mshikaji wake tu lakini amekiri kuwa muimbaji huyo wa ‘Come Over’ ana kila sifa ya kuwa mke. Jux ambaye hivi karibuni alionekana kuwa karibu na Vanessa amesema Vanessa ni mtu wake wa karibu anayefanya kazi naye. “No ni mshikhaji wangu tu, tunafanya naye kazi, kuna tabia zinaendana, kama ninavyokuwa na rafiki na Stamina, Mo Music ni kawaida, sema unajua ni mwanamke na ni njia toafuti ndio maana imekuwa hivyo,” alisema Jux. Alipoulizwa kama Vanessa anafaa kuwa wife material Jux alijibu Vanessa ana kila sifa ya kuwa mke. “Ni msichana mzuri, mwonekano wake mzuri, she is smart, yeah she is a wife material, yuko vizuri, lakini na mimi tumeendana sana tabia zetu kama washikaji. Sema nipo naye karibu na kwa sababu mimi sionekanagi na wasichana wengi ndio maana imekuwa hivyo. Lakini sijui labda baadaye kwa sasa hivi ni mapema, vyote anapanga Mungu,” alisisitiza Jux.

Source bongo5

TETESI ZA SOKA ZILIZOSHAMILI KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA ULAYA LEO JUMATATU ZIPO HAPA

Manchester City wameacha kumfuatilia kiungo wa Everton Ross Barkley, 20, baada ya kuambiwa atagharimu pauni zisizopungua milioni 50 (Mirror), Manchester United wanakaribia kumsajili winga wa Real Madrid Angel Di Maria, 26, na huenda atavunja rekodi ya uhamisho ya Uingereza kwa mkataba wa pauni milioni 56 (Sky sports), Manchester United pia wamepanda dau kwa mara ya pili kumwania kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27, katika mkataba utakaohusisha Man U kutoa na mchezaji (Star), Mario Balotelli, 24, huenda akawa mchezaji kamili wa Liverpool katika mkataba wa pauni milioni 16 ifikapo Jumatatu, lakini Liverpool wameacha kumfuatilia mshambuliaji wa zamani wa Chelsea Samuel Eto'o, 33, (Liverpool Echo), Eto'o anadhaniwa kudai mshahara wa pauni 100,000 kwa wiki kutoka kwa Liverpool, lakini sasa inaripotiwa kuwa anafanya mazungumzo na Everton ingawa kuna timu za Mashariki ya Kati pia zinamtaka (Mirror), Balotelli hatosaini mkataba wenye kipengele cha utovu wa nidhamu. Mwakilishi wa mshambuliaji huyo Mino Raiola amedai kuwa mkataba huo hauna tofauti na mikataba yoyote ya Liverpool na kuwa makubaliano yatafikiwa kabla ya Jumanne (Express), Arsenal wanafikiria kumchukua Toby Alderweireld, 25, kutoka Atlètico Madrid kuziba nafasi ya Thomas Vermaelen aliyekwenda Barcelona (Star), Gunners pia wanamfuatilia beki wa Olympiakos Kostas Manolas, 23, ambaye alichezea Ugiriki katika Kombe la Dunia na ambaye anatazamwa pia na Man U (Express), kipa wa Chelsea Petr Cech, 33, anajiandaa kuondoka Darajani baada ya nafasi yake kuchukuliwa na Thibault Courtois (Mail on Sunday), Lukas Podolski anajiandaa kuondoka Arsenal na kwenda Juventus kwa mkopo (Sunday Express), Arsene Wenger alimkataa mara mbili Mario Balotelli anayekwenda Liverpool. Balotelli angeweza kwenda Emirates kama Wenger angemtaka (Metro), Valencia wanataka kumsajili Alvaro Negredo kutoka Manchester City kabla ya dirisha la usajili halijafungwa, pia wanawafuatilia Fernando Llorente na Anthony Martial (Superdeporte). Zimesalia siku nane kabla ya dirisha la usajili kufungwa. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Credit salim kikeke