BARCELONA imeanza vyema La
Liga kufuatia ushindi wa mabao
3-0 dhidi ya Elche Uwanja wa
Camp Npu usiku wa kuamkia leo.
Katika mchezo huo, kiungo wa
Barca Javier Mascherano
alitolewa nje kwa kadi nyekundu
kipindi cha kwanza, kocha mpya
Luis Enrique akiiongoza timu kwa
mara ya kwanza, alionyesha
mwanzo mzuri.
Lionel Messi aliifungia Barca bao
la kwanza baada ya kuwazidi
ujanja mabeki sita Elche, kabla
ya kinda Munir El Hadaddi
kufunga la pili, mabao yote
kipindi cha kwanza.
Nyota wa Argentina, Lionel Messi
alifunga bao lake la pili na la tatu
la kuhitimisha ushindi wa Barca
baada ya jitihada binafsi kipindi
cha pili.
Paka mweusi alikatiza Uwanja wa
Camp Nou mwanzoni tu mwa
mchezo na kusababisha mechi
isimame kwa muda ili aondoke. |
0 comments:
Post a Comment