Saturday, August 23, 2014

CHEKI CHELSEA WANAVYOJIFUA KUIWINDA LEICESTER CITY LEO

KATIKA MECHI YA KWANZA YA LIGI KUU ENGLAND, CHELSEA ILIANZA KWA KUITWANGA BURNLEY 3-1; SASA INAJIWINDA DHIDI YA LEICESTER LEO JUMAMOSI NA KWA KOCHA JOSE MOURINHO ATAKUWA ANAKUTANA NAYO KWA MARA YA KWANZA

RASMI, BALOTELLI ATUA LIVERPOOL, MASHABIKI WAJAZANA KUMSHUHUDIA

MSHAMBULIAJI WA ZAMANI WA MAN CITY ALIYEKUWA AKIKIPIGA AC MILAN, MARIO BALOTELLI AMEFUZU VIPIMO NA SASA UNAWEZA KUSEMA NI MCHEZAJI WA LIVERPOOL. MASHABIKI WAMEJITOKEZA KWA WINGI KUMLAKI INGAWA HATACHEZA MECHI DHIDI YA MAN CITY, JUMATATU USIKU. MSHAHARA WAKE KWA WIKI UTAKUWA NI PAUNI 125,000.

ULEVI MBAYA, ANGALIA UNAVYOMMALIZA SHUJAA WA ENGLAND, SURA IMEKUWA KA' KINYAGO

GAZZA (KULIA) WAKATI AKIWA FITI ANAITUMIKIA ENGLAND.
AKICHUKULIWA NA POLISI BAADA YA KUKUTWA AMELALA NJE YA NYUMBANI KWAKE KUTOKANA NA KUZIDIWA NA KILEVI. MARA KADHAA AMEKUWA AKITIBIWA LAKINI GAZZA AMESHINDWA KUJIONDOA KWENYE ULEVI KUPINDUKIA. ALIKUWA NYOTA WA TIMU YA TAIFA YA ENGLAND, LAKINI ULEVI KUPINDUKIA UNAMTAFUNA

ANGALIA TANZANIA ELEVEN WANAVYOPIGA BATA NDANI YA SAPPHIRE COURT KABLA YA KUIVAA MADRID LEO

NSAJIGWA, NYENGE NA MASATU.
KIKOSI CHA TANZANIA ELEVEN WAKIJIACHIA KWA MISOSI YA NGUVU KWA MGAHAWA WA HOTELI YA SAPPHIRE COURT YA JIJINI DAR ES SALAAM AMBAKO WAMEWEKA KAMBI KUJIWINDA DHIDI YA WAKONGWE WA REAL MADRID AMBAO WATAWAVAA LEO KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR KATIKA MECHI YA KIRAFIKI INAYOSUBIRIWA KWA HAMU KUBWA NA MASHABIKI
LUNYAMILA NA ATHUMANI CHINA.
IDDI MOSHI MNYAMWEZI NA MAXIME.
CHINA

Credit salley ally

Haya ndo matokeo ya mechi kati ya ATLETICO MADRID VS REALMADRID, super cup

Wakati wakongwe wao wakitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki leo jijini Dar es Salaam, Real Madrid imeshindwa kuonyesha kuwa wanaweza baada ya kuchapwa bao 1-0 na wapinzani wao wakubwa Atletico Madrid. Kipigo hicho cha bao 1-0 katika mechi ya pili ya Super Cup, maana yake Atletico wameibuka mabingwa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya 1-1 katika mechi ya kwanza ndani ya Camp Nou. Muuaji wa jana alikuwa na Mario Mandzukic ambaye amejiunga na Atletico akitokea Bayern Munich ambaye alifunga bao hilo katika dakika ya 2 tu. Pamoja na juhudi za Kocha Carlo Ancelotti kumuingiza Cristiano Ronaldo katika kipindi cha pili, bado Madrid haikuweza kupindua matokeo. Kiungo Luca Modric alilambwa kadi mbili za njano na kuwa nyekundu. NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

MSAFARA WA MWISHO WA REAL MADRID ULIVYOTUA DAR, LEO TAIFA PATAPENDEZA

Magwiji wa Real wakisubiri usafiri kuelekea Bahari Beach
Watu walijitokeza kuwapokea
Wanaelekea kwenye basi la Azam FC kwa safari ya hotelini
Msafara wa mwisho wa Real Madrid baada ya kuwasili Dar es Salaam jana jioni tayari kwa mchezo wa leo dhidi ya magwiji wa Tanzania Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Friday, August 22, 2014

KARIBU TANGA: MAHABA NAMNA HII KWANINI MTU UCHEPUKE?!!!!....HAPO NDIO MAANDALIZI YA FOOD...

BALOTELLI ATUA LIVERPOOL KUKAMILISHA USAJILI WAKE

MSHAMBULIAJI Mario Balotelli alitarajiwa kuwasili England leo mchana kwa ajili ya kufikia makubaliano ya kujiunga na Liverpool baada ya klabu hiyo kufikia makubaliano na wawakilishi wake. Mpachika mabao huyo wa zamani wa Manchester City yuko karibu kusaini kikosi cha Brendan Rodgers na amekwenda huko kukamilisha dili hilo mara moja. Baada ya kuwasili, Balotelli alitarajiwa kwenda kufanyiwa vipimo katika hospitali ya klabu hiyo, Spire Liverpool kabla ya kwenda kufanyiwa vipimo zaidi vya afya katika viwanja vya Melwood vinavyotumika kwa mazoezi na klabu hiyo. Pamoja na hayo, mshambuliaji huyo wa Italia hataweza kuichezea Liverpool dhidi ya klabu yake ya zamani, Manchester City Jumatatu usiku, katokana na muda wa usajili kwa leo kupita.NA MDADISIBLOG/FESTOSAIMON

FAHAMU KIWANGO KIPYA ANACHOLIPWA DIAMOND KWA SHOW MOJA YA MZIKI HAPA TANZANIA

Tangu mwaka juzi tulifahamu kuwa Diamond Platinumz ndiye msanii wa Tanzania anaelipwa kiasi kikubwa cha pesa, na mwaka jana ikaelezwa kuwa bila milioni 10 au 8 za Kitanzania humpati kwenye show yako. Lakini kiwango kipya kilichotajwa jana kitawapa kizunguzungu zaidi hasa mapromota wenye mitaji midogo wenye ndoto za kufanya kazi na mwimbaji huyo. Kwa mujibu wa, Babu Tale ambaye ni meneja wake, hivi sasa kiwango cha chini anachochaji kwa show moja hapa nchini ni $15,000 (sawa na shilingi Milioni 25 za Tanzania). “Tuna show Marekani show kumi na tano (15), show kumi na tano dola elfu ngapi? Na kwa hapa Tanzania hatufanyi show chini ya dola e15,000.” Babu Tale aliiambia Bongo5. Kwa mujibu wa Babu Tale, wanachaji kiasi cha hadi dola 25,000 kwa show moja za nje ya nchi (ikiwemo Marekani). “Tunalipwa milioni 20 show moja, tunalipwa dola elfu 25,000 show moja, hii ni zaidi ya madawa ya kulevya.” Alisema wakati akikanusha tuhuma kuwa Diamond anauza dawa za kulevya. Kwa mahesabu ya haraka haraka, shows 15 mara dola 25,000 ni sawa na $375,000 (Sawa na shilingi za Tanzania 625,687,500). Yesss! Ni zaidi ya Milioni mia sita ishirini na tano za kitanzania. Kama ni kweli, basi Diamond anastahili kweli kuitwa Dangote wa Bongo Flava. Bado michongo inaendelea kumiminika ambapo hivi karibuni meneja wa Trey Songz alimtumia ujumbe kuwa atakapokuwa na nafasi amshitue waongee.