Wednesday, August 20, 2014

MAMBO YAIVA ZIARA YA REAL MADRID NCHINI… FIGO, OWEN NA KAREMEBU WATUA KESHO DAR

MWANASOKA bora wa zamani wa dunia, Mreno Luis Filipe Madeira Caeiro Figo anatarajiwa kutua kesho na msafara wa kwanza ya magwiji wa Real Madrid tayari kwa mchezo dhidi ya magwiji wa Tanzania Agosti 23 Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Figo ataongozana na nyota wengine wawili waliowika Real Madrid muongo uliopita, mshambuliaji Michael Owen aliyeshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi Kombe la Dunia mwaka 1998 Ufaransa na mwanasoka bora wa Oceania mara mbili 1995 na 1998 Christian Karembeu. Figo aliyestaafu Mei 31 mwaka 2009, alipiga tuzo mbili mfululizo mwaka 2000, Mwanasoka Bora Ulaya na Dunia na anakuja Tanzania kuwakumbushia watu enzi zake anatamba Real Madrid. Mapokezi makubwa yameandaliwa kwa ajili ya magwiji hao Real Madrid ambao sasa wanakuja kwa awali na hadi Agosti 22 kikosi kizima kitakuwa kimekamilika Dar es Salaam. Mkurugenzi wa makampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), Farough Baghozah ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba magwiji hao watapokewa kwa maandamano Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kupelekwa hoteli ya Ladger Plaza, Bahari Beach. Kikosi cha magwiji wa Tanzania, kitakachomenyana na Real Madrid kinaendelea mazoezi Uwanja wa Karume kwa wiki sasa kwa ajili ya mchezo huo wa kihistoria. Makipa maarufu waliowahi kuwika nchini, Mwameja Mohamed na Manyika Peter wamejumuishwa katika kikosi cha Tanzania All Stars kitakachomenyana na magwiji hao wa Real Madrid. Chini ya makocha Charles Boniface Mkwasa ‘Master’ na Wasaidizi Freddy Felix Minziro na Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, Daktari Mwanandi Mkwankemwa na viongozi Mtemi Ramadhani, Hassan Mnyenye, Omar Gumbo na Hamisi Kisiwa kikosi hicho kitaingia kambini Dar es Salaam kujiandaa kwa mchezo huo wa Agosti 23, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Wengine walioItwa ni mabeki Nsajigwa Shadrack, Mecky Mexime, Boniface Pawasa, John Mwansasu, Abubakar Kombo, George Masatu, Habib Kondo, Viungo Suleiman Matola, Shaaban Ramadhani, Salvatory Edward, Sabri Ramadhani ‘China’, Yussuf Macho, Abdul Mashine, Abdul Maneno, Mao Mkami, Steven Nyenge, Madaraka Suleiman, Akida Makunda na Mtwa Kihwelo. Washambuliaji ni Monja Liseki, Iddi Moshi, Dua Said, Emmanuel Gabriel, Said Maulid, Thomas Kipese, Nasor Mwinyi ‘Bwanga’, Edibilly Lunyamila, Mohamed Hussein ‘Mmachinga’, Clement Kahbuka, Madaraka Suleiman na Akida Makunda. Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Real Madrid watakuja nchini. Katika ziara hiyo, pamoja na kucheza mchezo wa kirafiki na kikosi maalum cha wachezaji nyota wa Tanzania Agosti 23, pia watafanya utalii katika vivutio mbalimbali, ikiwemo kupanda mlima Kilimanjaro. Miongoni mwa nyota wanaotarajiwa kuja na Real nchini ni pamoja na Wanasoka Bora wa zamani wa Dunia, Mfaransa Zinadine Zidane, Mreno Luis Figo na Mbrazil, Ronaldo Lima. Na mdadisiblog,/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII 

Barcelona wameitaja hii ndio bei ya Suarez lakini kuna mambo yanachanganya.

Tunafahamu kwamba Luis Suarez alijiunga na Barcelona mwaka huu wa 2014 akitokea Liverpool aliyoichezea toka mwaka 2011-2014 na kuifungia magoli 69 kwenye mechi 110 alizocheza. Sasa ishu imekuja kwenye ada ya uhamisho kwenda Barca ambapo club hiyo imeweka wazi jana kwamba ilimchukua kwa pounds milioni 65 kutoka Liverpool. Kuna mchanganyiko umetokea baada ya hiyo bei kutajwa kwa sababu Liverpool walisema bei waliyomuuza mng’ataji huyu ni Pound milioni 75.

HII NDIO SABABU YA MIMI KUAMUA KUTAFUTA MKWANJA KWA NGUVU ZOTE ILI SIKUMOJA NIJE KUWAPATA WATOTO KAMA HAWA

BAYERN WALIVUNJA 'PROMISI', WALIMUAMBIA GUARDIOLA KWAMBA, KROOS HATOUZWA

Bayern Munich walivunja ahadi waliyompa Kocha Pep Guardiola kwamba kiungo Toni Kroos hatouzwa. Uongozi wa Bayern ulimuahidi Guardiola ambaye alisisitiza kiungo huyo ni muhimu sana. Lakini mwisho ilishindikana, akauzwa kwa wababe wa Hispania, Real Madrid. Pamoja na kuwa na Xabi Alonso ambaye ni mmoja wa viungo nyota, Madrid imemwaga mamilioni kumtwaa Kroos ambaye tayari ameanza kuonyesha cheche. Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI PUNDE ZITUFIKIAPO 

MWANADADA FUNMI AJIACHIA ILE MBYA SIKU YA BIRTHDAY YAKE…CHEKI PICHA HIZI AKIYAKATA MAYENU…!!!

Jina lake kamili ni Funmi Iyanda , mwandishi na mtangazi wa TV kutoka Nigeria...ana host kipidi cha New Dawn with Funmi. .Aliwahikutajwa na jarida la forbes kama Forbes 20 Youngest Power Women in Africa, 2011…cheki picha hizi akiselebuka na ma friend..kwenye siku yake ya kuzaliwa!!!!

MIZIGO KAMA HII NDIO HUWA INANIFANYA MIMI NISHINDE KUTWA NZIMA HUKO INSTAGRAM

HAYA NDO MATOKEO YA MECHI YA ARSENAL VS BESKITAS,UWANJA WA ATARARK

ARSENAL imejiweka katika mazingira mazuri ya kuvuka hatua ya mchujo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana na wenyeji Beskitas, Uwanja wa Ataturk. The Gunnes walimpoteza nyota wao, Aaron Ramsey aliyeonyeshwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu dakika ya 80 baada ya kucheza rafu. Mkali mpya: Demba Ba (kulia) aliyejiunga na Besiktas kwa Pauni Milioni 4.7 kutoka Chelsea msimu huu leo alikuwa mwiba mbele ya mabeki wa Arsenal Katika mchezo huo, mshambuliaji wa zamani wa Chelsea, Demba Ba alikaribia kuifungia Beskitas dakika ya sita baada ya shuti lake kugonga besela, wakati Alex Oxlade-Chamberlain naye pia alikaribia kuifungia Arsenal alipogongesha mwamba mwishoni. Kocha wa Besiktas, Slaven Bilic pia alipandishwa jukwaani mwishoni mwa mchezo. Mchezo wa marudiano utafanyika Jumatano ijayo Uwanja Emirates. Kikosi cha Besiktas: Tolga, İsmail, Motta, Ersan, Pedro, Olcay/Tore dk72, Veli, Necip, Ozyakup/Frei dk80, Mustafa/Tosun dk88 na Demba Ba. Arsenal: Szczesny, Debuchy, Koscielny, Chambers, Monreal, Arteta/Flamini dk50, Ramsey, Cazorla/Rosicky dk90, Wilshere, Sanchez/Oxlade-Chamberlain dk72 na Giroud. Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI 

Hatimaye Man United wakamilisha usajili mwingine – huyu ndio mchezaji wao mpya

Baada ya usajili wa Ander Herrera na Luke Shaw, klabu ya Manchester United leo hii imekamisha usajili wa mchezaji mwingine. Marcos Rojo, beki wa kiargentina aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Sporting Lisbon amethibitishwa rasmi kujiunga na kikosi cha Louis Van gaal.

Rojo ambaye alichaguliwa katika kikosi bora cha kombe la dunia, amejiunga na United kwa ada ya uhamisho wa £16 pamoja na Luis Nani kwenda Sporting kwa mkopo. Manchester United wanaripotiwa kuhamishia nguvu zao kwa Angel di Maria wa Real Madrid.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI