Baada ya usajili wa Ander Herrera na Luke Shaw, klabu ya Manchester United leo hii imekamisha usajili wa mchezaji mwingine. Marcos Rojo, beki wa kiargentina aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya Sporting Lisbon amethibitishwa rasmi kujiunga na kikosi cha Louis Van gaal.
Rojo ambaye alichaguliwa katika kikosi bora cha kombe la dunia, amejiunga na United kwa ada ya uhamisho wa £16 pamoja na Luis Nani kwenda Sporting kwa mkopo. Manchester United wanaripotiwa kuhamishia nguvu zao kwa Angel di Maria wa Real Madrid.
0 comments:
Post a Comment