Sunday, August 17, 2014

Coutinho, Yondani wampasua kichwa Maximo


Sweetbert Lukonge na Goodluck Ngai
KOCHA Mkuu wa Yanga, Marcio Maximo, amejikuta akitumbukia katika lindi la mawazo baada ya kuwakosa mazoezini nyota wake, Andrey Coutinho na Kelvin Yondani.
Wachezaji hao kwa pamoja jana walishindwa kufanya mazoezi na wenzao ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara kutokana na kusumbuliwa na maradhi mbalimbali.
Hali hiyo imemfanya Maximo aonekane kuwa ni mwenye mawazo mengi kutokana na kutojua siku ambayo wachezaji hao ambao ni kati ya nyota wake wa kutumainiwa, watarudi uwanjani kuendelea na kazi yao.

Kelvin Yondani.
Daktari wa Yanga, Juma Sufiani, ameliambia Championi Jumamosi kuwa, wachezaji hao ni wagonjwa, ndiyo maana katika mazoezi ya jana hawakuweza kuonekana uwanjani.
Alisema Coutinho ambaye amejiunga na klabu hiyo hivi karibuni akitokea nchini Brazil, anasumbuliwa na maumivu ya mgongo wakati Yondani anasumbuliwa na Malaria.
“Hata hivyo, kwa sasa wanaendelea vizuri baada ya kupatiwa matibabu, hivyo ni matumaini yetu kuwa watarudi uwanjani hivi karibuni kabla ya safari yetu ya kisiwani Pemba,” alisema Sufiani.
Kikosi hicho cha Yanga kinatarajia kuondoka Dar es Salaam manmo keshokutwa Jumatatu kwenda Pemba kwa ajili ya kupiga kambi ya siku 10 ya kujiandaa na msimu ujao wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Septemba 20, mwaka huu.

Na mdadisiblog/festosaimon

Credit gpl

WASTARA AOLEWA NA MWANAUME ASIYEMJUA

HiSTORIA KWA UFUPI
Wastara alizaliwa mwaka 1983 katika Hospitali ya Turiani iliyopo wilayani Mvomero mkoani Morogoro akiwa ni mtoto wa tano kati ya saba waliozaliwa katika familia yao.

Staa katika tasnia ya filamu Bongo,Wastara Juma.
Alisoma Shule ya Msingi Mvomero na baada ya kuhitimu darasa la saba alijiunga na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Kibamba Agriculture ambapo alipofika kidato cha pili aliacha shule.
MATUKIO YA UTOTONI
Mwandishi: Unakumbuka utotoni mwako ni matukio gani ya hatari ambayo ulikuwa ukiyafanya?
“Nilikuwa naparamia miti ya miembe, mikorosho kama sina akili nzuri huko nilikuwa nafuata pia ngedere kwani nilikuwa nawapenda sana, nakumbuka nilishawahi kuvunjika miguu yote pia kuvunjika mkono wa kulia kwa kuparamia miti.”
SABABU ZA KUACHA SHULE
Mwandishi: Umesema uliacha shule ukiwa kidato cha pili, nini sababu?
“Niliacha shule baada ya rafiki yangu kuiba hela nyumbani kwao ambapo alikuwa anakuja nazo shuleni tunakula wote chips,
wazazi wake walipogundua wakaja kushtaki shuleni nikawa natafutwa ili nisimamishwe mbele ya wanafunzi wote nieleze na kuchapwa, nilipogundua hivyo sikwenda tena shuleni maana nilikuwa nina aibu sana.”
AUZA MADUKA
Mwandishi: Je, baada ya kuacha shule ulienda wapi?
“Mama yangu alikuwa mfanyabiashara, alikuwa na duka la nguo na lingine la kuuza madini hivyo nilienda kumsaidia kwenye maduka hayo.”
Mwandishi: Ulifanya hizo biashara kwa muda gani?
APATA MCHUMBA
“Nilifanya kwa muda wa miezi mitatu nikapatiwa mchumba nikaolewa japokuwa nilikuwa simpendi.’’
Mwandishi: Sasa ilikuwaje ukaolewa na mwanaume usiyempenda?
“Nakumbuka nilikuwa na miaka kumi na sita na sikuwahi hata kumuona wala kuzungumza na huyo mwanaume kabla ya ndoa,
alienda moja kwa moja kwa mama yangu wakakubaliana na wakati huo wazazi wakishaamua huwezi kupinga ,hivyo nililazimika kuolewa hivyohivyo kwani mama yangu alikuwa akiogopa aibu ya kuzalia nyumbani kwa vile kwa mila zetu sisi Waarabu ukiwa na miaka hiyo msichana unaonekana ni mkubwa na unastahili kuolewa.”(Wastara baba yake alikuwa Mwaarabu.)
MUME AMZIDI UMRI
Mwandishi: Huyo mwanaume wako mlikuwa mnalingana naye umri au alikuzidi?
“Mwanaume alikuwa mkubwa sana kwangu hivyo kutokana na udogo niliokuwa nao sikuwa najua nini maana ya ndoa kitu nilichokuwa najua kufanya ni usafi tu, suala la mapenzi ndiyo lilikuwa ni shughuli haswa kwani nilikuwa sijui.”
TENDO LA NDOA
Mwandishi: Sasa mumeo alipokuwa akitaka haki ya ndoa ulikuwa unafanyaje?
“Ilikuwa ni kama tunapigana wakati huo ukifika na nilipopata ujauzito sikutaka hata aniguse hivyo mpaka mtoto anazaliwa sikushiriki tena tendo la ndoa na huyo mwanaume kwani nilikuwa namwambia kwamba naumia.”
MAISHA MAGUMU
Mwandishi: Vipi sasa maisha ya ndoa yalikuwaje?
“Maisha yalikuwa magumu sana kwani mwanaume aliyenioa hakuwa na kazi ya aina yoyote na mama hakuligundua hilo, baada ya kunioa alikuwa anaenda kushinda nyumbani kwao ndiyo ndugu zake wakawa wanatupatia chakula na kutulipia kodi.
“Baada ya kuwa na ujauzito wazazi wake walinichukua, nikaenda kukaa nao Zanzibar lakini nikawa nateseka sana ambapo mama yangu aligundua na kusema nije Dar kwani anataka kuniona na kipindi hicho alikuwa anaumwa, nilikuja kwa mama aliponiona alihuzunika sana kwani nilikuwa nimedhoofika.

Teknolojia: Ifahamu Smartphone ya kwanza duniani ‘IBM Simon’ inayotimiza miaka 20 (picha)

Naamini ni wengi wanaomiliki simu za kisasa ‘smartphones’ ambazo zinaendana na teknolojia ya sasa iliyozidi kurahisisha maisha ya
mwanadamu kupitia simu hiyo ya kiganjani.Lakini yawezekana si wote ambao wanaifahamu
‘smartphone’ ya kwanza kuingia sokoni.


Smartphone ni nini?
Ni simu ya mkononi ambayo inauwezo wa kufanya mambo mengi yanayofanywa nakompyuta.

Smartphone ya kwanza

IBM Simon ndio ilikuwa ‘Smartphone’ ya kwanza duniani iliyoenda sokoni Agosti 16,
1994 na jan Agosti 16, 2014 ilitimiza miaka 20.

Hata hivyo IBM Simon ilikuwa haiitwi ‘Smartphone’ kipindi hicho, lakini ilikuwa na ‘features’ nyingi zilizoko kwenye ‘Smartphone’
za sasa.

“But it had a lot of the features we see today. It had a calendar, it could take notes and send emails and messages and combined all of this with a cell phone.” amesema Charlotte Connelly ambaye ni content developer wa makumbusho ya sayansi ya London.

IBM Simon ilikuwa na uzito wa gram 500. “It looks like a grey block but it’s not as big as
you’d imagine, It had a stylus and a green LCD screen, which is similar in size to the iPhone 4. In fact, it’s not a bad looking thing.”Aliongeza ms Connelly.

Charlotte Connelly, content developer wa makumbusho ya sayansi ya London.


Hata hivyo inasemekana ukubwa wa bei (kwa wakati huo) pamoja na maisha mafupi ya betri ni miongoni mwa sababu za kupotea haraka kwa simu hizo sokoni ndani ya miaka miwili baada ya kuzinduliwa.

IBM Simon ilikuwa ikiuzwa $899, na hapakuwa na internet ya simu wakati huo hivyo haikufanya vizuri. Ziliuzwa simu 50,000 tu na nyingi zilinunuliwa na wafanyabiashara.

Motorola ya 1984 (kushoto), IBM Simon ya 1994 (katikati) na simu za sasa 2014 (kulia)

Katika kuadhimisha miaka 20 ya IBM Simon,Makumbusho ya sayansi ya London, wataiweka
simu hiyo kama sehemu ya maonesho ya ‘Information Age’ mwezi Octoba mwaka huu.
IBM Simon ilitengenezwa na kampuni ya IBM pamoja na kampuni ya simu ya Marekani,
BellSouth. IBM wamesema waliita Simon kwasababu ilikuwa simple na iliweza kufanya karibu kitu
chochote mtu alichohitaji.

Na mdadisiblog/festosaimon

HUYU NDIE DJ WAKIKE ANAYETAMBA KWASASA HAPA TOWN....BAADA YA DJ FETY KUJIKITA ZAIDI KWENYE UTANGAZAJI

Anaitwa DJ.SINORITA...Cheki baadhi ya PIC zake hapa akiwa anawajibika!!!








Alikiba: Nawaomba watu wasinikosanishe na Diamond, sina ugomvi naye!

Alikiba anataka watu wafahamu kuwa hana na
tatizo na Diamond Platnumz na amewataka watu waache kuwakosanisha.

Akizungumza na mwandishi wetu jana, AliKiba amewataka watu kuachana na tabia ya
kuwagombanisha Diamond ili wafanye muziki mzuri.

“Kila mtu anaandika anachotaka juu ya mimi na Diamond, mpaka wengine wanatumia akaunti
fake za Facebook kutukosanisha, ndio maana nikasema kuna wengine wanafanya for fun na
wengine wanafanya ili kutukosanisha wengine
wanafanya lakini hawajui wanachofanya,”amesema Alikiba.
“Mimi najaribu kuwaomba wadau mbalimbali waache hiyo tabia ya kutukosanisha kwa sababu
mimi sina ugomvi na Diamond na wala sina mambo hayo.

Ninachowataka waendelee
kusupport kazi zetu ili mambo yaende vizuri kwa sababu sisi ndo wasanii wao tunaoiwakilisha Tanzania. Wanapotupa moyo
wao sisi tunazidi kukaza buti ili tufike mbali zaidi.

Watu wanaotengeneza ugomvi wangu na Diamond waache cha zaidi wafanye kusupport
muziki na watuambie ni mapungufu gani ambayo yamepungua ili tujirekebishe,”
ameongeza. Katika hatua nyingine, Alikiba amezungumzia
mapokezi ya wimbo Mwana na Kimasomaso pamoja na ujio wa video zake.

“Kwanza watu wamenipokea vizuri sana kama nilivyokuwa nikitarajia, imeonyesha ni jinsi gani yale malalamiko ya maana walikuwa
wakilalamika kwamba nimekumiss na nilivyotoa nyimbo watu wanasikiliza na kuinjoy na nyimbo
zenyewe zimekuja wakati mzuri na zenye maadili mazuri ya kuelimisha na kuchezeka na
ya kufurahisha.

Maandalizi ya video yapo tayari
na booking ipo tayari vilevile, maandalizi nimeandaa hata kabla sijatoa nyimbo, video itafanyika nje na moja ni hapa siwezi sema ni
nchi gani bado ni mapema nitasema baadae nikishaitoa, kwasababu nimetoa track mbili
moja itafanyika hapa na nyingine itafanyika nje.”

LIVERPOOL YASAJILI BONGE LA BEKI LA HISPANIA

BEKI wa pembeni wa Hispania, Alberto Moreno amesaini Liverpool kwa ada ya Pauni Milioni 12.

Makubaliano ya uhamisho huo yalifikiwa mapema wiki hii, lakini ikachukua muda hadi sasa klabu hiyo inamtambulisha rasmi mchezaji huyo.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekuwa akifanya vizuri kwa miaka miwili iliyopita - ikiwa ni pamoja na kuwamo kwenye kikosi cha U21 cha Hispania kiloichochukua ubingwa wa Ulaya mwaka 2013, na kung'ara Sevilla. Moreno alishinda taji la Europa League na Sevilla msimu uliopita na alimwaga machozi baada ya kufungwa na Real Madrid katika mechi ya UEFA Super Jumanne.

Na mdadisiblog/festosaimon
 
ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILI TUNAOMBA UJIUNGE NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

Angalia picha Wasanii walivo wawasili Dodoma katika Kili Music Tour

DJ Choka ingawa hatujui mkoba aliobeba ni wa nani kati ya Mwasiti, Khadija Kopa au Shilole
Shilole akieleza alivyojipanga. Pembeni yake ni DJ Choka
Ben Pol ambaye ni mwenyeji wa wasanii wote akiongea
Joh Makini baada ya kuwasili jijini Dodoma
Joh Makini akisikiliza moja ya maswali toka kwa tangazaji wa Dodoma FM
Izzo Bizness katika interview
Wasanii wakisubiri kuingia studio za ABM FM
Rich Mavoko akifanyiwa mahojiano ndani ya Dodoma FM
Malkia wa mipasho Khadija Kopa akiimba moja ya vibwagizo vya wimbo wake

Hatimaye wakali watakaopanda jukwaani Agosti 16 wamewasili mkoani Dodoma salama salmini.

Wasanii hao waliwasili kwa basi maalum linalotumika katika ziara hiyo mchana na kwenda moja kwa moja katika mahojiano ya moja kwa moja katika vituo vya redio vya mkoani Dodoma. Wakihojiwa kwa nyakati tofauti wasanii hao wamewahakikishia mashabiki kuwa wamejipanga vizuri kulishambulia jukwaa.

Wasanii wanaotarajiwa kupanda jukwaani ni Mwasiti, Khadija Kopa, Shilole, Izzo Bizness, Rich Mavoko, Christian Bella, Madee, MwanaFA na Weusi.

 BONYEZA HAPA KAMA BADO UJAUNGANA NA BLOG HII 

Saturday, August 16, 2014

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, SPURS NAYO YAUA MTU

Alexis Sanchez akiwatoka mabeki wa Crystal Palace
Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza Aaron Ramsey baada ya kufunga bao la ushindi

BAO la dakika ya 90 na ushei la Aaron Ramsey limeipa mwanzo mzuri Arsenal katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa 2-1 Crystal Palace kwenye Uwanja wa Emirates, London.

Ilibaki kidogo tu Gunners kuanza kwa sare baada ya Crystal kutangulia kupata bao kupitia kwa Brede Hangeland dakika ya 35 kabla ya Laurent Koscielny kuisawazishia Arsenal dakika ya 45 na ushei.

Refa Jon Moss alimtoa nje kwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu Jason Puncheon wa Crystal Palace dakika ya 88 baada ya kumchezea rafu Monreal.

Kikois cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Debuchy, Chambers, Koscielny, Gibbs/Monreal dk53, Wilshere/Oxlade-Chamberlain dk69, Arteta, Sanchez, Ramsey, Cazorla, Sanogo/ Giroud dk62. Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann/Delaney dk75, Hangeland, Ward, Puncheon, Jedinak, Ledley, Bolasie/O'Keefe dk90, Chamakh na Campbell/Gayle dk85.

Katika mechi nyingine za ufunguzi leo Ligi Kuu England, Stoke City imelala nyumbani 1-0 mbele ya Aston Villa, bao pekee la Andreas Weimann dakika ya 50 Uwanja wa Britannia, Leicester City imetoka sare ya 2- 2 na Everton, Queens Park Rangers imefungwa 1-0 nyumbani na Hull City, bao pekee la James Chester dakika ya 52 Uwanja wa Loftus Road, West Bromwich Albion imetoka 2-2 na Sunderland Uwanja wa The Hawthorns, West Ham United imefungwa 1-0 nyumbani na Tottenham Hotspur bao pekee la Eric Dier dakika ya 90 na ushei Uwanja wa Boleyn Ground, wakati Manchester United imefungwa 2-1 nyumbani na Swansea City.

Na mdadisiblog/festosaimon
 UNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI ZA KIMICHEZO ZAID BONYEZA HAPA  

AZAM FC YAUA 4-1 NA KWENDA ROBO FAINALI ILE KIBABE HASWA

AZAM FC imemaliza kwa ushindi mnono mechi za makundi, Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame baada ya kuifumua mabao 4-1 Adama City ya Ethiopia Uwanja wa Nyamirambo mjini hapa.

Kwa matokeo hayo Azam FC ya Tanzania Bara, imepanda kileleni mwa Kundi A kwa kufikisha pointi nane baada ya mechi nne, ikishinda mbili na sare mbili- hivyo kutinga Robo Fainali kibabe.

Rayon Sport ambayo hivi sasa inacheza na Atlabara ya Sudan Kusini, inaweza kupanda kileleni mwa kundi hilo iwapo itashinda. Dakika 45 za kwanza zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, Azam wakitangulia kupitia kwa Nahodha John Bocco ‘Adebayor’ akiunganisha krosi ya Khamis Mcha ‘Vialli’ kabla ya Desaleny Debesh kuisawazishia Adama dakika ya 39.

Refa Mohamed Hassan kutoka Somalia alikataa bao la Kipre Herman Tchetche dakika ya 42, akidai kipa alibughudhiwa na kipindi cha pili Azam iliingia na moto mkali na kufanikiwa kuongeza mabao matatu.

Alianza Didier Kavumbangu dakika ya 55, akimalizia krosi ya Erasto Nyoni akafuatia Khamis Mcha ‘Vialli’ dakika ya 60 baada ya kuuwahi mpira uliotemwa na kipa na Kipre Tchetche akamalizia dakika ya 74, krosi ya Nyoni.

Kocha Mcameroon Joseph Marous Omog alifurahia matokeo hayo na akasema sasa anajipanga kwa Robo Fainali. “Ushindi huu ni mzuri, nafurahi tunaingia Robo Fainali kwa kujiamini, sasa tunaelekeza nguvu zetu huko,”alisema.

Kikosi cha Azam FC; Mwadini Ali, Erasto Nyoni, Gardiel Michael/Said Mourad dk51, David Mwantika, Aggrey Morris, Kipre Balou, Khamis Mcha ‘Vialli’/Farid Mussa dk61, Salum Abubakar ‘Sure Boy’/Mudathir Yahya dk72, John Bocco ‘Adebayor’, Didier Kavumbangu na Kipre Tchetche. Adama City; Yakoub Fiseha/Yeraswork Terefe dk38, Suleiman Mohamed, Henok Gemtesa, Demetros Wisilase, Mintesinot Kebede, Wonooson Milkesa, Abreham Yisak, Ameha Belete, Abdulkerim Abafogi, Desaleny Debesh/ Abiy Beyene dk68 na Benyam Ayele.

Na mdadisiblog/festosaimon

 BONYEZA HAPA KUJIUNGA NASI UPATE HABARI KIRAHISI 

KOCHA MPYA, GUNDU PALE PALE MAN UNITED, YAFUMULIWA 2-1 NA SWANSEA OLD TRAFFORD UFUNGUZI LIGI KUU ENGLAND

Matatizo pale pale; Kocha Van Gaal kulia na Msaidizi wake, Ryan Giggs kushoto wakiwa hawaamini macho yao

KOCHA mpya matatizo yale yale Manchester United- hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mashetani hao Wekundu kuanza vibaya Ligi Kuu ya England kwa kuchapwa mabao 2-0 na Swansea City Uwanja wa Old Trafford. Mabao yaliyomfanya kocha Mholanzi, Louis Van Gaal aanze vibaya Ligi Kuu yamefungwa na Ki dakika ya 28 na Sigurdsson dakika ya 72, wakati Nahodha Wayne Rooney aliifungia United dakika ya 53. Kikosi cha Man Utd kilikuwa; De Gea; Jones, Smalling, Blackett, Lingard/Januzaj dk24, Fletcher, Herrera/Fellaini dk67, Young, Mata, Hernandez/Nani dk46 na Rooney. Swansea; Fabianski; Rangel, Amat, Williams, Taylor/Tiendalli, Ki, Shelvey, Routledge, Sigurdsson, Dyer/Montero dk67 na Bony/ Gomis dk77.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NA BLOG HII