Saturday, August 16, 2014

ARSENAL YAANZA VYEMA LIGI KUU ENGLAND, SPURS NAYO YAUA MTU

Alexis Sanchez akiwatoka mabeki wa Crystal Palace
Wachezaji wa Arsenal wakimpongeza Aaron Ramsey baada ya kufunga bao la ushindi

BAO la dakika ya 90 na ushei la Aaron Ramsey limeipa mwanzo mzuri Arsenal katika Ligi Kuu ya England, baada ya kuichapa 2-1 Crystal Palace kwenye Uwanja wa Emirates, London.

Ilibaki kidogo tu Gunners kuanza kwa sare baada ya Crystal kutangulia kupata bao kupitia kwa Brede Hangeland dakika ya 35 kabla ya Laurent Koscielny kuisawazishia Arsenal dakika ya 45 na ushei.

Refa Jon Moss alimtoa nje kwa kadi ya pili ya njano na kuwa nyekundu Jason Puncheon wa Crystal Palace dakika ya 88 baada ya kumchezea rafu Monreal.

Kikois cha Arsenal kilikuwa; Szczesny, Debuchy, Chambers, Koscielny, Gibbs/Monreal dk53, Wilshere/Oxlade-Chamberlain dk69, Arteta, Sanchez, Ramsey, Cazorla, Sanogo/ Giroud dk62. Crystal Palace: Speroni, Kelly, Dann/Delaney dk75, Hangeland, Ward, Puncheon, Jedinak, Ledley, Bolasie/O'Keefe dk90, Chamakh na Campbell/Gayle dk85.

Katika mechi nyingine za ufunguzi leo Ligi Kuu England, Stoke City imelala nyumbani 1-0 mbele ya Aston Villa, bao pekee la Andreas Weimann dakika ya 50 Uwanja wa Britannia, Leicester City imetoka sare ya 2- 2 na Everton, Queens Park Rangers imefungwa 1-0 nyumbani na Hull City, bao pekee la James Chester dakika ya 52 Uwanja wa Loftus Road, West Bromwich Albion imetoka 2-2 na Sunderland Uwanja wa The Hawthorns, West Ham United imefungwa 1-0 nyumbani na Tottenham Hotspur bao pekee la Eric Dier dakika ya 90 na ushei Uwanja wa Boleyn Ground, wakati Manchester United imefungwa 2-1 nyumbani na Swansea City.

Na mdadisiblog/festosaimon
 UNGANA NA BLOG HII ILI UPATE HABARI ZA KIMICHEZO ZAID BONYEZA HAPA  

0 comments:

Post a Comment