Thursday, August 14, 2014

JB FILAMU ZAKO NI NZURI ILA HIKI KITU KINAKERA KATIKA FILAMU ZAKO. JIREKEBISHE

Mimi sio mpenzi sana wa kuangalia filamu, ila mara chache tu huwa naangalia hasa kwenye mabasi ninaposafiri.

Kitu kinachonikera kwenye hizi Bongo movie hasa za JB ni kutumia wahusika wale wale na theme ile ile mwisho ana bore sasa.

Mfano ni huyu Shamsa Ford, huwezi kuangalia picha ya JB usimkute, tena kwenye filamu hiyo lazima ataishia kuolewa na JB. Ni kweli Shamsa ni mzuri, lakini kwani yuko pee yake kwenye filamu? Halafu kwa nini theme iwe mapenzi tu? Nachoka kabisa

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI 

Hutaamini ukiisikia sababu iliyomfanya Dogo Janja aache shule!

Rapper kutoka Arusha, Dogo Janja ameamua kuacha shule ili kusomea masomo ya muziki.

Akiongea na 255 ya kipindi cha XXL cha Clouds FM, Janjaro amedai kuwa usumbufualiokuwa akiupata shuleni ndio sababu kubwa iliyomfanya aache shule.

“Shule ambayo mimi nimesoma nilikuwa napata matatizo kwasababu kitu kidogo ambacho mnaweza mkafanya wote lakini wewe ukaonekana chanzo. ‘Msanii mhuni, huyu hivi,” alisema rapper huyo. “Sometimes unaweza ukawa unasoma watu wengi wako dirishani wanapita wanakuangalia. Au unaweza ukakosea.. yaani wanakuwa wewe ni mtu ambaye upo sahihi all the time.

Kwa mfano labda unajua zile za kushtukizwa ‘fulani jibu swali’ kila saa unaulizwa wewe,” aliongeza. “Kwahiyo unakuwa hakuna pale Uabdul, unakuwa unaweka Ujanjaro Udogojanja.

Kwasababu unajua ile kushtukizwa kila saa unakuwa unahisi kama mwalimu anakuandama sana. Au kwenye mtihani, mnaweza mkawa mnafanya wote mtihani lakini mwalimu anakuja kukusimamia wewe, anakukazia kinoma.” Nini mtazamo wako kuhusiana na sababu hiyo ya Dogo Janja iliyomfanya aache shule?

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA TUNAOMBA SUPPORT YAKO KWA KUBONYEZA HAPA 

ANGALIA BALE ALIVYOTOA PASI MARIDADI KWA RONALDO ALIYEFUNGA BAO DHIDI YA SEVILA

BONGE LA PASI ALILOTOA BALE KWA RONALDO.

JEURI YA FEDHA SIMBA SC, PHIRI AFIKISHIWA HOTELI LA BEI MBAYA DAR, ATAIGHARIMU KLABU SH 400,000 KWA USIKU MMOJA TU

Hoteli la bei chafu; Kocha Patrick Phiri kulia akisaini kitabu cha kuingi chumba katika hoteli ya Regency. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC, Collins Frisch

Na Prince Akbar, DAR ES SALAAM KOCHA Patrick Phiri amefikishiwa kwenye hoteli ambayo gharama ya chumba chake ni dola za Kimarekani 120 (karibu Sh. 200,000 za Tanzania) kwa siku- na wakala wake pia, amechukuliwa chumba cha hivyo.

Maana yake, malazi ya Phiri katika hoteli ya Regency, Dar es Salaam pamoja na wakala wake yataigharimu Simba SC wastani wa Sh. 400,000 kwa siku. Phiri anaweza kusaini Mkataba kesho na baada ya hapo wakala wake atarejea Zambia, naye kuendelea kuishi katika hoteli hiyo- na atapewa usafiri pia.

Haijulikani mshahara wa Phiri utakuwa kiasi gani, lakini mara ya mwisho aliondoka Simba SC akiwa analipwa dola za Kimarekani 5,000 (zaidi ya Sh. Milioni 7.5) kwa mwezi. Phiri amepokewa mchana wa leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam na kuwekwa kwenye gari la wazi juu akipitishwa mitaa ya Jiji la Dar es Salaam ili manazi wa timu hiyo wamuone, kabla ya kufikishwa Regency Hotel.

Kocha huyo bora wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2009/2010, kesho anatarajiwa kusaini Mkataba wa kuifundisha klabu yake hiyo ya zamani, Simba SC, akirithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyefukuzwa mwishoni mwa wiki.

Mzaliwa huyo wa Mei 3 mwaka 1956, alifanya kazi kwa awamu tatu tofauti akiwa na Wekundu hao wa Msimbazi kati ya mwaka 2004 na 2010 na kwa mafanikio makubwa- na sasa anataka kurejesha enzi za wana Simba ‘kutembea vifua wazi’.

Mzambia huyo alishinda mataji mawili ya Ligi Kuu akiwa na Simba SC, misimu ya 2004/2005 na 2009/2010 na pia alishinda Makombe ya Tusker mwaka 2005 la Tanzania na Kenya.

Phiri ni kocha anayekubalika zaidi mbele ya mashabiki wa Simba SC miongoni mwa makocha waliowahi kufundisha klabu hiyo- rekodi yake ya kukumbukwa zaidi ikiwa ni kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2009/2010 bila kufungwa hata mechi moja.

Lakini pia, namna alivyoweza kuiongoza Simba SC kuwatambia watani wa jadi, Yanga SC ni jambo lingine linalomfanya awe kocha mwenye heshima ya kipekee Msimbazi.

Katika awamu zote tatu alizofundisha Simba SC awali, Phiri hajawahi kufukuzwa- kwani amekuwa akiondoka mwenyewe kwa sababu mbalimbali.

Kwa sasa, mume huyo wa Cecilia Mutale waliyezaa naye watoto wawili, Melesianiah na Patrick Junior, anarejea Simba SC akitokea Green Buffaloes ya Ligi Kuu ya Zambia.

Phiri ni kocha mwenye mafanikio tangu anacheza soka katika klabu za Rokana United (sasa Nkana F.C.) na Red Arrows zote za nyumbani kwao, Zambia kama mshambuliaji. Alikuwemo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kilichocheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 1978 na 1982, kabla ya kuiwezesha Chipolopolo kufuzu kwa AFCON ya mwaka 2008 nchini Ghana. Akiwa kocha, Phiri pia aliiongoza timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 ya Zambia kucheza Fainali za kwanza kabisa za Kombe la Dunia nchini Nigeria mwaka 1997 kabla ya kushinda tuzo ya kocha bora wa mwaka nchini mwake mwaka 1999.

Simba SC Jumapili ilivunja mkataba na Mcroatia, Zdravko Logarusic ikiwa ni siku moja tu baada ya timu hiyo kufungwa mabao 3-0 na ZESCO ya Zambia katika mchezo wa kirafiki Jumamosi Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Loga ambaye aliongezewa Mkataba wa mwaka mmoja mwezi uliopita- inadaiwa amefukuzwa kwa sababu za kutotii miiko na maadili ya klabu na Rais wa klabu hiyo, Evans Aveva alisema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kumvumilia kwa kiasi cha kutosha.

Loga ameondoka Simba SC baada ya kuiongoza katika mechi 21 tangu Desemba mwaka jana, kati ya hizo akishinda nane, sare tano na kufungwa nane. Loga aliyerithi mikoba ya Mzalendo, Abdallah Athumani Seif ‘King Kibadeni’, aliikuta Simba SC bado ipo kwenye mbio za ubingwa msimu uliopita, lakini mwishowe ikamaliza nafasi ya nne nyuma ya Mbeya City, Yanga SC na Azam FC mabingwa.

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI UPATE HABARI KIRAHISI PUNDE TUWEKAPO MTANDAONI 

Wednesday, August 13, 2014

KIPENZI CHA WANA SIMBA SC, PATRICK PHIRI ALIPOWASILI DAR LEO KUREJESHA ENZI ZA UFALME MSIMBAZI

Kocha Phiri amerejea Msimbazi baada ya miaka minne
Anazungumza na Waandishi wa Habari
Kocha mpya wa Simba SC, Patrick Phiri akiwapungia mikono mashabiki wa timu hiyo baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam mchana wa leo tayari kusaini Mkataba wa kurithi mikoba ya Mcroatia, Zdravko Logarusic aliyevunjiwa Mkataba mwishoni mwa wiki.
Amepokewa kwa matarumbeta
Amepokewa kwa mashada ya maua

Kibonde, Gardner wapandishwa kizimbani kwa kosa la kusababisha ajali na kutoa lugha za matuzi

Watangazaji Ephraim Kibonde (wa kwanza kushoto) na mwenzake Gardner G Habash (wa pili kulia) wakielekea kizimbani.

Mtangazaji wa kipindi cha jioni cha Clouds FM, Jahazi, Ephraim Kibonde na mtangazaji wa
kipindi cha jioni cha Times FM ‘Maskani’, Gardner Habash, leo wamepandishwa kizimbani
katika Mahakama ya Wilaya Kinondoni jijini Dar es Salaam kwa kusababisha ajali na kudharau
amri ya polisi na kutoa lugha ya matusi.

Watangazaji hao wamesomewa mashitaka hayo na Wakili wa Serikali, Salim Mohammed mbele ya Hakimu Aniseta Wambura. Kibonde na Gadner wanadaiwa kutenda makosa hayo Jumamosi ya Agosti 9, mwaka huu saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.

Kesi yao imeahirishwa mpaka Septemba 10 mwaka huu itakaposikilizwa tena

Source:Global Publisher

 BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI ILI KILA TUKIPATA HABARI ZIKUFIKIE KIRAHISI 

DANTE, BOATENGE MABISHOO KINOMA, ONA WALICHOFANYA WAKATI WA KUPIGA PICHA

Mabeki wa Beyern Munich, Dante na Boateng wameonyesha wenyewe ni bonge ya mabisho. Wakati wakipiga picha ya pamoja ya kikosi, mabeki hao walizivuta jezi kwa nyuma, eti kisa zibane miili yao na SIX PAC zitokeee! Utaona picha inavyoonyesha namna mabeki hao walivyo mabishoo na wanavyotaka kuteka watoto, hahaha!

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA JIUNGE NASI KWA KUBONYA HAPA 

TFF HAITAMBUI MABADILIKO YA UONGOZI COASTAL UNION

SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limesema halitambui mabadiliko ya uongozi ndani ya Coastal Union yanayodaiwa kufanywa na mkutano wa wanachama wa klabu hiyo uliofanyika hivi karibuni.

TFF imesema uongozi wa Coastal Union uliochaguliwa na mkutano wa uchaguzi wa klabu hiyo ndiyo ambao wanautambua, na wataendelea kufanya nao kazi, na sio uongozi mwingine wowote ule.

“Tunapenda kuwakumbusha wanachama wetu (ikiwemo Coastal Union) kuheshimu katiba ya TFF pamoja na katiba zao, kwani hazitambui mapinduzi ya uongozi wala kamati za muda za utendaji.

TFF inafanya kazi za kamati za utendaji zilizopatikana kwa njia ya uchaguzi tu,”. “Tayari tumepokea barua kutoka kwa Kaimu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mnguto ikilalamikia kusimamishwa kwake,”.

“Hivyo, tunafuatilia suala hilo kwa kina, na ikibainika kuwa kuna viongozi wamehusika katika mapinduzi hayo watafikishwa katika vyombo husika kwa hatua zaidi,”imesema taarifa ya TFF.

Na mdadidiblog/festo saimon

 ASANTE KWA KUTEMBELEA BLOG HII ILA BONYEZA HAPA KUHUNGANA NASI 

Martino ni kocha mpya Argentina

Argentina imemteua aliyekuwa kocha wa Barcelona Gerardo Martino kuiongoza timu ya taifa baada ya kung'atuka kwa kocha wa zamani Alejandro Sabella.

Martino, 51, alifurushwa kutoka Barca mwisho wa msimu uliyopita baada ya kushindwa kushinda taji lolote kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 2007.

Aliwahi kuwa meneja wa Paraguay kati ya mwaka wa 2006 na 2011 alipowaongoza kufuzu kwa robo fainali ya kombe la dunia la 2010 .

kocha wa zamani Sabella aliondoka baada ya kushindwa kwa bao moja kwa nunge na Ujerumani katika fainali ya kombe la dunia huko Brazil.

Martino alimrithi kocha wa zamani wa Braca Tito Vilanova mwezi Julai 2013,Camp Nou baada ya kutia sahihi kandarasi ya miaka 2 .

Katika kipindi hicho Barca ilisajili ushindi katika mechi 40 kati ya 59 alizokuwa kocha lakini wakashindwa kusajili ushindi wowote wa tuzo la bara ulaya. Argentina imemteua aliyekuwa kocha wa Barcelona Gerardo Martino kurithi nafasi yake Alejandro Sabella Barcelona ilishindwa na Atletico Madrid katika hatua ya robo fainali ya kombe la mabingwa barani Afrika.

The Catalans walishindwa tena na vibonde wao Real Madrid katika fainali ya kuwania kombe la Copa del Rey. Punde baada ya kuondoka kwake Camp Nou Barcelona,ilimteua Luis Enriqueas kurithi nafasi yake. Atajulishwa rasmi hapo kesho (Alhamisi) kama mkufunzi wa Argentina.